Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kwamba ukiwa unaishi geto, hata wale waishio nyumbani kwa wazazi, wewe kijana wa kiume, halafu mathalani wakati unapika chakula chako ukaonja chakula kwa kutumia ule mwiko wa kupikia.
Au wakati unakula chakula, ukawa unakula mulemule kwenye masufuria ya kupikia, badala ya kupakua kwenye sahani, na unakuta mwingne hadi anakunywa kama ni supu ya maharage, rosti maini au nyama, kwa ule utamu wa kukombelezea ananyanyua sufuria na kunywa kilichobakia; sasa tulikua tukiambiwa kwa kufanya hivyo tutachelewa kuoa ama kutokuoa kabisa.
Je, kuna ukweli wowote kwenye hili wajuvi wa mambo na watafiti wa kijamii au ilikua mbinu ya kuchochea vijana kuoa na kufukuzwa nyumbani kiaina?