Ni kweli hatufanikiwi sababu ya serikali zetu au Kuna namna maisha ya kizungu yametuathiri?

Ni kweli hatufanikiwi sababu ya serikali zetu au Kuna namna maisha ya kizungu yametuathiri?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,678
Reaction score
5,166
Maisha ya kwenye runinga ni gharama kubwa sana Kuna picha nzuri ya Teknolojia,majengo,Magari na hali safi ya mazingira Kuna picha ya uhuru wa vyama na Ibada.

Unadhifu huu unalinganishwa maendeleo ya nchi zetu ambazo kiuhalisia ni changa,kiuhalisia zimejengwa katika mitazamo mingi,Imani na itikadi tofauti,kimsingi mifumo inayotumiwa ni agenda/ipo remoted upande Fulani kwa hiyo Kuna shinikizo au msukumo mkubwa wa kimaendeleo ukilinganisha na uchanga wa mataifa ya kiafrika.

Kuna wakati natamani Kulinganisha maendeleo yetu na nchi nyengine ila nashindwa kuangalia vigezo vipi ni sahihi kwa uzani.

1.Umri wa Mataifa
Ulaya na Amerika ni mataifa makongwe yenye mizizi katika nchi zetu lakini ni tofauti na nchi zetu za Afrika,wao ndiyo waliyotutawala,wanaotutawala kwa fikra na mitazamo kimsingi hata vijana wetu wanatumia rungu hilo fikra na mitazamo hafifu kulinganisha Mataifa au mabara haya.

2.Elimu na teknolojia
Mataifa yetu bado yanajikongoja kufikia malengo ya Teknolojia tunayoiwaza ila Kuna kikwazo cha rasilimali na masharti magumu yanayoturidisha nyuma.

Naomba Ndugu zangu hizi fikra potofu zinazotawala akili zetu tuachane nazo,Uhuru wa Fikra upon katika Mabano ya kiitikadi,
 
Back
Top Bottom