Ni kweli Cleopatra, mwanamke mrembo kuliko wote duniani alikuwa wa Misri?

Ni kweli Cleopatra, mwanamke mrembo kuliko wote duniani alikuwa wa Misri?

flulanga ndiyo maana nikaandika kuwa inasadikika,na hizo zake ni za kusadikika,na wale siyo orijino!

Picha orijino peke yake ni hiyo ya kwenye picha ya sarafu hapo juu
 
Kipimo gani kilitumika kujua kwamba Yeye ndiyo Mrembo kuliko Warembo wote waliopo duniani? Kuna baadhi ya maandiko yanatudanganya sana Wanadamu.
....Yeye ameweka references ku support arguments zake, do the same please.
 

Inasadikika kuwa huyu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wote katika historia ya dunia.


Ametajwa katika vitabu kadhaa ikiwemo Biblia na aliishi kwa miaka 39.


Cleopatra alikuwa ndiyo mtawala wa mwisho wa Kigiriki kutawala Misri na ndiyo aliyekuwa Farao
wa Kwanza wa kike mgeni.


Alizaliwa mwaka 69 na akiwa na miaka 18 akatawazwa kuwa Malkia.


Cleopatra ni neno la Kigiriki linalomanisha "baba yangu ni maarufu"
Cleopatra ni jina walilolopewa
mabinti kifalme wa kigiriki huku wale wa kiume wa kifalme
waliitwa Ptolemy.


Ptolemy alikuwa ni mmoja wa wale majenerali wanne wa
Alexander Mkuu,ndiyo hawa waliougawa ufalme wa Alexander katika falme nne!


Ptolemy ndiye aliyeanzisha utawala wa Kigiriki Misri na mji
wa Alexandria ndiyo ukawa makao makuu ya ufalme wake.


Hivyo Cleopatra huyu
tunayemzungumzia hapa
alikuwa ni Cleopatra wa Saba na wa mwisho.
Dola la Misri lilitawaliwa na Ugiriki tangu mwaka 323 baada ya Alexander Mkuu kuishinda Misri na utawala huu uliisha
mwaka 30 baada ya Cleopatra kujiua kwa kumruhusu nyoka
aina ya Cobra kumgonga kifuani.


Cleopatra alikuwa na mahusiano na wanaume wengi ila wale maarufu walikuwa ni Julius Caesar na Mark Anthony huyu
Caesar ndiye ambaye walizaa naye mtoto mmoja wa kiume.


Baada ya kifo cha Julius Caesar mwaka 44 mapenzi yakahamia
kwa Mark Anthony mnamo mwaka 42
Ili kuweza kutawala pekee yake Cleopatra alifanikiwa kuwaua wadogo zake wote,na
pia aliutumia uzuri wake kupata ulinzi wa kijeshi kutoka majemedari mashukhuri wa kipindi hicho!


Mathalani,kuna kipindi akiwa binti mbichi wa miaka 21 aliwaagiza watumishi wake wamviringishe kwenye zuria zuri na kulibeba kama zawadi na
kulipeleka kwa Julius Caesar!


Julius Caesar alipolifunua
akakutana na Cleopatra na hapo hapo akamfanya Cleopatra mchepuko wake.


Mark Anthony na Cleopatra walijiua baada ya kushindwa kwenye vita ya Actium na Octavian!


Huyu Octavian ndiye mtawala alietoa
amri ya Wayuhudi wote kwenda walikozaliwa wahesbiwe Sensa!


TUNAJIFUNZA NINI?


Uzuri,pesa,mali,na madaraka yatarahisisha maisha yetu ya duniani,ila hayotukufikisha mbinguni.


Ni kumtegemea Mungu tu ndiyo kutatufikisha mbinguni!


REFERRENCES:


1 Makabayo 10:57-58
Daniel 11:12
Luka 2:1-7
Antiquities of Jews by Josephus
Cleopatra and Anthony by
Shakespeare


ANGALIZO:
Miaka yote ni Kabla ya Kristo.

We mbinguni unapajua pako kona gani?
 

Inasadikika kuwa huyu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wote katika historia ya dunia.

Mkuu asante kwa hii, umenikumbusha mbali. Zamani watangazaji wa RTD walikuwa waajariwa form IV kwa kupimwa sauti tuu yaani voice test.

Mimi ni miongoni mwa watu tulioingia kwenye hii fani ya utangazaji kwa bahati mbaya, nikiwa A-Level Ilboru, nilipania kwenda chuo kusoma sheria, enzi hizo chuo kikuu ni kimoja tuu, UDSM, ili kusoma sheria lazima mtu upate Div 1 kali, na chuo kilikuwa kinachukua wanafunzi 60 tuu. Baada ya kuikosa div 1, mimi na form VI yangu nikaamua kwenda TSJ kusomea uandishi wa habari na utangazaji, nilipomaliza nikapostiwa RTD, nikapangwa idhaa ya Kiingereza, External Service. Kwa vile nilipenda sana muziki, nikaanzisha kipindi cha miziki na wanamuzi, nilikutana na changamoto kubwa, wanamuziki wengi wa Tanzania, hawajui Kiingereza, hivyo nilipata shida sana kufanya mahojiano ya Kiingereza. Zahir Alli Zorro ni mmoja wa wanamuziki wachache sana waliozungumza Kiingereza safi, hivyo nilifanya nae mahojiano, na moja ya nyimbo aliyovuma sana wakati huo ni hii ya Cleopatra, hivyo leo umenirudisha mbali kwenye enzi za ujana!.

Baadaye baada ya kuoa, mmoja wa mabinti zangu nimempa jina la Cleopatra, hivyo mimi ni Baba Cleopatra!.
Thanks for this!.
Paskali.
 
marinji

" Mark Anthony na Cleopatra
walijiua baada ya kushindwa
kwenye vita ya Actium na
Octavian!"
Huo mstari haumutaji Cleopatra moja kwa moja,ila hilo neno mfalme wa kusini linamanisha jeshi la Misri likiongozwa na Mark Anthony na Cleopatra,ambalo lilishindwa vita na Octavian mfalme wa kaskazini yaani Roma!
 
Nilikua nataka kuona picha ya huyo mwanamke nione kama anamzidi mama watoto wangu nadhani mngefuta kauli ya kumwita Cleopatra mzuri kuliko wote duniani
 
Mhembejr kama umekisoma kichwa cha habari vizuri,utaliona neno "kusadikika"...hivi unaelewa maana ya hilo neno?
 
troublemaker picha halisi ya Cleopatra ni hiyo sarafu hapo juu,picha zingine zote ni za kusadikika!

Ebu rudia kukisoma kichwa cha habari!
 
Hyo cleopatra hata picha hana?? Au story tu za nyani kuwa mtu?? Halafu hyo mark anthony ndo huyu huyu wa JLo??
 
Back
Top Bottom