Pantomath
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 842
- 3,449
Nina mdogo wangu amemaliza masomo kaomba asirudi nyumbani aende Dar ili apambane, sio mbaya sababu ni mchakarikaji tukaona haina haja ya kumlazimisha kuja mkoa.
Nikamuambia kama ni hivyo basi atoke kwa ndugu, ana vitu vyake akapange, nitamsapoti kodi kwa mwanzoni,
Juzi tukapatana atafute chumba, Siku nzima bila, jana pia, leo namuuliza vipi anasema vyumba vipo ila mpaka madali, nikamuona kama mzembe hivi, nikamuuliza unashindwa kuzunguka kuulizia? Akasema ndio amefanya hivyo ila kila anapobahatika kukuta chumba anaambiwa apitie kwa dalali.. Nikamwambia asiulize wapangaji amtafute mmiliki, akasema wanaomjibu hivyo wapo wamiliki pia. Na akaambiwa dalali atataka hela ya usumbufu na kodi ya kwanza.
Hii mimi haijaniingia akilini kabisa, naona dogo ashaanza uzembe, hata moyo umepungua.
Hii kitu ipo kweli? Kwa logic gani? Yaani mmiliki wa nyumba na kodi yako, halafu unataka dalali wakati mteja kaja mpaka mlangoni? Faida yake ni nini?