SI KWELI Ni kweli Kikwete amesema watoto wake hawatapata hata shilingi moja kutoka kwenye utajiri wake wa fedha taslimu?

SI KWELI Ni kweli Kikwete amesema watoto wake hawatapata hata shilingi moja kutoka kwenye utajiri wake wa fedha taslimu?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
photo_2026-03-06_20-05-34.jpg
photo_2026-03-06_20-05-26.jpg
 
Tunachokijua
Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia mwaka 2005 hadi 2015. Kabla ya kuwa Rais, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali muhimu serikalini kuanzia 1994 hadi 2005, zikiwemo, Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Waziri wa Wizara ya Fedha ya Tanzania, Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini ya Tanzania.


Madai

Kumekuwapo na taarifa iliyochapishwa na tovuti ya pertamina-invest.com ikiwa na kichwa cha habari "Unachopaswa Kujua: Jakaya Mrisho Kikwete - Watoto wangu hawatapata hata shilingi moja kutoka kwenye utajiri wangu wa fedha taslimu"

Aidha taarifa hiyo inamtaja Rais mstaafu huyo kuwa alitoa mahojiano yenye utata kwa chombo cha habari cha kitaifa kuhusu asili ya wosia wake kile anachopanga kuwaachia watoto wake badala ya fedha zake taslimu zinazotajwa kwa kukadiriwa kufikia Shilingi za kitanzania trilioni 32.5


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?


Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli. Kwa kutumia nyenzo za kidigitali imebainika kuwa hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo.

Aidha imebainika kuwa taarifa hii inafanana sana na mitindo ya maudhui ya kuvutia sana ili kuwafanya watu wabofye kiungo "clickbait" au taarifa za kutengenezwa ambazo mara nyingi hutumia majina ya viongozi mashuhuri kuvuta wasomaji kwenye tovuti zisizoaminika au matangazo ya biashara.

Kadhalika, hakuna taarifa kama hiyo iliyochapishwa na The Citizen, ingawa taarifa hiyo inadai kuwa alifanya mahojiano na gazeti hilo.

Kadhalika nyenzo za kidigitali zinabainisha uwezekano wa uwepo wa hatari za kiusalama kutoka kwenye tovuti hiyo ambapo vinabainishwa viashiria mbalimbali ikiwemo tovuti hiyo kuonekana ni mpya ikiwa ina miezi mitatu tu, huku ikiwa na hali ya orodha ya vizuizi vya Domaini ambapo kiwa tovuti imeorodheshwa kwenye orodha ya vizuizi, inaweza kuwa inahusiana na shughuli kama malware au spam​

screenshot-2026-03-06-211817-png.3553832

screenshot-2026-03-06-213000-png.3553833

screenshot-2026-03-06-212712-png.3553834

screenshot-2026-03-06-212753-png.3553835

screenshot-2026-03-06-212753-png.3553835

screenshot-2026-03-06-212834-png.3553836





​
kwa vyanzo gani vya mapato na biashara gani kubwa, Anglia article iliyoandikwa na citzen
 

Attachments

  • Screenshot_20260309_144818_Instagram.jpg
    Screenshot_20260309_144818_Instagram.jpg
    292.8 KB · Views: 35
😅😅 za kuambiwa changanya na zako. Tanzania hakuna biashara ya ukwasi kama siasa hasa kama ukicheza nayo vizuri, isipokubaka
 
kwa vyanzo gani vya mapato na biashara gani kubwa, Anglia article iliyoandikwa na citzen
Feki website nyengine, picha ya website nyengine. Angalia picha ni Citizen na juu kwenye website ni Pertamina invest.

Pia Trilioni 80 ni hela nyingi mno, hata Dangote Tajiri zaidi Africa hio hela Hana.
 
Feki website nyengine, picha ya website nyengine. Angalia picha ni Citizen na juu kwenye website ni Pertamina invest.

Pia Trilioni 80 ni hela nyingi mno, hata Dangote Tajiri zaidi Africa hio hela Hana.
Watanzania wakikosa kazi wanaingia kwenye uzushi. Siku ikijakujulikana kwamba kinachosambazwa ni taarifa feki tayari sumu imeshasambazwa.

Chuki ya October 29 2025 ilisambaa kijinga namna hii, watu bila aibu wanatunga habari za kugushi kisa wanazisambaza mitandaoni.
 
Wongoooo.......hiyo ni budget ya nchi. ana hela ila hazifiki huko.
 
Back
Top Bottom