Tyrone Kaijage
JF-Expert Member
- Jul 19, 2021
- 1,617
- 3,405
Jana niliona uzi wako ukizungumzia masuala mbalimbali ya nyota, ndoto nk.
Sasa Mimi niliota ndoto kuhusu Jambo ambalo liliniachia maswali mengi, Kama hutojali naomba unisaidie kunielewesha juu ya hii ndoto.
Niliota nilikuwa najiandaa na mtihani muda unafika wa kupanga foleni kuingia kwenye chumba cha mtihani, ghafla nakumbuka sina ID nikaanza kufanya juu chini ili nirudi nyumbani kuifuata.
Kuangalia vizuri nyumbani mbali, lakini ikabidi nianze kukimbia haraka, ghafla nikakanyaga vitu vya watu, wale watu waliponiona wakaanza kunifukuzia, nikapita njia nyingine ambayo ni mzunguko.
Wakati najaribu kuona namna gani naweza kuiwahi ID, wazo likanijia nikodi bodaboda zilizo maeneo hayo, nikafanikiwa. Ile tumeondoka nikawa namwambia boda aongeze spidi ili niwahi kuchukua ID halafu anirudishe tena.
Sasa ghafla spidi ikapungua kumuliza akasema nimlipe kwanza, Basi nikamlipa baada ya kumlipa ndo ananiambia pikipiki imeharibika, kucheki muda ni saa tatu na mtihani ulikuwa unaanza saa mbili, na sheria ukichelewa nusu saa haufanyi mtihani.
Basi nikawaza ngoja niachane na ID nirudi eneo la mtihani ili nikawabembeleze kwa kutunga hata Sababu yenye mashiko nifanye mtihani bila ID, wakati nawaza hivyo naona jamaa watatu wapo na bodaboda wanakuja, miongoni mwao Kuna jamaa nilikuwa namfahamu nikaomba ashuke mtu mmoja wanipakie mimi ili niwahi kunako mtihani.
Ile tupo njiani nashtuka kutoka usingizini...
Basi nikawaza juu ya ndoto hii nimekosa majibu mpaka Sasa.
Hii wanasemaga kuna jambo kubwa la stage ya kimaisha hujalifanya bado na unaliwazia sana mfano, kuoa/kuolewa, kujenga, kuanzisha biashara kubwa unayoiwaza miaka etc
Ila watakuja kunyoosha zaidi