Ni kweli katika Serikali hii na kwenye CCM hii hakuna wazalendo?

Ni kweli katika Serikali hii na kwenye CCM hii hakuna wazalendo?

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
581
Japokuwa Serikali yetu haiongozwi na Malaika, lakini kusema kweli yapo mambo mengi yanayoendelea nchini yanayotia kichefu chefu, kukatisha tamaa na kusikitisha.

Hali hii ya mambo imesababisha ukosoaji mkubwa dhidi ya CCM na Serikali yake kutoka kwa kada mbalimbali za wananchi na hata ughaibuni, hali inayotia doa kubwa kwa Historia nzuri ya nchi yetu na hata Diplomasia ya Kimataifa kwa ujumla wake.

Wakati ukosoaji huo wa ndani na nje ukishika kasi wanaolalamikiwa kwa upande wao yaani Serikali na CCM wako busy na mipango yao kama kawaida na hata kwa namna moja au nyingine wanawakejeli au kuwabeza wanaowanyoshea vidole.

Kitendo hiki cha CCM na Serikali yake kimezidi kuchochea hasira miongoni mwa raia ambapo sasa wengi wanasema ndani ya Serikali na katika CCM hakuna aliye msafi, hakuna Mzalendo, wote wamejaa makovu ya uadilifu ndio maana hakuna anayesema lolote huku wakisahau kuwa ukijitokeza kuasi mfumo kama alivyofanya Polepole basi jiandae kuishi maisha ya Digidigi au Nguchiro huku ukila jeuri yako.

Pamoja na mitazamo hiyo ya wananchi wengi dhidi ya CCM na Serikali yake, bado tunawapata watu wa aina ya Polepole, Tundu Lissu, Gwajima, Dk. Slaa, Evarist Chahali Jasusi wa zamani wa TISS aliyekimbilia uhamishoni nchini Uingereza. Nikitaja kwa uchache.

Hawa kila mmoja kwa nyakati tofauti waliibua mambo mengi na mazito kwa nchi yetu.

Si kweli kwamba walilala wakapewa maono, hapana. Walipenyezewa na watanzania wenzetu waliomo CCM, TISS na katika Serikali kwa ujumla.

Kuvuja kwa taarifa za ndani na kuwafikia baadhi ya wenzetu ambao kwa ujasiri wao huzitoa kwa umma, je wanaovujisha taarifa hizo ni wazalendo au wapinzani?
 
Back
Top Bottom