Ni kweli Burundi ilitaka kuunganika na Tanganyika ilivyopata Uhuru na ingekuwa sehemu ya Tanganyika?

Ni kweli Burundi ilitaka kuunganika na Tanganyika ilivyopata Uhuru na ingekuwa sehemu ya Tanganyika?

Ingekua sehemu ya Tanganyika tu, afterall tulikua wamoja.

wakati wa ukoloni wa Mjerumani Burundi, Rwanda, Tanganyika na kieneo cha kionga triangle( Cabo Delgado msumbiji kwa sasa).
ilikua ni nchi moja ilokua inaitwa German East Africa.

Wakati wa vita ya kwanza ya dunia Belgium ( ubeligiji) colonizers wa Belgian Congo ( DRC) walilichua eneo la magharibi la GEA hadi tabora,

Na baada ya vita ya kwanza ya dunia kuisha palisainiwa Versailles treaty ambapo Mjerumani alinyanganywa koloni lake GEA na
Eneo la Rwanda-Burundi likachukuluwa na wabelgium,
Kionga triangle wakapewa Wareno (liko province ya Cabo Delgado msumbiji)

Eneo kubwa la GEA likapewa waingereza ndo hii nchi ya wezi Tanganyika.
 
Warundi ni ndugu zetu wa damu kabisa kuliko Wanyarwanda. I love these people. Hongereni sana Warundi kwa kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wenu.

Mwenyezi Mungu aendelee hivyo hivyo kuwajalia moyo wa kuwaona Watanganyika kama ndugu zenu wa damu. Hakika nyinyi ni watu msio na makuu, majivuno na kujimwambafai kama Wanyarwanda.
Wezi sana.
 
Jana Julai mosi, wananchi wa Burundi waliadhimisha miaka 60 tangu nchi yao ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Jumapili ya Julai mosi, 1962. Mwaka moja kabla ya siku ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi wa Umoja Mataifa na chama kilichoshinda katika uchaguzi huo UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore, aliyemuoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili.

Hata hivyo, Jumamosi ya Oktoba 13, 1962 Rwagasore aliyefikiriwa kuwa alikuwa anajenga uelewano wa kuishi pamoja kati ya Watutsi na Wahutu, aliuawa. Kifo chake kilikatisha ndoto ya shirikisho la Tanganyika na Burundi alilokuwa nalo Mwalimu Julius Nyerere.

Tanganyika ilipata uhuru Desemba 9, 1961 na baadaye ikawa Jamhuri Desemba 1962. Baada ya Uhuru wa Tanganyika katika hotuba yake kwa mkutano wa mwaka wa chama cha Tanu mwaka 1962, Mwalimu Nyerere alionyesha wazi kufadhaishwa kwake kulikotokana na mauaji ya Rwagasore.

Soma zaidi Gazeti la Mwananchi leo Jumamosi Julai 2,2022

View attachment 2280084
Wapigania Uhuru wengi wa Africa walikua na ndoto ya kuwa na nchi moja ya Africa.

Ila kiukweli ndoto hii n unrealistic.

Na hii ni moja ya motive ya Nyerere kuleta huu muungano wa kipumbavu uloiua Tanganyika. Afterall alikua anataka kuunganisha na Kenya pia

Kiasili sisi waafrica ni wabinafsi sana hii itabaki kuwa ndoto.

kama ikija kuwa kweli tukawa nchi moja basi dola ya afrika utavunika tuu.
asili ya viongozi wa kiafrica na sis waafrika wenyewe ni tamaa ya madaraka, ufisadi na rushwa na nepotism.
Hivi vinafanya muungano wowote wa waafrica kitaifa au hata kikanda kutokua na faida.
 
Back
Top Bottom