Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kumekucha!
Binadamu wanapenda kupewa maneno laini, hawapendi ukweli, wanapenda sifa hata wasizozistahili.
Yapo Matoto ya hovyo,
Wapo wazazi wa hovyo bila kujali ni wanani,
Hayo Matoto yakikua ndio yanaleta kizazi cha hovyo hovyo,
Unakuta kiongozi hovyo,
Mchungaji hovyo,
Sheikhe Hovyo,
Mwananchi Hovyo.
Sijaona makosa katika kauli ya IGP Siro, ameongea ukweli mchungu sana.
Hata hivyo ukweli huo unagusa kundi kubwa la watu wa Zama hizi sio tuu tabaka la chini Bali pia hata tabaka la juu.
Kuna watu wanajifanya wanamsema na kumzingua igp Kwa kauli yake ya kusema watu wasizae mitoto ya hovyo ati kakosea, hakuna makosa hapo kimaadili.
Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa wa hovyo, watoto wote Mungu amewaumba wakiwa wema, kila kitu Mungu alikiumba kikiwa chema. Isipokuwa mazingira ndio humgeuza mtu kuwa vile alivyo.
Mtoto amezaliwa akiwa Hana anachojua, mtu anazaliwa akiwa hana anachomiliki zaidi ya roho na mwili wake aliokuja nao ukiwa uchi.
Wazazi na jamii ndio humfanya mtoto awe qa hovyo au mwema.
Mzazi WA hovyo huzaa Matoto ya hovyo.
Jamii ya hovyo huzalisha Matoto ya hovyo
Hovyo! Hovyo hovyo!
Nikionaga Matoto ya hovyo, iwe ni kiongozi au mtu wa kawaida huwaga moja Kwa moja akili yangu inarejea Kwa wazazi na walezi WA mtoto husika.
Kuna watu wanasema Kwa kujitetea ati wachungaji au masheikhe wapo waliozaa Matoto ya hovyo, ni kweli kwa sababu baadhi ya hao wachungaji hujifanya watakatifu mbele za jamii lakini ukienda kwenye nyumba zao unakuta mambo ya hovyo kabisa.
Siku zote mwana wa nyoka ni nyoka. Iwe karithi Kwa Mama au Kwa Baba, iwe mi uzembe wa kimalezi uliosababishwa na Mama au Baba
Hakuna kisingizio linapokuja suala la Uovu au Uhalifu. Sijui ati toto limesomea boarding ndio maana limeweza kuharibikia huko, mbona wengine tumesomea huko na hatujaharibika.
Wengine wanajitetea kuwa kuwa mtoto akilelewa na Bibi au akiwa mbali na Baba na Mama anakuwa wa hovyo, Jambo ambalo sio kweli, wangapi wanelelewa na Bibi na wameishi pasipo wazazi lakini ni watoto wema.
Uovu hauna kisingizio, Uhalifu haunaga kisingizio,
Bungeni yapo Matoto ya hovyo,
Shuleni, hospitalini, mashirika, viwandani huko kote yapo Matoto ya hovyo.
Ndio maana Matoto hayo hayaoni ajabu kudhulumu na kuonea wengine.
Matoto ya hovyo yanasifa ZIFUATAZO;
1. Mabinafsi
Toto la hovyo linajijali lenyewe na familia yake. Unakuta linalipwa mamilioni ya Fedha, posho kibao lakini bado haliridhiki, linaiba na kudhulumu wengine, linataka kuongezewa Mshahara ati ili iliendeshe magari mazuri wakati kuna watu wanakojoa pesa ya Kula. Hili litakuwa toto la hovyo Sana.
Toto la hovyo ni binafsi mno, halioni shida kudhulumu uhai WA wengine kisa mambo yake binafsi Kama vile Cheo, mamlaka, uchumi, au masuala ya Kidini.
Ubinafsi ni Dalili ya Kwanza ya toto la hovyo.
Kwa bahati mbaya. Ni kuwa jamii ya kiafrika Matoto mengi ni yahovyo.
2. Uhalifu na kutenda madhambi pasipo kujali.
3. Kupenda kujitetea na kuutetea Uovu.
Toto la hovyo kinaweza kuwa mtu yeyote iwe mi Mimi, wewe au Yule.
.
Hovyo!! Hovyo! Hovyo
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro