Online Pastor
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 1,948
- 1,523
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee kuna rekodi nyingine huwa hazifutwi au kuvunjwa kutokana na muda kupita na kubakia kuwa historia. Inawezekana tungemchukua na kumlinganisha na warembo tulionao kipindi hiki cha 'kibongo flavor' pengine angekuwa si chochote lkn shida ni kuwa alishafariki na 'sifa' yake. Wanaosema alikuwa mzuri kuliko wote walimlinganisha na wengine waliokuwepo kipindi hicho hasa ukizingatia ktk historia mpaka leo hii hakuna mwanamke aliepiganisha watawala wa mataifa tofauti kutokana na uzuri wake... Yaani mfano anatokea binti bomba wa Zambia anamfuata Mh President hapa kwetu, amsaidie kuchukua uongozi Zambia mkulu anakubali kutokana na uzuri wa demu. Baadaye anaenda Rwanda anamkuta mkuu anamwambia Msumbiji wananisumbua kwenye mpaka, Rwanda wanatoa jeshi kupiga msumbiji. Katika historia ni Cleopatra pekee alieweza kugonganisha vichwa vya watawala. Abeid Pele anaitwa mchawi wa soka kwa kuwa alistaafu na sifa hiyo na atabaki nayo siku zote, lkn angecheza kipindi hiki cha kina Ronaldo, Messi na wengineo huenda hiyo sifa asingekuwa nayo. Mimi pia huwa sitaki kuamini kuwa huyo mwanamke alikuwa ndio hakuna tena duniani. Sio kweli ila ameibeba historia na itabaki kuwa hivyo... Labda atokee mwingine tusikie Trump na Putin wanapigana vita kwa sababu ya demu aliezaa na raisi wa Ufaransa ambaye nae alimpora waziri mkuu wa Canada, nae huyo wa Canada alimchukua kwa Waziri mkuu wa Israel. Na huyo demu ndio chanzo cha ugonvi wa Israel na Iran.... Halafu mwisho wanakwambia huyo demu pia amewahi kuwa na uhusiano na kiongozi wa ISIS ndio maana wanaripua mabomu, hapo habari za Cleopatra kidogo zitafunikwa japokuwa historia itabaki.Kipimo gani kilitumika kujua kwamba Yeye ndiyo Mrembo kuliko Warembo wote waliopo duniani? Kuna baadhi ya maandiko yanatudanganya sana Wanadamu.
Hahahahaaa atapata wapi picha yake?bila picha sawa na kipara bila hela
[emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419] [emoji419]Mwanamke mzuri kuliko wote ni mke wako
Inasadikika kuwa huyu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wote katika historia ya dunia.
Ametajwa katika vitabu kadhaa ikiwemo Biblia na aliishi kwa miaka 39.
Cleopatra alikuwa ndiyo mtawala wa mwisho wa Kigiriki kutawala Misri na ndiyo aliyekuwa Farao
wa Kwanza wa kike mgeni.
Alizaliwa mwaka 69 na akiwa na miaka 18 akatawazwa kuwa Malkia.
Cleopatra ni neno la Kigiriki linalomanisha "baba yangu ni maarufu"
Cleopatra ni jina walilolopewa
mabinti kifalme wa kigiriki huku wale wa kiume wa kifalme
waliitwa Ptolemy.
Ptolemy alikuwa ni mmoja wa wale majenerali wanne wa
Alexander Mkuu,ndiyo hawa waliougawa ufalme wa Alexander katika falme nne!
Ptolemy ndiye aliyeanzisha utawala wa Kigiriki Misri na mji
wa Alexandria ndiyo ukawa makao makuu ya ufalme wake.
Hivyo Cleopatra huyu
tunayemzungumzia hapa
alikuwa ni Cleopatra wa Saba na wa mwisho.
Dola la Misri lilitawaliwa na Ugiriki tangu mwaka 323 baada ya Alexander Mkuu kuishinda Misri na utawala huu uliisha
mwaka 30 baada ya Cleopatra kujiua kwa kumruhusu nyoka
aina ya Cobra kumgonga kifuani.
Cleopatra alikuwa na mahusiano na wanaume wengi ila wale maarufu walikuwa ni Julius Caesar na Mark Anthony huyu
Caesar ndiye ambaye walizaa naye mtoto mmoja wa kiume.
Baada ya kifo cha Julius Caesar mwaka 44 mapenzi yakahamia
kwa Mark Anthony mnamo mwaka 42
Ili kuweza kutawala pekee yake Cleopatra alifanikiwa kuwaua wadogo zake wote,na
pia aliutumia uzuri wake kupata ulinzi wa kijeshi kutoka majemedari mashukhuri wa kipindi hicho!
Mathalani,kuna kipindi akiwa binti mbichi wa miaka 21 aliwaagiza watumishi wake wamviringishe kwenye zuria zuri na kulibeba kama zawadi na
kulipeleka kwa Julius Caesar!
Julius Caesar alipolifunua
akakutana na Cleopatra na hapo hapo akamfanya Cleopatra mchepuko wake.
Mark Anthony na Cleopatra walijiua baada ya kushindwa kwenye vita ya Actium na Octavian!
Huyu Octavian ndiye mtawala alietoa
amri ya Wayuhudi wote kwenda walikozaliwa wahesbiwe Sensa!
TUNAJIFUNZA NINI?
Uzuri,pesa,mali,na madaraka yatarahisisha maisha yetu ya duniani,ila hayotukufikisha mbinguni.
Ni kumtegemea Mungu tu ndiyo kutatufikisha mbinguni!
REFERRENCES:
1 Makabayo 10:57-58
Daniel 11:12
Luka 2:1-7
Antiquities of Jews by Josephus
Cleopatra and Anthony by
Shakespeare
ANGALIZO:
Miaka yote ni Kabla ya Kristo.
mkuu umenifurahisha sana aiseeAisee kuna rekodi nyingine huwa hazifutwi au kuvunjwa kutokana na muda kupita na kubakia kuwa historia. Inawezekana tungemchukua na kumlinganisha na warembo tulionao kipindi hiki cha 'kibongo flavor' pengine angekuwa si chochote lkn shida ni kuwa alishafariki na 'sifa' yake. Wanaosema alikuwa mzuri kuliko wote walimlinganisha na wengine waliokuwepo kipindi hicho hasa ukizingatia ktk historia mpaka leo hii hakuna mwanamke aliepiganisha watawala wa mataifa tofauti kutokana na uzuri wake... Yaani mfano anatokea binti bomba wa Zambia anamfuata Mh President hapa kwetu, amsaidie kuchukua uongozi Zambia mkulu anakubali kutokana na uzuri wa demu. Baadaye anaenda Rwanda anamkuta mkuu anamwambia Msumbiji wananisumbua kwenye mpaka, Rwanda wanatoa jeshi kupiga msumbiji. Katika historia ni Cleopatra pekee alieweza kugonganisha vichwa vya watawala. Abeid Pele anaitwa mchawi wa soka kwa kuwa alistaafu na sifa hiyo na atabaki nayo siku zote, lkn angecheza kipindi hiki cha kina Ronaldo, Messi na wengineo huenda hiyo sifa asingekuwa nayo. Mimi pia huwa sitaki kuamini kuwa huyo mwanamke alikuwa ndio hakuna tena duniani. Sio kweli ila ameibeba historia na itabaki kuwa hivyo... Labda atokee mwingine tusikie Trump na Putin wanapigana vita kwa sababu ya demu aliezaa na raisi wa Ufaransa ambaye nae alimpora waziri mkuu wa Canada, nae huyo wa Canada alimchukua kwa Waziri mkuu wa Israel. Na huyo demu ndio chanzo cha ugonvi wa Israel na Iran.... Halafu mwisho wanakwambia huyo demu pia amewahi kuwa na uhusiano na kiongozi wa ISIS ndio maana wanaripua mabomu, hapo habari za Cleopatra kidogo zitafunikwa japokuwa historia itabaki.