HOJA Ni kweli baadhi ya mali za Kambuni ya The Guardian Ltd zinapigwa mnada?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Umeandika vyema sana! Tena sana!
Mzee anaoa binti mhuni muda ambao angekuwa amewaimarisha watoto kwenye usimamizi wa biashara.

Yaani alipifikisha tu miaka 50 alipaswa, huku akiwa amewajua uwezo wa watoto wake vyema - alipaswa kuwakabidhi mambo mengi ya usimamizi wa biashara.

Sasa mpaka miaka ya uzeeni anahangaika kutongoza na kubembeleza vitoto.
 
Kumbe kuna kesi ya fidia.. Zinauzwa kufidia malimbikizo ya fidia
 
Hata na hivyo

Sasa hizo mali zikiuzwa hiyo pesa anapewa yote huyo bwana nyari au inakuaje 🤔

Halafu kina nyari sio ndg zako min -me mnataka kuwafilisi wamachame hifihifi meku 😂
 
Shida ya wanaume wa jamii yetu, akipata mali nyingi badala ya kuandaa kizazi kijacho kuziendeleza,anaenda kuzaa na wadada warembo wa mjini. Kwa hili,marehemu hakwepi lawama.
 
Hapa mnamsingizia tu Mjane, biashara zake nyingi ikiwemo media ilianza kuwa changamoto
Mnamsingizia bure huyo Mjane. Kabla hata hajamuoa tayari kulikuwa kuna ushindani mkubwa kwenye biashara ya media na IPP media hawakuendana na mabadiliko yale. Hata viwanda vyake havikuongezeka ikiwemo kuuza kimoja kwa Subhash Patel. Mmesahau, kulikuwa pia hapo nyuma na malalamiko ya mishahara kwa watumishi wa the guardian limited.
 
Ameoa huyo Dada tayari ana 60+. Kabla hajaoa tayari Watoto wake walikuwa na 40+, mpaka hapo mlitaka awafundishe kipi kipya. Jack hakuwa akiendesha biashara, katika biashara zake walikuwepo haohao Watoto wake, mnamlaumu vipi! Yaani mlitaka Mtu asile maisha, afungue mafaili kila siku mpaka afariki!!
 
Kama kawaida wabongo always looking for someone blame..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…