Ni kweli kuwa Mbowe aliondoa ukomo wa uongozi kwenye katiba ya CHADEMA kwa hila?

Pengine ndiyo maana kuna watu wanawaita nyumbu.
 
Namaanisha haikua deal yaani Kama chauma,mwenye chauma akibadili Katiba nani atahamaki!?
Bado hujanielewa; haikuwa deal kwa nani? wanachama? Ok.

Hata kama haikuwa deal kwa wanachama, then kwanini wajumbe wa mikutano yao nao wasiulizie hilo suala kwenye vikao vyao?
 
Tunapopambania katiba mpya kuimarisha demokrasia lazima tuanze kwenye vyama vyetu hilo la chadema ni doa sio kwa ngazi ya mwenyekiti tu bali nafasi karibu zote ni walewale miaka yote.mabadiliko ya viongozi ni muhimu sana kuleta maendeleo ya vyama
 
Mpaka leo hakuna kiongozi shupavu ambaye anaweza kuwa mwenyekiti pale Chadema?
 
Hatuna MAJI wala UMEME hapa home Ukonga sababu Mbowe alibadili katiba na kuwa Mwenyekiti wa kudumu CDM?

CCM wakiona tunajadili mambo kama haya na kuacha kuwa hold accountable kwa huu uchumi mbovu,huwa wanatucheka sana
Wakati mnataka katiba nzur ya nchi basi tengenezen katiba njema ya vikundi vyema.
 
Nimeona hii habari huko Twitter. Inasema kuwa Mbowe alikuwa mwenyekiti wa CDM mwaka 2004. Wakati huo katiba ya chama ilikuwa imezungumza kuwa kutakuwa na ukomo wa miaka kumi kwa mwenyekiti.
Ni kweli Mbowe alipoingia kuwa Mwenyekiti wa Chadema, katiba ya Chadema ilikuwa na ukomo wa uongozi mwisho ni vipindi 2 vya miaka 5 jumla ni miaka 10.
Mwaka 2006 yalifanyika mabadiliko ya katiba. Lakini suala la ukomo wa uongozi halikuzungumzwa kwenye mkutano.
Ni kweli 2006 Chadema walifanya mabadiliko ya katiba na ni kweli kipengele hicho hakikujadiliwa.
Inasema kuwa katiba ilipoendwa kuchapwa, Mbowe akaondoa kipengele cha ukomo wa uongozi kinyemela. Hii ndiyo hadi leo mwaka wa 20 bado ni mwenyekiti.

Madai haya yanaukweli wowote?
Ni kweli katiba ilipoenda kuchapwa, hicho kipengele hakikuwepo, kiliyeyuka ila aliyekiyeyusha sio lazima awe ni Mbowe.

Hili jambo tuliisha lijadili humu kwa kirefu, Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Dr. Slaa alikuwa KM na alichangia Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

na JJ Mnyika akiwa Mkurugenzi wa Habari wa Chadema pia alichangia Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Nyuzi nyingine zinazohisiana na hili ni hizi Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA Elections 2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu! ila juzi kati hapa hili jambo Lissu kalifafanua vizuri kabisa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

P
 
wewe ni legend
 
Kwanini usiulize kuwa ni kweli MAGUFULI aliagiza Tundu lussu Auawe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…