HOJA Ni kweli baadhi ya mali za Kambuni ya The Guardian Ltd zinapigwa mnada?

HOJA Ni kweli baadhi ya mali za Kambuni ya The Guardian Ltd zinapigwa mnada?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kwanza Mzee Mengi marehemu naona alikosea kwenda kuoa yule sistaduu, pale ndipo alipojifungulia mlango wa kifo na haya mabalaa mengine ya mnada kufuatia.

Wale watoto wake wakubwa wawili angewapa a,b,c, za kusimamia mali zake, azigawanye yupi asimamie ipi, na mwingine ipi. Sidhani kama alifanya hivyo.

Amekuja kuondoka matokeo yake watoto wakubwa badala ya kupoteza muda kusimamia biashara za baba yao, wanajikuta wanahangaikia kesi za mirathi za yule sistaduu.
Umeandika vyema sana! Tena sana!
Mzee anaoa binti mhuni muda ambao angekuwa amewaimarisha watoto kwenye usimamizi wa biashara.

Yaani alipifikisha tu miaka 50 alipaswa, huku akiwa amewajua uwezo wa watoto wake vyema - alipaswa kuwakabidhi mambo mengi ya usimamizi wa biashara.

Sasa mpaka miaka ya uzeeni anahangaika kutongoza na kubembeleza vitoto.
 
Wana JF, kumekuwa na kipeperushi hiki kinasambaa mitandaoni na kwenye magazeti (kama inavyoonekana hapo chini) kikionesha tangazo la mnada wa hadhara wa mali za kampuni kongwe ya uchapishaji nchini, The Guardian Limited.

Hili ni jambo ambalo limenishtua na kunifikirisha sana kuhusu hatima ya makampuni makubwa ya wazawa pindi waasisi wao wanapotangulia mbele za haki.

Historia Fupi ya The Guardian Limited
Kama wengi tunavyofahamu, The Guardian Limited ni sehemu ya himaya kubwa ya vyombo vya habari ya IPP Media iliyoasisiwa na marehemu Dkt. Reginald Mengi.

Kampuni hii imekuwa kinara katika tasnia ya habari nchini Tanzania kwa miongo kadhaa, ikichapisha magazeti maarufu na yenye ushawishi mkubwa kama The Guardian (kwa lugha ya Kiingereza) na Nipashe (kwa Kiswahili). Imekuwa shule na kimbilio la waandishi wengi nguli hapa nchini na kujenga heshima kubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kuhusu Kesi na Tangazo la Mnada
Ukisoma kwa makini tangazo hilo lililotolewa na kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart Limited kwenye picha, inaonekana wazi kuwa hii inatokana na amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa ufupi:
Aliyeshinda Kesi (Decree Holder): Justine Nyari.

Wanaodaiwa (Judgement Debtors): The Guardian Limited (Mdaiwa wa 1) na Printa Afrique Limited (Mdaiwa wa 2).

Namba ya Kesi: Kesi ya Utekelezaji (Execution Case) Na. 6005/2024 iliyotokana na Kesi ya Madai Na. 35/2021.

Mali Zinazopigwa Mnada: Majengo mawili yaliyopo Mikocheni; Jengo moja la ofisi/utawala na jengo jingine ambalo ni ghala (Godown), kwenye kiwanja Na. 122. Eneo hili lipo jirani kabisa na ofisi za ITV na Radio One.

Tarehe ya Mnada: Ijumaa ya tarehe 25 Septemba, 2026 kuanzia saa nne asubuhi.
Kwa amri hii ya mahakama, inamaanisha The Guardian Ltd imeshindwa kulipa deni au kutekeleza hukumu iliyotolewa dhidi yao tangu kesi ya msingi ya mwaka 2021, mpaka kufikia hatua ya mali zake kushikiliwa na kupigwa mnada.

Utajiri wa Dkt. Mengi na "Kashkash" Tangu Kifo Chake
Dkt. Reginald Mengi alikuwa mmoja wa mabilionea na matajiri wakubwa kuwahi kutokea Afrika Mashariki. Utajiri wake ulitokana na viwanda, uchimbaji madini, na utengenezaji wa vinywaji kupitia IPP Group of Companies. Alikuwa mfanyabiashara anayeheshimika sana, mkarimu, na aliyesaidia makundi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu.

Hata hivyo, tangu Dkt. Mengi afariki dunia mwezi Mei 2019 kule Dubai, kumekuwa na wingu zito (kashkash) linaloikabili familia yake na himaya ya biashara aliyoiacha.

Tumekuwa mashahidi wa migogoro mikubwa ya kisheria iliyogonga vichwa vya habari, hasa kuhusu urithi na usimamizi wa mali zake.

Kulikumbwa na mvutano mkali mahakamani kati ya watoto wake wakubwa (Abdiel na Regina Mengi) na mjane wake (Jacqueline Mengi) kuhusu uhalali wa wosia ulioachwa, ambapo mahakama hatimaye ilitengua wosia uliokuwa ukimpa mali zote mjane huyo na watoto wake pacha.

Kuona tangazo hili la mnada leo, kunazua maswali mengi:

Je, migogoro ya kifamilia imeanza kuathiri uendeshaji na ustawi wa makampuni haya?

Kampuni kubwa kama The Guardian Ltd kufikia hatua ya kupigiwa mnada majengo yake ya utawala inaashiria mdororo mkubwa wa kifedha ndani ya kundi hili?

Je, hili ni tatizo la uongozi mpya ulioshindwa kuvaa viatu vya mwanzilishi, au ni changamoto za kibiashara zinazokumba sekta ya habari kwa ujumla?

Wana JF, mna mtazamo gani juu ya hili?
Kumbe kuna kesi ya fidia.. Zinauzwa kufidia malimbikizo ya fidia
 
Nani anasoma Magazeti siku hizi?

Hicho ni kifo cha asili cha biashara hasa ya magazeti. Baada ya hapo biashara inayofuata ni TV na Redio.

Ukiangalia kwa jicho zuri, makampuni ya TV, Redio na Magazeti mengi yanakwenda kufungwa na kuwa mufilisi (Bankruptcy).

Ujio wa teknolojia mpya ya habari unafanya hizi biashara kufa kifo cha asili. Ujio wa online TV, social media, simu janja umechukua nafasi, hakuna mtu siku hizi anakaa kuangalia habari saa mbili, watu wanapata habari kwenye simu zao hapo hapo. 😊

ITV, Capital TV, Capital radio, EATV wanachechemea, hata matangazo sijui kama wanapata. Wapeleke pesa kwingine, biashara ya habari za magazeti, TV na Redio haina future.

Wataendesha kwa hasara na mwisho watapiga mnada plants zao hizo kulipa madeni ya uendeshaji.
Hata na hivyo

Sasa hizo mali zikiuzwa hiyo pesa anapewa yote huyo bwana nyari au inakuaje 🤔

Halafu kina nyari sio ndg zako min -me mnataka kuwafilisi wamachame hifihifi meku 😂
 
Shida ya wanaume wa jamii yetu, akipata mali nyingi badala ya kuandaa kizazi kijacho kuziendeleza,anaenda kuzaa na wadada warembo wa mjini. Kwa hili,marehemu hakwepi lawama.
 
Kwanza Mzee Mengi marehemu naona alikosea kwenda kuoa yule sistaduu, pale ndipo alipojifungulia mlango wa kifo na haya mabalaa mengine ya mnada kufuatia.

Wale watoto wake wakubwa wawili angewapa a,b,c, za kusimamia mali zake, azigawanye yupi asimamie ipi, na mwingine ipi. Sidhani kama alifanya hivyo.

Amekuja kuondoka matokeo yake watoto wakubwa badala ya kupoteza muda kusimamia biashara za baba yao, wanajikuta wanahangaikia kesi za mirathi za yule sistaduu.
Hapa mnamsingizia tu Mjane, biashara zake nyingi ikiwemo media ilianza kuwa changamoto
Kwanza Mzee Mengi marehemu naona alikosea kwenda kuoa yule sistaduu, pale ndipo alipojifungulia mlango wa kifo na haya mabalaa mengine ya mnada kufuatia.

Wale watoto wake wakubwa wawili angewapa a,b,c, za kusimamia mali zake, azigawanye yupi asimamie ipi, na mwingine ipi. Sidhani kama alifanya hivyo.

Amekuja kuondoka matokeo yake watoto wakubwa badala ya kupoteza muda kusimamia biashara za baba yao, wanajikuta wanahangaikia kesi za mirathi za yule sistaduu.
Mnamsingizia bure huyo Mjane. Kabla hata hajamuoa tayari kulikuwa kuna ushindani mkubwa kwenye biashara ya media na IPP media hawakuendana na mabadiliko yale. Hata viwanda vyake havikuongezeka ikiwemo kuuza kimoja kwa Subhash Patel. Mmesahau, kulikuwa pia hapo nyuma na malalamiko ya mishahara kwa watumishi wa the guardian limited.
 
Umeandika vyema sana! Tena sana!
Mzee anaoa binti mhuni muda ambao angekuwa amewaimarisha watoto kwenye usimamizi wa biashara.

Yaani alipifikisha tu miaka 50 alipaswa, huku akiwa amewajua uwezo wa watoto wake vyema - alipaswa kuwakabidhi mambo mengi ya usimamizi wa biashara.

Sasa mpaka miaka ya uzeeni anahangaika kutongoza na kubembeleza vitoto.
Ameoa huyo Dada tayari ana 60+. Kabla hajaoa tayari Watoto wake walikuwa na 40+, mpaka hapo mlitaka awafundishe kipi kipya. Jack hakuwa akiendesha biashara, katika biashara zake walikuwepo haohao Watoto wake, mnamlaumu vipi! Yaani mlitaka Mtu asile maisha, afungue mafaili kila siku mpaka afariki!!
 
Kama kawaida wabongo always looking for someone blame..
 
Back
Top Bottom