Ni kweli kwamba nafasi za polisi zimetoka?

Zimetoka,ila ni kwa fom six wa 2012,fom zipo kwa wakuu wa shule,na makamanda wa mikoa,na wilaya,tovuti ya polisi.5
 
so ni zamu ya kidato cha sita....
kazi kweli kweli unatakiwa ufaulu vizuri form six then umri 18 - 25
 
Nackia zimetoka tujuzane wana jf kama ni kweli
Yah,ila kweli serikali kigeugeu.Walisema wangewachukua wahitimu wa JKT kujiunga na vyombo vingine vya usalama,mfano TISS,POLISI,UHAMIAJI,MAGEREZA.
Sasa nashangaa eti wameamua kurudisha ule utaratibu wa zamani.Ssa hawa vijana waliomaliza JKT juzi waende wapi au hakuna waliyemaliza form six kati ya hao vijana wa JKT?
 
Ivi kuna mtu anayefaulu vzr form 6 afu akaprefer kujiunga na police?
 
Huko police labda waliofeli mtihani wa kidato cha sita na waliotelekezwa na ndugu na jamaa waweza kwenda.
 
TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni.
Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa.
Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku.
Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa.
Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi.

A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI
1. Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
3. Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
4. Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
5. Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.
6. Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.
B: MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.
3. Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:
• Ofisi ya Mkuu wa shule
• Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu
• Pata fomu hapa(sel-form)
 
Mkuu umejitahidi sana ku draft hili tangazo ila umeharibu sehemu ndogo sana. Wanataka waliomaliza mwaka 2012, wakati hao form 6 wenyewe hata mitihani hawajaanza bado!!?
 
nimelichukua kama lilivyo hapo...
 
Hii ya form 6 waliomaliza mwaka 2012??? kweli wako tayari na majibu yao yameshatoka? mbona inachanganya hapo kidogo.
 
Nimeliona tangazo lenyewe halina deadline sijui wanasubiria hadi majibu ya form 6 yatoke mwezi wa 4 ndio waweke hyo deadline yao.!!

Sorry wakuu, mbona nimefungua webu yao ya 'moha.go.tz' silioni, au ukishafungua lipo sehemu gani?
 
Polisi ss mishahara yao mizuri ndo mana wengi tumeweza kumudu kununua magari makali!!
 
TANGAZO LA AJIRA

Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.

Angalau kidogo wangechukua graduate ningesema wako serious, xo hao form six watakuwa na mbinu za kisasa za kuondoa changamoto zilizopo?
 
wanapelekwa training mkuu.kwan graduate ana nin cha zaidi?
 
Back
Top Bottom