Ni kweli kuna dawa za biashara?

Senior masai

Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
88
Reaction score
89
Here comes,

Waungwana kuna hili swala la kufanya biashara iende smoothie,, kuna rafki yangu kanishauri swala la kwenda kwa baadhi ya mashekhe ili tukapatiwe dawa kwa ajili ya biashara iende vema.

Sikufanikiwa kukubali ila yeye alienda na akaanza biashara yenyewe ikaenda vizuri miezi miwili lakini kwa sasa kafunga ofisi,, sasa kwa wataalam wa mambo mwenye kunieleza kitu chochote kuhusu hili swala niongeze upeo.
 
Here comes,,
Waungwana kuna hili swala la kufanya biashara iende smoothie,, kuna rafki yangu kanishauri swala la kwenda kwa baadhi ya mashekhe ili tukapatiwe dawa kwa ajili ya biashara iende vema,,
Kafunga kwa sababu zipi?
 
Ujinga mtupu
 
Dawa kwenye biashara, kazi (vyeo hasa serikalini) zipo ila inabki swala la imani.

Mm nina rafiki zang mwaka jana wameenda malawi (nyanda za juu kusini wanaita KUJILIPUA) sasa hv wanabishara kubwa vibaya mno ila kuna deni la kulipa kwenye kila kitu unachokifanya ukiteleza kidogo tu unapotea mazima.

Dawa zipo zinafanya kazi na MUNGU yupo na anafanya kazi so kazi ni kwako ukae upande gani, ila chagua upande mmoja ukikaa katikati kuna balaaa ndugu.
 
Thread nzuri sanaaa.

Imani za kishirikina zipo.
Tembelea Mafinga uone vijana wadogo wafanyabiashara wanamiliki pesa kuliko umri wao ila NI WALOZI BALAA.

Mshana Jr ataongezea.

#YNWA
 
Ukiskiliza stori za wapumbavu na wapuuzi hausongi mbele. We achana nao, ulivyoumbwa ni dawa tosha, fanya tafiti za biashara yako, jua wateja wanachotaka unakipata wapi kwa bei ya chini na kuwauzia kwa bei ya faida inayokubalika.
Hiyo mifumo iliyobaki ni ya kizamani na haina tija.
Ila kama unahisi umekuwa mvivu, na una fungu la kufanya utafiti kwa waganga nenda mkuu.
Next comment, ngoja nijifanye kukubashiria uone kama kwa asilimia kadhaa sitakulenga sahihi
 
Unauza bidhaa mchanganyiko, eneo lako la biashara sio mbali sana na taasisi kama shule, kanisa au msikiti au kampuni.
Umekuwa unajiuliza sana kuhusu watu wanaopata mali haraka kiasi kinachokuwazisha kuwa mbona unapambana lakini haupati kama wao, mpaka unahisi kuna namna ya ziada isiyo ya kawaida.
Kuna watu wanahisi unapata nyingi wakati wewe unaona unapata kidogo.
**********************************
Ushauri simple: je una database ya wateja wako ikiwa na taarifa kama namba ya simu, mara ngapi anarudi kununua bidhaa?
Una takwimu ya siku, wiki, miezi ambayo unakuwa na mapato kidogo au mengi?
Unafanya mawasiliano na wateja wanaonunua zaidi na kwa namna ambayo hawatahisi unawashinikiza kununua?
Unajaribu na kujifunza njia tofauti za kutafuta wateja?
 
Cjakupata , unamshauri au
 
Kamwe usiingie huko .. Utajiingiza kwenye shida ambazo hutaweza kuzimaliza... Sana sana ukiweza tumia chimvi kwenye biashara yako..hiyo ni remedy bora na haina maagano
 
Kamwe usiingie huko .. Utajiingiza kwenye shida ambazo hutaweza kuzimaliza... Sana sana ukiweza tumia chimvi kwenye biashara yako..hiyo ni remedy bora na haina maagano
Kaka kama hutojali tupe mwongozo namna yakutumia chumvi kwenye biashara zetu mkuu ... natanguliza shukurani 🙏🤝
 
Siku zote shetani hakupi kitu bure lazima utalipia hata kwa kuchelewa,,mungu ndo anaweza kukupa utajiri wa kudumu tuu.
 
Good customer care na Branding ndo dawa tosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…