Ni kweli kuna Limbwata au ni vitisho tu?

Ni kweli kuna Limbwata au ni vitisho tu?

Labda tungepata maoni kutoka kwa watu wa Tanga au Mbeya!
 
😂😂😂 wasituchukulie pouwa
Halafu unapewa maelekezo dawa unafanya mwenyewe, utaona kimtu kinavyoweweseka!!
Kumtoa mpaka umchoke wewe!! Ila la maokoto ndo muhimu, wadada mje msione aibu. Ex kakuacha bado unampenda dawa ipo, wabahili dawa ipo, na wale wa kisasi dawa ipo. Usipofanikiwa narudisha pesa yako 🤣🤣🤣🤣🤣
Inakuaje mnakuwa na roho ngumu hivyo?
 
Limbwata lipo sana, huko KAGERA liliibuka Limbwata aina ya SHUNTAMA, acha kabisa wanaume waligeuzwa kama mazuzu , hii kitu ilileta shida miaka hiyo ya 90 mpaka 2000, ilibidi mpaka mapadre na viongozi wa dini waingilie kati na kuhubiri hilo janga makanisani mpaka likatoweka! Nasikia wamama walikuwa wanavizia maji yaliyooshewa na maiti halafu wanafanyia hiyo limbwata basi mwanaume anakuwa hajitambui Kwa mkewe kama maiti!
Kuna mshikaji wangu alipigwa limbwata na mwanamke wa kigoma Mmanyema , daah ofisi nzima ilijua kwamba mwenzetu kakamatika, alikuwa anafua, anapiga deki anachuma kisamvu , siku tukimfuata TWENDE nae viwanja anaweza kupiga hatua kadhaa kuondoka mwanamke akimuuita tu jina jamaa ataghairi safari na kuomba arudi home fasta , Kuna siku tulifanikiwa kumnunulia pombe alipokaliza kunywa alitafuta mapipi na vitu vya kukata harufu ya bia Ili mke asigundue mshikaji kanywa , Yaani mambo yalikuwa mengi , hatukuwa na la kufanya kumnsuru mshikaji ilibidi tumtafute mama yake MZAZI aje amnusuru mwanae, baada ya kunusurika jamaa aliokoka akawa mlokole kabisa,
Kuna mbinu za kujidhatiti dhidi ya haya makitu. Maana inatisha sana hizi habari zake.
 
Back
Top Bottom