Ni kweli hilo halina ubishi..
Unapolala na mwanake spiritual mnaunganika na kuwa nafsi moja (kitu kimoja ).. bahati yake inakuwa yako mkosi wako unakuwa wako... ila pia utatembelea ki smart chake kama nyota yake kali kukuzidi kuliko wewe kwenye mafanikio au kama nyota yako kali kuliko yeake atakuwa mnufaika, na kama mmebalace pia nzuri...
ndio maana kuokota okota ni hatari sana pia, unaweza haribu maisha yako kwa usiku mmoja na kabao kamoko tu.... ngono nyuma yake ina mafumbo makubwa sana, kama watu wangejua wangekuwa waoga sana kutiana tiana ovyoo.. nikitulia nitashusha nondoo iliyoshiba.. ili atae taka kuelewa aelewe na mmbishi akaze shingo pia
Jana niliona uzi wako ukizungumzia masuala mbalimbali ya nyota, ndoto nk.
Sasa Mimi niliota ndoto kuhusu Jambo ambalo liliniachia maswali mengi, Kama hutojali naomba unisaidie kunielewesha juu ya hii ndoto.
Niliota nilikuwa najiandaa na mtihani muda unafika wa kupanga foleni kuingia kwenye chumba cha mtihani, ghafla nakumbuka sina ID nikaanza kufanya juu chini ili nirudi nyumbani kuifuata.
Kuangalia vizuri nyumbani mbali, lakini ikabidi nianze kukimbia haraka, ghafla nikakanyaga vitu vya watu, wale watu waliponiona wakaanza kunifukuzia, nikapita njia nyingine ambayo ni mzunguko.
Wakati najaribu kuona namna gani naweza kuiwahi ID, wazo likanijia nikodi bodaboda zilizo maeneo hayo, nikafanikiwa. Ile tumeondoka nikawa namwambia boda aongeze spidi ili niwahi kuchukua ID halafu anirudishe tena.
Sasa ghafla spidi ikapungua kumuliza akasema nimlipe kwanza, Basi nikamlipa baada ya kumlipa ndo ananiambia pikipiki imeharibika, kucheki muda ni saa tatu na mtihani ulikuwa unaanza saa mbili, na sheria ukichelewa nusu saa haufanyi mtihani.
Basi nikawaza ngoja niachane na ID nirudi eneo la mtihani ili nikawabembeleze kwa kutunga hata Sababu yenye mashiko nifanye mtihani bila ID, wakati nawaza hivyo naona jamaa watatu wapo na bodaboda wanakuja, miongoni mwao Kuna jamaa nilikuwa namfahamu nikaomba ashuke mtu mmoja wanipakie mimi ili niwahi kunako mtihani.
Ile tupo njiani nashtuka kutoka usingizini...
Basi nikawaza juu ya ndoto hii nimekosa majibu mpaka Sasa.