Ni kweli Diamond Platnumz anatumia unga/madawa ya kulevya?

Ni kweli Diamond Platnumz anatumia unga/madawa ya kulevya?

Kwani muandiko mzuri unaliwa? Kama muandiko mzuri ungekuwa dili graduates wasingesaga soli kitaa na vyeti vyao...
Jibu murua kabisa mkuu. Kijana katoka Umakondeni na Elimu ndogo na ametoboa. Na akaingiza mpango wa KUJIFUNZA Kiingereza na soon atatoboa vizuri mno. Kwa level ya English aliyofikia wapo wa form 4 au F6 au Chuo hawezi kuongea. Wamejua kukariri mitihaani tu wafaulu. Si tunaona application zao za KAZI? Akifika kwenye interview mnajiuliza mara 2 kama alisomaje na transcript inasoma A,B,na C. Kumbe alikariri madesa tu.
 
Kuna uchizi fulani upo instagram wa kugombana na mtu usiye mjua wala kukutana nae hata siku moja,hiki kipaji Mange anacho kifuani kawajaza watu kibao anao wachukia na kumbuka kwenye blog yake aliwajaza watu alio gombana nao, ukisoma sababu unagundua ni roho mbaya na uchizi wake.

Yaani hawa ndio wale mtaani, ukiwauliza kwa nini una mchukia fulani utawasikia "basi tu si mpendi........" na mara nyingi wana kuwaga wanawake ila siku hizi mpaka wanaume.

Mange yupo US lkn hana tabia za watu wa huko, manake US watu hawana muda wa kufuatiliana.
Stress kimebeba gunia zima,ndio ulivyo huku hana kazi zaidi ya kufuatilia ya watu
 
Sasa hapo anamfokea vipi mtu aliyemzidi maisha kwa gap kubwa, ana mafanikio makubwa ya Mziki, ana muda mrefu kwenye game na still mpaka now yupo juu mwisho kabisa kafundishwa kimziki na katolewa kimziki na huyo huyo
Huyo Kupe mwenye wivu akiona msanii mzuri kumshinda yeye lazima amfanyie fitna?
 
Twende mbele turudi nyuma konde boy kajistukia aisee.

Mi naona hakukua na haja ya povu kubwa namna hiyo ambalo kiukweli linamshusha yeye na kuonekana ana chuki kweli kweli tofauti na mwenzie ambae hajamsema moja kwa moja. Na bado hatujui mondi alimlenga nani hasa ila konde boy kaonesha wazi wazi kua anamsema boss wake wa zamank.
Mtu akunyonye 600m akaona hujafa. Akaamua akuweke chawa wa kukutafuna na yeye kutumia mafumbo. Huwezi kukaa kimya na ukweli alisema. He deserves a credit for that #Harmonize. Tumeujua ukweli.
 
Kumbuka baraka ni kisirani kwa kila mtu nadhani hata mameneja wanafeli kufanya nae kazi kutokana na jinsi alivyo
Lakini ukiwa na kipaji vizuri ni uhakika tofauti na zamani leo hii soko la mziki liko huru hatuhitaji kunyenyekea mtu ili kusikika
Harmo hana tabia hizo pamoja na kuhama wasafi lakini bado alionyesha kumkubali boss wake lakini boss alitaka kuleta zile za kutaka kumpoteza kwenye gemu kwa sababu tu ameondoka wasafi

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Well said
 
Harmonize yupo sahihi kabisa....Diamond anayo pes ila tabia zake ni kama Mo tu maneno meengi ya kwenye kanga

Harmonize yupo sahihi kabisa....Diamond anayo pes ila tabia zake ni kama Mo tu maneno meengi ya kwenye kanga
Sure mkuu. Mswahili haswa. Mtu mlishaachana na akakulipa 600m inakuwaje kumfuatafuata kwa mafumbo na Chawa cheap wa Tecno na bando.
 
N
Nimeshangaa sana ila lisemwalo lipo hata enzi zile miaka ya 2007 wakati kalapina anaimba Hiphop bila madawa halafu kwenye video wanaonyesha mabango yenye majina ya Ngwair,Ray C ,Lord Eyes wengi tuliona kama wanapakaziwa ila Wote gari zikaja kuwaka.
Mkuu gari ya Mond itawaka vibaya mno yaani full light kabisa. MLA Cocaine Yule.
 
Harmonize kipindi anakaribia kuondoka WCB alidhani yeye ndiye anayeenda kuwa namba moja yani atamfunika bossi wake, sasa baada ya kutoka ndio akakutana na uhalisia ulivyo. Uthibitisho wa hili ni namna ya utoaji wa nyimbo pasipo na mpangilio unaoeleweka na namna anavyosign wasanii hovyo hovyo inaonyesha dhahiri ni frustration ya kutaka kumpindua diamond.

Kwenye moja ya interviews alizofanya Salam sk aliwahi kuongelea kuhusu swala la harmonize kuvuta bangi hadharani baada ya kujaribu kumkanya majibu yake ni kama ifuatavyo "kwani sitoi hit" hii inaonyesha ni namna gani dogo anajisahau.

Swala la kulipa m600 bila shaka lipo kimkataba zaidi, WCB ni kampuni hivyo mambo hufanyika ki- professional hivyo bila shaka alitakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kama endapo angehitaji kuvunja mkataba wake na label hiyo, hawezi mtu akakutoa from nothing akainvest muda na fedha kibao alafu akuache tu ufaidike na vijembe umchimbe.

Harmonize baada ya kukutana na uhalisia wa namna game ilivyo ngumu akaona bila kutumia kiki ya bosi wake wa zamani hatoboi na ndio maana toka day one anatoa ngoma yake ya UNO mpaka kufikia album yake ya juzi bado anamuandama tu.

Harmonize anatumia nguvu nyingi sana kutaka kumshusha diamond akiamini ndiye anayemkwamisha yeye kuwa namba 1 ndiyo maana haoni shida kumkashifu kwa kila namna anayoona itamshusha, ishu ya kutumia madawa ya kulevya sio ndogo hata kidogo na ubaya ni kwamba mashabiki ni kama watoto wadogo ishu kama hizi wanaweza kukukataa mazima na ukapoteza bila kusahau namna alivyotaka kumpoteza rayvanny kwa ishu kuwa anatembea na mwanafunz (Paula) .

Mbaya zaidi anawasahau vijana wadogo kama akina rayvanny ambao na wenyewe wanamkimbiza mostly ni record aliyoweka vannyboy juzi ya kuwa msanii wa kwanza kutokea Africa kuperform kwenye MTVEmas hii inaonekana ilimchoma sana harmonize na haswa ule msumali wa moto aliyo ushindilia diamond ndo kabisa akaamua aje ateme nyong'o insta.

Kama mnafuatilia mtakua mliona juzi alipost akijinasibu kuwa nobody sounds better than him bila shaka hii yote ni frustration ya album yake aliyoachia recently kutofanya vizuri.

Mwisho wa yote anayofanya Harmonize ni kutaka sikio lizidi kichwa kuna namna ambavyo mtu anakusaidia kiasi kwamba hata umlipe kiasi gani bado huwezi kumlipa fadhila, sometimes sio swala la pesa tu bali ni ule moyo tu ambao anakuwa nao mtu. 2015 diamond tayari alikua msanii mkubwa sana, angeweza kumvimbia harmonize akaendelea na maisha yake kwani lazima ? .. lakini akaona hapana huyu ni kijana mwenzangu anatafuta sio mbaya kumshika mkono.

Kuna mtakao sema " kwani si alishamlipa m600? Au kwani yeye harmonize si ana kipaji ? ..kama alivyosema member mmoja hapo juu" kipaji pekee hakitoshi kutokana na ugumu wa mziki wa bongo unahitaji watu kama wakina diamond, alikiba ambao wana crowd kubwa wakushike mkono, wangapi wana vipaji na wanasota kitaa ?? ..

Mwisho wa yote haya mambo hatuyajui kiundani ila kwa vyovyote harmonize hakupaswa hata kidogo kumjibu au kubishana na diamond hadharani hata kama diamond ndiyo mwenye matatizo, sio dhambi kuhisi unaweza kumzidi bossi wako ila mziki ndio ulipaswa uongee alafu sisi mashabiki tungesema who is who na sio kumpiga vijembe kila uchwao ..

Najaribu kuvaa viatu vya diamond lakini nashindwa, ni maumivu kiasi gani mtu ambaye umemsaidia na kumuheshimisha ana kujibu dharau na kwenda mbali zaidi kutaka kukupoteza, kwakweli inavunja moyo. Leo hii harmonize ni msanii mkubwa sana east Africa, same applies kwa rayvanny lakini wote ni products of diamond platnumz .. namna hii diamond atakuwa na moyo kweli wa kuendelea kuibua vipaji vingine ?? ..

Mwisho kabisa sina ushabiki wa kipumbavu wa mtu yeyote, sijui team kiba, team wcb, team konde .. mimi ni shabiki wa mziki mzuri namkubali alikiba, diamond platnumz, kondeboy na wengine wote wanaofanya mziki mzuri .. nime analyze kutokana na ninayo yaona personally ..
Umeona vizuri. Ila issue ya Konde na Mond ni uadui mkubwa Sana. Na Mond hataki Amani. Kondeboy alijitajidi mno Suluhu ikashindikana. Diamond ana kiburi cha mafanikio. Iko wazi Sana hiyo. Ngoja tusubiri chawa wake wapeweTecno na bando waje hapa kusafisha Hali ya hewa. Ila ndiyo tayari iko masikioni mwa wengi kuwa Diamond hafai. Hana tofauti na alivyokuwa anailaumu Clouds na Marehemu Ruge.
 
Baada ya Ile interview ya Harmonize Jana 18 Nov 2021 nimeamua kumuomba Mungu ampige Diamond kwa huo unga mpaka afikre level ya Yule Jamaa wa "Home Alone". Yaani awe ni kulala Tu. Yaani anatesa vijana kwa kuwa hawajui watokee wapi. Ila Mungu kamuona Harmonize.
Mungu sio jirani yako
 
Back
Top Bottom