Ni kweli Fumanizi mara nyingi humarisha ndoa...!

Ni kweli Fumanizi mara nyingi humarisha ndoa...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
argument.jpg

Fumanizi husababisha hisia zenye maumivu, hasira, kutokuaminiana, woga, aibu na kujilaumu. Lakini kufumania au kufumaniwa hakupaswi kuwa sababu ya kuwa mwisho wa ndoa yenu, ingawa kunaweza kuwa pia.

Baada ya fumanizi, inabidi ujitahidi kuelewa na kuweza kujenga tena ndoa yako, pengine sasa ikiwa ni ndoa imara zaidi. Hata hivyo hii inataka kujituma kwingi na uvumilivu na subira. Ndoa inaweza kuendelea hata baada ya fumanizi kwa kutumia ushauri, kupeana muda na kushirikiana. Kuna ndoa ambazo zimeweza kudumu zaidi baada ya fumanizi kutokea.

Pale kutoka nje kwa mwanandoa mmoja kunapogundulika hupelekea hisia kali kwa wanandoa wote, mshtuko, aibu, kujilaumu, kujiona mkosaji, hasira kali na wasiwasi. Kutokana na hisia hizi zote mara nyingi wengi hufanya maamuzi yasiyo mazuri kama kutengana au kuachana kabisa. Badala ya kufanya hivyo katika kipindi kile cha muda mfupi baada ya fumanizi, tunahitaji kuwa watulivu sana ili tuweze kuchukua hatua zinazofaa.

Kupata msaada:
Kwa uzima na afya yako mwenyewe, tafuta msaada kutoka kwa familia, rafiki, mchungaji, shekhe au mshauri yeyote unayemwamini wewe na kujihisi huru kwake. Kuongea kuhusu hisia zako kwa wale unaowapenda sana itakusaidia wewe kupunguza nguvu za hisia za maumivu ya tukio hilo. Kuongea na watu wengine kunaweza kukupa wewe uwezo wa kuelewa zaidi hisia zako na kupata mtazamo mwingine kuhusu tukio.

Pengine aliyetoka nje inawezekana hatosheki katika mahusianao katika ndoa yake au hawajibiki vizuri katika ndoa. Au pengine hawezi kudhibiti mihemko yake. Mabadiliko ya maisha kama kuzaliwa mtoto au upweke wa aina fulani, unaweza kuwa ndio sababu ya kutoka nje. Inabidi haya yatazamwe kabla mtu hajaamua lolote.

Kwa hiyo kujua sababu ya mwingine kutoka nje ni muhimu sana na hii inaweza kukupa ahueni, kwani unaweza kubaini kitu ambacho kinaonesha kwamba, kwako pia kuna matatizo. Hatua zitakazokusaidia kujenga upya ndoa yako baada ya fumanizi ni nyingi. Lakini hizi ni baadhi tu ambazo kwa mazingira yanayokukabili, zinaweza kukusaidia.

Kuacha kutoka nje ya ndoa:
Hatua ya kwanza ni kwa mwanandoa kuacha tabia ya kutoka nje ya ndoa kiukweli.

Kukubali kuwajibika:
Kama umetoka nje ya ndoa, kuwa tayari kuwajibika katika vitendo vyako.

Onyesha nia ya malengo yako:
Kuwa na uhakika kuwa wote wawili mko tayari kujenga upya ndoa yenu.

Onana na mshauri wa wanandoa:
Mtafute mshauri wa ndoa ambaye atakusaidia kujenga upya ndoa yako kama itakuwa inahitajika. Onana na mshauri wa ndoa ambaye alishawahi kukutana na kusaidia kutataua matataizo ya fumanizi. Mwepuke mshauri ambaye anaamini kufumania au kufumaniwa ndio mwisho wa ndoa yenu.

Kuchunguza tatizo:
Kufumania au kufumaniwa huzua matatizo katika ndoa. Chunguzeni kwa makini mahusiano yenu ili uweze kujua nini kilichosababisha au kilichopelekea kutoka nje ya ndoa na nini mfanye ili kuzuia kutoka nje ya ndoa tena

Kila mmoja apewe nafasi:
Kila mwanandoa anahitaji kupumzika kwa ajili ya kuondoa msongo na wasiwasi kutokana na tukio la fumanizi, hii ni kwa sababu huwa ni vigumu kusikiliza ushauri wakati mihemko iko juu sana.

Pata muda:
Epuka kujua undani zaidi kuhusu fumanizi la mwenzi wako kwa wakati wa mwanzoni. Ahirisha mjadala huo kwanza mpaka uzoee ile hali ya kumfumania mwenzi wako.

Mwisho wa ndoa au hapana ?
Siyo kila ndoa iliyoguswa na suala hili la fumanizi ni lazima imalizike kwa kutokuachana. Wakati mwingine kunakuwa na uharibifu mkubwa na wanandoa hawana budi kuachana na pia kama wanandoa hawako tayari kuwa pamoja tena.

Lakini kama wote mko tayari kujenga upya ndoa yenu, basi suala hili huwa rahisi sana na uhusiano utaendelea kuwa mzuri na wa amani zaidi.
 
Mtambuzi… Hili fumanizi unaliongelea kwa mwenza wa kike, wa kiume ama woote?

So far hadi dakika hii ni wanaume wachache wana ubavu wa kusamehe mke anayetoka nje ya ndoa… Tena basi bora ahisi ama asikie na huyo mwanamke aombe msamaha, but nielewavyo ni kuwa nyie akina baba ukimkuta mwanamke wako (hata kama siyo mkeo) uchi kabisa na jamaa mwingine uvumilivu mara nyingi ni ‘O'.

Kuna lingine la msingi la kuangalia… Fumanizi linaweza lisivunje ndoa. Ila namna ya fumanizi hilo ndio ikavunja. Unapofumania mwenza wako ukapaniki na kupiga makelele ama ukataka kuchukua mashahidi wa kuenda kufumania nao inaweza sababisha hata ukimsamehe mwenzi wako kwa kosa alilifanya ila unashindwa kumrudisha sababu tu jamii nzima (familia, ndugu, marafiki na jamaa) wanaelewa na hivyo waogopa kuchekwa (Hii hasa kwa wanaume).
 
hapo kwenye kuchunguza tatizo, sio wote watokao sababu ya matatizo,wengine hawaridhiki na mwanamke mmoja toka tumboni mwa mama zao, kama wangu alitoka coz ya ujinga wake, mama yake na mdogo wake wa kike, eti mama analazimisha nibebe mimba, mtoto ana mwaka na nusu nibebe mimba nyingine kisa kumridhisha mama? hell no, mwanaume akaanza vituko, mama akaona poa tu, dada mtu akiniletea pozi/mdomo, nikasema hawamjui mmarangu hawa, ndio yakatokea na kutokea, siku ya usuluhishi mwanaume mzima anasema mama yake alimshauri azae watoto chap chap, so aliona bora ajipumzishe huko nje,mana mkewe hakumtimizia alichotaka, sasa nikamwambia japo tumesuluhishwa, mtoto mwingine ni mpaka mie niamue, kutokana na ulivyonisumbua hakuna cha wewe, mama/dada yako, ni maamuzi yangu mie kubeba mimba kama vipi pita kushoto au jifunge salifeti ulale.
 
Inategemea na damage iliyofanyika wakati wa fumanizi.

kama 'damage' inaweza kuwa managed, basi penzi litaimarika. kuna damage zingine hazina dawa, basi mnaachana for good.

So not always!, si eti Nyani Ngabu?
 
Last edited by a moderator:
Dah!

Pole aisee

KAma hiyo ndio ilikuwa sababu ya kutoka nje, kweli ilikuwa haki yako kumtesa vile
Ni bora mtu hata aeme alipitiwa kuliko aliamriwa na mama yeke, kama teen.

hapo kwenye kuchunguza tatizo, sio wote watokao sababu ya matatizo,wengine hawaridhiki na mwanamke mmoja toka tumboni mwa mama zao, kama wangu alitoka coz ya ujinga wake, mama yake na mdogo wake wa kike, eti mama analazimisha nibebe mimba, mtoto ana mwaka na nusu nibebe mimba nyingine kisa kumridhisha mama? hell no, mwanaume akaanza vituko, mama akaona poa tu, dada mtu akiniletea pozi/mdomo, nikasema hawamjui mmarangu hawa, ndio yakatokea na kutokea, siku ya usuluhishi mwanaume mzima anasema mama yake alimshauri azae watoto chap chap, so aliona bora ajipumzishe huko nje,mana mkewe hakumtimizia alichotaka, sasa nikamwambia japo tumesuluhishwa, mtoto mwingine ni mpaka mie niamue, kutokana na ulivyonisumbua hakuna cha wewe, mama/dada yako, ni maamuzi yangu mie kubeba mimba kama vipi pita kushoto au jifunge salifeti ulale.
 
it's rare for a +ve result. kama utamsamehe then ndoa yenu haitavunjika becoz mtakuwa mmeonehsa maturity na uvumilivu wa hali ya juu. but normally this end is divorce
 
Mtambuzi… Hili fumanizi unaliongelea kwa mwenza wa kike, wa kiume ama woote?

So far hadi dakika hii ni wanaume wachache wana ubavu wa kusamehe mke anayetoka nje ya ndoa… Tena basi bora ahisi ama asikie na huyo mwanamke aombe msamaha, but nielewavyo ni kuwa nyie akina baba ukimkuta mwanamke wako (hata kama siyo mkeo) uchi kabisa na jamaa mwingine uvumilivu mara nyingi ni ‘O'.

Kuna lingine la msingi la kuangalia… Fumanizi linaweza lisivunje ndoa. Ila namna ya fumanizi hilo ndio ikavunja. Unapofumania mwenza wako ukapaniki na kupiga makelele ama ukataka kuchukua mashahidi wa kuenda kufumania nao inaweza sababisha hata ukimsamehe mwenzi wako kwa kosa alilifanya ila unashindwa kumrudisha sababu tu jamii nzima (familia, ndugu, marafiki na jamaa) wanaelewa na hivyo waogopa kuchekwa (Hii hasa kwa wanaume).

Ahsante dada AshaDii kwa uwepo wako katika uzi huu.
Mada hii inawahusu wote yaani wanaume na wanawake, na kuhusu hilo la wanaume kutowavumilia wake zao pale wanapowafumania niliwahi kulijadili hili, naomba ufungue hii link hapa chini:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...kuwa-kijogoo-na-mwanamke-kahaba%85%85%85.html
 
Last edited by a moderator:
Dah!

Pole aisee

KAma hiyo ndio ilikuwa sababu ya kutoka nje, kweli ilikuwa haki yako kumtesa vile
Ni bora mtu hata aeme alipitiwa kuliko aliamriwa na mama yeke, kama teen.

kama nyamayao, nakubaliana kabisa kwamba fumanizi linaimarisha ndoa, "labda muwe hampo tayari kwa usuluhishi", msukuma kama anafanya kwasasa anafanya kwa akili/abadu zote,amekuwa na mapendo tofauti kwangu,huruma imezidi kwangu, amekuwa na hofu ya makubaliano yetu siku ya upatanisho, kwangu imenipa ujasiri/somo.
 
Mtambuzi… Hili fumanizi unaliongelea kwa mwenza wa kike, wa kiume ama woote?

So far hadi dakika hii ni wanaume wachache wana ubavu wa kusamehe mke anayetoka nje ya ndoa… Tena basi bora ahisi ama asikie na huyo mwanamke aombe msamaha, but nielewavyo ni kuwa nyie akina baba ukimkuta mwanamke wako (hata kama siyo mkeo) uchi kabisa na jamaa mwingine uvumilivu mara nyingi ni ‘O'.

Kuna lingine la msingi la kuangalia… Fumanizi linaweza lisivunje ndoa. Ila namna ya fumanizi hilo ndio ikavunja. Unapofumania mwenza wako ukapaniki na kupiga makelele ama ukataka kuchukua mashahidi wa kuenda kufumania nao inaweza sababisha hata ukimsamehe mwenzi wako kwa kosa alilifanya ila unashindwa kumrudisha sababu tu jamii nzima (familia, ndugu, marafiki na jamaa) wanaelewa na hivyo waogopa kuchekwa (Hii hasa kwa wanaume
).

ukweli 100%, umesema vema, mie nilishukuriwa coz nilienda pale mwenyewe tena kwa "ustaarabu"....khaa ndoa hizi, kwangu mie sikuona sababu ya kubebana na mtu kwanza aliejua naenda ni dada yangu tu, nilitaka kulimaliza mwenyewe, nipambane mie na wazinzi wangu, na ukweli mwingine ni kwamba "HII KITU SIO RAHISI KABISA, SIKIA TU KWA MTU KUFUMANIA, KAMA UNA ROHO NDOGO USIJARIBU KUFANYA), inaumiza sana sana!
 
Una bahati kama kwako imeimarisha ndoa.

Kwa wengine ndio mwisho wa masimulizi

Si kila mtu yuko tayari kutafuta suluhu, na inategemea uliyamfumania ana 'umuhimu' gani maishani mwako.

kama nyamayao, nakubaliana kabisa kwamba fumanizi linaimarisha ndoa, "labda muwe hampo tayari kwa usuluhishi", msukuma kama anafanya kwasasa anafanya kwa akili/abadu zote,amekuwa na mapendo tofauti kwangu,huruma imezidi kwangu, amekuwa na hofu ya makubaliano yetu siku ya upatanisho, kwangu imenipa ujasiri/somo.
 
Very true

Mie siwezi kufanya biashara hii hata kwa mtutu wa bunduki, sina kifua hicho aiseee, nikiona sijui kama naweza samehe asilani, my 'ego' won't let me nisamehe.

Mambo ya kufanya watu waanze kuita ambulensi sitaki

ukweli 100%, umesema vema, mie nilishukuriwa coz nilienda pale mwenyewe tena kwa "ustaarabu"....khaa ndoa hizi, kwangu mie sikuona sababu ya kubebana na mtu kwanza aliejua naenda ni dada yangu tu, nilitaka kulimaliza mwenyewe, nipambane mie na wazinzi wangu, na ukweli mwingine ni kwamba "HII KITU SIO RAHISI KABISA, SIKIA TU KWA MTU KUFUMANIA, KAMA UNA ROHO NDOGO USIJARIBU KUFANYA), inaumiza sana sana!
 
kama aliyefumania anampenda kwa dhati mwenza wake na hayuko tayar kumwacha na pia ana MOYO wa kusamehe,,,na kama yud aliyefumaniwa yuko tayari kujirekebisha na kutokutoka tena nje ya ndoa basi ndoa itaimarka....
Bt most couples fumanizi lkitokea talaka inahusika sana......
Pia swali la kujiulza ni kwa nini mtu anatoka nje ya ndoa??
 
Ahsante dada AshaDii kwa uwepo wako katika uzi huu.
Mada hii inawahusu wote yaani wanaume na wanawake, na kuhusu hilo la wanaume kutowavumilia wake zao pale wanapowafumania niliwahi kulijadili hili, naomba ufungue hii link hapa chini:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/230118-fumanizi-mwanaume-anapokuwa-kijogoo-na-mwanamke-kahaba%85%85%85.html

Ok.. Kama inahusu woote kuna umuhimu sasa nyie kwa nyie akina baba mhamasishane umuhimu wa kusamehe. Kuwa hata wake zao wanaweza wakatoka (iwe makusudi ama bahati mbaya) so nao wawe wanasamehe kama wanavyosamehewa.

Nikiangalia katika jamii ninayotoka, wapo wanawake wengi wapo kwenye ndoa na wanafanyiwa vituko na waume zao. Suala la kuwa na wanawake tena wengine ku flaunt kabisa huyo hawara yake ni moja ya tatizo sugu. Ukiuliza wanandoa wengi (ingawa wanaweza wasiwe wazi); wengi wa wake wameshawahi jua mume wake katoka nje tena pengine hata zaidi ya mara moja na alisamehe... Siamini kuwa inaimarisha ndoa. Labda katika matukio machache... Mara nyingi kinachofanya wabaki ni circumstances ambazo hata bila kufumania ndizo humuweka hapo.
 
ukweli 100%, umesema vema, mie nilishukuriwa coz nilienda pale mwenyewe tena kwa "ustaarabu"....khaa ndoa hizi, kwangu mie sikuona sababu ya kubebana na mtu kwanza aliejua naenda ni dada yangu tu, nilitaka kulimaliza mwenyewe, nipambane mie na wazinzi wangu, na ukweli mwingine ni kwamba "HII KITU SIO RAHISI KABISA, SIKIA TU KWA MTU KUFUMANIA, KAMA UNA ROHO NDOGO USIJARIBU KUFANYA), inaumiza sana sana!

Hongera saana Nyamayao kwa moyo wa ujasiri... Ni wachache huweza hivyo. Wengi hutaka dunia nzima isikie ili mwenza wake aadhirike; kumbe pengine in a way na yeye pia anajiadhiri bila kuelewa.
 
Mara nyingi naona wanaosamehe wakifumania ni wanawake kwa wanaume ni mara chache sana, mwanamke anaweza hata akafanya fumanizi la skendo lkn bado akawa anampenda mumewe mfano yule dada S wa makumbusho alimfuma mumewe live na akatangaza kuwa ndio amezidi kumpenda mumewe na hatamwacha, sijui hilo fumanizi lilimuongezea upendo kwa mumewe? mimi sikuelewa!
 
Maswali ya kujiuliza baada ya fumanizi....................

Kwanza, hebu jikague, Je, umevunjika moyo kupita kiasi? Unadhani itakuwa bora kuvumilia? Unadhani kumvaa na kumwambia umechoka na unataka kuondoka itakuwa ni kujiongezea mfadhaiko zaidi?

Pili, unadhani utaendelea kubaki katika ndoa kwa sababu za kidini? Unataka kufanya kitu kilicho sahihi daima? Uko tayari kuendelea kudhalilika na kuwa hatarini kwa sababu ya imani yako ya kukukataza kuvunja ndoa? Je ni kwa imani yako au wasiwasi wako umelazimika kubaki? Nijuavyo mimi, kosa la kutoka nje halitetewi na dini yoyote linapokuja swala la kuvunja ndoa.

Tatu, unadhani unalazimika kubaki kwa usalama wa watoto? Unadhani ni wewe pekee unawajali watoto na mwenzio hawajali? Inawezekana na mzazi mwenzio pia ni mpenda watoto? Unadhani kuachana kutawaletea watoto matatizo zaidi? Una wasiwasi na maisha ya watoto kama utaamua kuondoka? Kumbuka kuishi kwenye vurugu za ndoa huwavuruga watoto kuliko watoto kuishi na baba au mama wa kambo mwenye upendo.

Nne, unadhani hakuna uwezekano kabisa katika ndoa hii? Umekwama? Umenata kama ulimbona huwezi kuondoka? Unaweza kufikia muafaka kwamba umejitahidi kwa uwezo wako wote kumrekebisha mwenzio lakini wapi. Hivyo umeamua kuishi hivyo hivyo?

Tano, unadhani huwezi kuondoka? Kuna kitu unachodhani kinakuletea ugumu wa kuanza safari? Kuanza maisha mapya? Huna uwezo wa kujiamulia? Kumbuka kwamba, huenda ni mazoea tu yanayokuzuia au utegemezi wa kipato. Lakini, kila binadamu ameletwa duniani ili asimame kama yeye, na siyo kama kipande cha mwenzake.

Sita, unataka kumlinda? Kuna kitu kibaya unachodhani kinaweza kutokea kama utaamua kuondoka? Ataweza kuishi peke yake? Kama utaondoka unadhani itakuwa ni njia ya kumpeleka shimoni zaidi? Umeamua kubaki ukijua kwamba baada ya muda tatizo lenu linaweza kutatuliwa? Inawezekana likatatuliwa, lakini inawezekana wewe ni mtu wa kuumia kwa sababu ya wengine bila sababu.

Saba, unaendelea kuishi naye kwa sababu kuna hatari kumwambia unataka kuondoka? Unadhani atalipuka kwa hasira utakapomwambia unataka kuondoka? Una wasiwasi kwamba una haki ya kuamua kuhusu maisha yako na kuna sheria zinazokulinda.

Je, hujafikiria namna ya kuanza maisha mapya? Hii ni tofauti na hofu ya kuanza maisha mapya. Labda maisha yako, yake na ya watoto yameambatanishwa kupita kiasi, hivyo inakuwia vigumu kujinasua?

Pia kuambatanishwa huku labda ndiko kunakokufanya hata usiwe na chembe ya wazo la kutaka kuondoka? Umewahi kufikiria kuhusu utashi wako, ujuzi wako, ndoto zako, matumaini yako na mustakabali wa maisha yako bila yeye, au bila watoto?

Chukua muda wa kutosha kufikiri kwa makini na uyajibu maswali hayo yote ukishayajibu utakuta unatoa uamuzi sahihi utakaokupeleka kwenye maisha uyatakayo. Kumbuka, kila binadamu hukosea na kusamehe kwa aliyekosewa. Lakini kusamehe hakuna maana ya kuendelea kuumia au kuumizwa na uliyemsamehe.
 
Duh, ni kweli mara nyingi kwa wanaume ni vigumu kufumania, babu yangu aliwahi kuniambia enzi zao ilikuwa ni kosa kwa mwanamke kumfumania mumewe, unatakiwa kama mwanamke uwe makini na ikiwezekana usipite maeneo ambayo unaweza kukutana na mumeo akiwa na mwanamke mwingine!

Pia nimeshuhudia wakati mwingine hata mwanamake anaelewa wazi kuwa mumewe anatoka na mwanamke mwingine na hata haulizi anaamua kupiga kimya!
 
Mtambuzi, nimesha print article yako , nikifumaniwa tu, nasema,"nashukuru sana kwa kunifumania, sasa nina amini kuwa penzi letu litaimarika na kushamiri mara dufu" Kisha natoa print out ya article yako.
Tena nikiwa naenda huko nje kuchabanga infidelity nachagua kondoo aliyenona kama Madame B au cacico
 
Last edited by a moderator:
Very true

Mie siwezi kufanya biashara hii hata kwa mtutu wa bunduki, sina kifua hicho aiseee, nikiona sijui kama naweza samehe asilani, my 'ego' won't let me nisamehe.

Mambo ya kufanya watu waanze kuita ambulensi sitaki

sio rahisi "kusamehe" ndi mana nikasema kama una roho ndogo "usijaribu" ilinichukua muda sana kusamehe, kila wakati inanijia kichwani, lakini kwa jitihada alizoonyesha kuniondoa hapo mwishowe alifanikiwa, na nilikuwa namwambia kabisa hii kitu hainitoki rohoni, Mungu kaumba binadamu na kusahau, tunafiwa na wapendwa wetu tunasahau, pia hili utalisahau tu, japo "inaumiza sana"
 
Back
Top Bottom