Ni kweli kuwa watu wote walioko kwenye ndoa au waliooana wanapendana?

3. Kupika - msichana kila mkipanga date anakupa/anaomba offer ya kula nje, huwezi jua kama anaweza kupika au la. Na kwa kuwa mapenzi yako fire fire wala mwanaume hawezi kushituka kulazimisha kwamba anataka kula chakula kilichopikwa na mpenziwe. Na kama msichana ni mtoto wa geti kali, ukianza kumwambia kupika unahisi mtapoteza muda zaidi badala ya kuendelea na yale mambo mengine ya chumbani ama kukaa pamoja mkipiga stori.


Keil....mie wakakti naanzana na shem wako yeye alikuwa anaishi arusha mie moshi, wakakti huo kila wkeend nina semina arusha...lol, kupika lilikuwa jaribio langu la kwnza, nikiwa kwake hakuna cku tutasema tunaenda kula hotel/nyama choma bar...nope, tutakula home tunaenda kunywa bar!...huo mtihani nilifanikiwa kwa asilimia 100, sasa baadhi ya wadada wa cku hizi wao ni ooh tupitie cjui steers, cjui best bite hakuna walijualo...
 
Sawa kabisa kamanda. Ndoa ni ndoano.

Ndio maana waliokuwemo wanataka kutoka na wasiokuwemo wanataka kuingia.

Ila kiukweli kama unaoa/onaolewa na mtu Usiyempenda. Hiyo ndoa haitakaa idumu kwa sababu Upendo huvumilia yote, hata yale yajitokezayo ndani ya ndoa. Bila kumpenda mtu, huwezi kumvumilia katika yale unayoyaona ni kikwazo kwako. Kwangu mimi naamini ndoa zote zilizodumu ni kwasababu wanandoa WANAPENDANA.
 

Ur right my dear!U nailed it.Hivi ulisomea shule maalumu(special school?)
 
Hapo si unakubaliana na mimi kuwa hicho ndicho kinachosababisha ndoa nyingi kuvunjika?
 

Can you say this again?
 
Hahahahaha! Haya bana, ila kitafika kipindi utagundua huu upupu naouandika huku kimasihara kuwa ni UKWELI tena UKWELI MTUPU. Time will tell.

Hahahahahaaaa. Itabidi twendwe PM kidogo.Tusijetoa siri za ndani........
 

Hiyo ni kweli, lakini walianza kupendana lini? Kabla au baada ya kuingia jela (kwenye ndoa)?.

Unanikumbusha kitu kinaitwa "marriage triangle" ambayo inajumuisha, LOVE, SEX (one body) na LEAVING (kuachana na baba na mama na kuishi na mume/mke). Je kwenye ndoa kipi kinatangulia (what is is the enty point)? Does it matter?
 
Marriage is not living with the person u luv, but living with the person you cant live without.
 
hapo sasa kidogo inakuwa ngumu kujibu kwa sababu ukitizama enzi za wazee wetu, pointi ya mapenzi haikuwepo kabisa (wengi wao waliolewa na watu ambao walijuana baada ya kuoana) na kutimiza wajibu kwa wazee na jamii ndio ilikuwa pointi muhimu sana. Licha ya hivyo ndoa tuliona kuwa zilidumu.

sasa hapa ama kuna mawili..........(au matatu)

1. kuwa wazee nao hawakutaka kuwa kwenye ndoa hizi na zingevunjika lakini hawakuwa na guts za kutosha ( labda nguvu za wazee na jamii ziliwazidi nguvu mno na kuachwa waliona kuwa aibu) lakini wanawake wa sasa hawaoni tabu wanavunja ndoa

2. kuolewa kwa ajili ya kuridhisha jamii PLUS kujiridhisha kwa kuchagua unaempenda sio sababu inayopelekea kuvunjika kwa ndoa.

3. Ndoa ambazo watu walioanana kwa Mapenzi TU naweza kusema sizijui kwa hiyo siwezi jua zinadumu kwa kiasi gani ( yaani hapa wamependana lakini wazee wamepinga na jamii ikawachukia)
 
LOVE comes first!!!
 
Ur right my dear!U nailed it.Hivi ulisomea shule maalumu(special school?)


dearest, niliingia kwenye game bila kujua maana halic ya game, niliwahi kuingia kwenye game nikidhani ninavyompenda ndio maisha yote yatakuwa tambarare kama tulivyokuwa, ckuweka kichwani mambo ya familia mbili kuungana yaani niliingia ingia tu, imenifunza mambo mengi sana, pamoja na ya jamii inayonizunguka, bac nimejifunza mambo mengi, na mistakes wanazofanya ndugu, jamaa na marafiki ahh bac nikajua huu ulimwengu sio kama nilivyoujua mwanzoni.
 
Chrispin ...........wewe unazungumzia mtu kuolewa na mtu ASIYEMPENDA lakini akaridhisha jamii tu?! mimi nazungumzia mtu kuolewa na mtu ANAEMPENDA lakini akaridhisha na jamii pia.

hiyo ndio hoja yangu tokea mwanzo ..............kuwa mapenzi bila sababu nyengine pia hayapo kiuhalisia kwa wanawake karibia wote

sababu za ziada kwa wengi ni dini, wazazi, jamii, security, status............even money
 

Kwani hakuna watu ambao hizo sababu za ziada zinakuwa na uzito kuliko mapenzi?
 
Kweli ila hiyo ndo halisi kwa watu tulio wengi au nadharia (ideal Vs. reality)? Binafsi nilianzia kwenye sex, then love kabla ya kujivisha kitanzi.

wanaume wengi huwa wanaanzia hapo, kwa sisi wanawake asilimia kubwa tunaanzia na love.
 
Chrispin na wewe ulioa kwa sababu ya nini?
Teamo Je ?
Na wewe bana, haya soma hapa chini nilishasema mbona.

 
Chrispin na wewe ulioa kwa sababu ya nini?
Teamo Je ?


Kweli ila hiyo ndo halisi kwa watu tulio wengi au nadharia (ideal Vs. reality)? Binafsi nilianzia kwenye sex, then love kabla ya kujivisha kitanzi.
To me Love has nothing to do with sex. Ndo maana nilimpenda mamito wangu kwa zaidi ya miaka mitatu ndo tukasex. Niliposex tu, hapo hapo nikatangaza nia. I got what I wanted!!
 
Kwani hakuna watu ambao hizo sababu za ziada zinakuwa na uzito kuliko mapenzi?

wapo wengi tu...............mijini unakuta ni sababu za pesa zaidi na vijijini ni sababu za wazazi na jamii.

ila hapa nilikuwa naweka sawa tu kuwa mwanamke kuolewa kwa mapenzi tu haiko ...........ataolewa kwa mapenzi plus alpha. sasa sisi tuliotoa orodha ya sababu za kukubali kuolewa (hatukutaja mapenzi pekee) tusionekane wa ajabu sana. mapenzi bila alpha hiyo ni almost hayapo kwa wengi waliolewa

japokuwa alpha bila ya mapenzi ( atleast mwanzo wa ndoa) ipo sana tu katika jamii
 
LOVE comes first!!!

Kuna mifano mingi tu ya watu ambao walikuwa wanapendana sana tu.Na hata kujuana tabia vizuri,lakini baada ya muda wakiwa ndani ya ndoa upendo unaisha,tena wanakuwa maadui wakubwa(ninao mfano hai) Hii inatokana na nini wakuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…