Naomba utueleze mfano wa hizi tabia ambazo sio rahisi kuzijua kabla ya kuoana..........
Japo swali halijaelekezwa kwangu, lakini naomba nitoe mifano kwa ufahamu wangu.
1. Uaminifu - kama wapenzi wanakutana kwa appointment tu; mtu ambaye siyo mwaminifu anaweza kuhakikisha hagoganishi magari.
2. Uchafu - kuna wavulana siku akiwa anatembelewa na mpenzi wake ndipo ataweka nyumba soap soap na kuiweka ikiwa more organized, subiri uje umvamie siku moja bila taarifa inaweza kuwa aibu. Pia wapo wasichana ambao siku akiwa na date na bf wake ndipo anajiweka soap soap na anakuwa na kufuli special za kuendea kwenye hizo date, ukimvamia nyumbani unakuta kalunda vikufuli havijafuliwa wiki nzima, na hata kitanda kinaweza kuwa hakijatandikwa kwa wiki nzima.
3. Kupika - msichana kila mkipanga date anakupa/anaomba offer ya kula nje, huwezi jua kama anaweza kupika au la. Na kwa kuwa mapenzi yako fire fire wala mwanaume hawezi kushituka kulazimisha kwamba anataka kula chakula kilichopikwa na mpenziwe. Na kama msichana ni mtoto wa geti kali, ukianza kumwambia kupika unahisi mtapoteza muda zaidi badala ya kuendelea na yale mambo mengine ya chumbani ama kukaa pamoja mkipiga stori.
4. Ulevi - nina mfano hai. Nina cousin wangu (msichana) alikuwa anakunywa pombe kama hana akili nzuri lakini mchumba wake alikuwa hajui na mpaka wakaja kufunga ndoa. After 3 yrs ndio mume anakuja kugundua kwamba mkewe anakunywa pombe.
Lakini kasoro zote hizo inategemeana sana na closeness iliyopo kati ya wahusika, je wanatembeleana mara kwa mara? Pia distance iliyopo kati ya wahusika, siyo mmoja yuko Dodoma na mwingine yuko Dar hapo ndio hasara kabisa maana ukiwa unaenda kumtembelea lazima utoe taarifa ili ku-avoid kukutana na kufuli mlangoni.
Pia wahusika wanatakiwa kuwa huru, waweze kutembeleana any time hata bila miadi. Lakini kama msichana anaishi kwa wazazi ama walezi nafasi hiyo inakuwa ngumu na matokeo yake ni maumivu.