Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Mbona akina Dr Ben Carson wamesoma Yale University US, lakini wana MD, Mmed(Paed), Phd. Tena ni ma Neurosurgeon
 
Usipende kuandika mambo usiyoyajua, mimi nimesoma Kharkov mji aliosoma Prof Janabi miaka ya 90 katikati mpaka 2000 mwanzoni, na masuala ya medicine ya Ukraine ninayaelewa japo sio kwa kina.

Sio kweli kwamba mwili wa mzungu hauguswi na doctor mweusi, umeandika pumba tupu, yaani bull shit.

Punguza siasa za chuki humu mitandaoni, huyo mtu anayekutuma umchafue Prof Janabi mwambie atafute shughuli nyingine ya kufanya imuingizie kipato sio kuishi kwa kuchafua CV za watu.
 
Dah Unaamini Kwamba Janabi sio Daktari Bingwa..
Kweli leyman Wakiweza Kuandika wanaandika Vitu vinakeera...

Kama Mnamchukia Samia Mchukieni Ola msichukie Fani ya Kidaktari na Kuanza kuleta Dharau soon Mnanitafutia Bann Naona kabisa
Dr Mambo, watanzania ni jamii fulani ya kipumbavu sana, ni kuwavumilia tu. Kila mtu anajaribu kuidharau taalum ya mtu wakati hana uwezo wa kusoma medicine hata mwaka wa kwanza akaufaulu.
 
Nimecheck insta yake nadhani kaifuta
CV imeondolewa Instagram ingawa watu wamesha download! Kwanini Prof Janabi ameiondoa CV aliyoiweka mwenyewe ktk kuanza kampeni ya safari yake ya WHO! Je! Ni kweli kuna mambo hayako Sawa? Tunasubiri alete mpya tulinganishe!!!

Narudia tena kama TAIFA tunaenda kupambana na Africa nzima! Muda huu wameshachambua kila kitu kwenye taaluma ya mgombea wetu! Ni vyema busara itumike nchi isiingie
Ktk kashfa!!

Huu ni ushauri TUU ktk kuendelea kuiheshimisha mamlaka yetu tukufu! Inawezekana hii CV iliyofutwa ndiyo ilipelekwa kwa Rais na kwa kweli ilikuwa appealing!!

Queen Esther
 
Nimefanikiwa kuiona inakurasa (page) 18 .

Nahisi ndio itakuwa hiyo nahisi kaiondoa maana imekua mapema Sana kufanya hivyo labda
 
WHO utata huu,umefika😂 hata kabla hajaomba nafasi husika

Pia WHO wanajiuliza,mteule wao ambaye alikuwa hajaripoti kazini alipatwa nani?
Na kabla ya kwenda India kutibiwa alitibiwa hospital ipi hapa Tz?
Na no nani mkuu wa Hospital hiyo?
Maswali huko WHO ni mengi kuliko majibu
 
Maamuzi ya mtu kwenda kutibiwa sehemu Fulani ni maamuzi binafasi hayahusiani na Taifa. Wewe unaweza kuamua uende kutibiwa hospital Fulani na hakuna atakaekupangia au kukukataza ikiwa hospital hiyo haipo katika level ya kuhudumia tatizo lako au haina vifaa tosha au watalamu tosha watakupa Referral (rufaa) uende sehemu nyingine..

Karibu kutumia uelewa usilete Chuki za Ajabu
 
Hapo nimekupata mkuu. Uwiano unakosekana sometimes, mwenyewe kuna sister alinipa vyeti vyake nifuatilie ile taasisi iko karibu na ikulu. Ngazi walizoweka ni changamoto yeye hajafuata hizo, kwanza kasoma mtaala wa kimataifa, hajaenda A level, kasoma nje ya nchi ngazi zote alafu chuo kasomea Wuhan, China.

Mpaka wanakuja kugrade udaktari wake wa meno sijui walifanyaje.
 
Mkuu, kwani tumekukosea nini? Mbona unajaribu kutupiga kamba nyepesi hivyo? We huogopi?
Hii ni Harvard
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…