Jana nilipata bahati ya kusikiliza clip moja ya Lema inayosema kuwa BAKWATA inamtazamo hasi na Chadema kwa kuwa kupitia maandamano ya Oktoba 29/25 BAKWATA inaamini Chadema walitaka kupindua serikali.Nimejiuliza na kama hao BAKWATA hawatakanusha basi
Nchi yetu inatengeneza moja moja la hatari mno na pia itaendelea kuleta mtizamo hasi kwenye teuzi.Najiuliza kuna uhusuano gani kati ya serikali ya sasa na BAKWATA hadi BAKWATA wawe na chuki ya moja kwa moja na Chadema kuliko watanzania wengine.
Je, Rais kuwa muislam kunaifanya BAKWATA kuwa karibu na serikali kuliko taasisi nyingine za dini?
Je, BAKWATA hawaoni kuwa kwa kuwa na huo mtazamo wanaleta migawanyiko ya kidini katika jamii?
Je, Rais akiwa mkristo TEC au CCT wajimilikishe serikali na kuvichukua vyama ambavyo havina viongozi wajuu wakristo?
Kwa nini sasa jamii isiamini kuwa kuna upendeleo wa kidini kiasi cha jumuia moja ya Dini kujimilikisha kiongozi kwa kuwa tu ni wa dini yake.
Bado naamini BAKWATA wanayo nafasi ya kulizungumza hili ili tuondoke hapa na tusijenge jamii ya hatari sana maana tunaweza amini kuwa hata vile vikundi vya akina Mwaipopo labda ni vya kidini.