Ni kweli Cleopatra, mwanamke mrembo kuliko wote duniani alikuwa wa Misri?

flulanga ndiyo maana nikaandika kuwa inasadikika,na hizo zake ni za kusadikika,na wale siyo orijino!

Picha orijino peke yake ni hiyo ya kwenye picha ya sarafu hapo juu
 
Kipimo gani kilitumika kujua kwamba Yeye ndiyo Mrembo kuliko Warembo wote waliopo duniani? Kuna baadhi ya maandiko yanatudanganya sana Wanadamu.
....Yeye ameweka references ku support arguments zake, do the same please.
 
We mbinguni unapajua pako kona gani?
 
Inasadikika kuwa huyu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wote katika historia ya dunia.
Mkuu asante kwa hii, umenikumbusha mbali. Zamani watangazaji wa RTD walikuwa waajariwa form IV kwa kupimwa sauti tuu yaani voice test.

Mimi ni miongoni mwa watu tulioingia kwenye hii fani ya utangazaji kwa bahati mbaya, nikiwa A-Level Ilboru, nilipania kwenda chuo kusoma sheria, enzi hizo chuo kikuu ni kimoja tuu, UDSM, ili kusoma sheria lazima mtu upate Div 1 kali, na chuo kilikuwa kinachukua wanafunzi 60 tuu. Baada ya kuikosa div 1, mimi na form VI yangu nikaamua kwenda TSJ kusomea uandishi wa habari na utangazaji, nilipomaliza nikapostiwa RTD, nikapangwa idhaa ya Kiingereza, External Service. Kwa vile nilipenda sana muziki, nikaanzisha kipindi cha miziki na wanamuzi, nilikutana na changamoto kubwa, wanamuziki wengi wa Tanzania, hawajui Kiingereza, hivyo nilipata shida sana kufanya mahojiano ya Kiingereza. Zahir Alli Zorro ni mmoja wa wanamuziki wachache sana waliozungumza Kiingereza safi, hivyo nilifanya nae mahojiano, na moja ya nyimbo aliyovuma sana wakati huo ni hii ya Cleopatra, hivyo leo umenirudisha mbali kwenye enzi za ujana!.

Baadaye baada ya kuoa, mmoja wa mabinti zangu nimempa jina la Cleopatra, hivyo mimi ni Baba Cleopatra!.
Thanks for this!.
Paskali.
 
marinji

" Mark Anthony na Cleopatra
walijiua baada ya kushindwa
kwenye vita ya Actium na
Octavian!"
Huo mstari haumutaji Cleopatra moja kwa moja,ila hilo neno mfalme wa kusini linamanisha jeshi la Misri likiongozwa na Mark Anthony na Cleopatra,ambalo lilishindwa vita na Octavian mfalme wa kaskazini yaani Roma!
 
Nilikua nataka kuona picha ya huyo mwanamke nione kama anamzidi mama watoto wangu nadhani mngefuta kauli ya kumwita Cleopatra mzuri kuliko wote duniani
 
Mhembejr kama umekisoma kichwa cha habari vizuri,utaliona neno "kusadikika"...hivi unaelewa maana ya hilo neno?
 
troublemaker picha halisi ya Cleopatra ni hiyo sarafu hapo juu,picha zingine zote ni za kusadikika!

Ebu rudia kukisoma kichwa cha habari!
 
Hyo cleopatra hata picha hana?? Au story tu za nyani kuwa mtu?? Halafu hyo mark anthony ndo huyu huyu wa JLo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…