Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Kwa hiyo medicine ya Urussi sio internal medicine
 
Uk
Natamani ungesema neno kuhusu sifa/taratibu za kuwa /kusomea Udaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, maana, ndiyo Hoja hasa ya Mleta mada kuhusu Prof.
Ukimaliza miaka mitano ya udaktari unaruhusiwa kwenda kusomea udaktari bingwa

Miaka ya udaktari inatofautiana nchi na nchi

Na ukimaliza sisi tunaita masters in medicine
Mmed
 
Mama yangu alitibiwa moyo na Dr Janabi.
Daktari yoyote anaweza na anaruhusiwa kutibu moyo popote, lakini linapokuja suala la kutibu moyo kwa ngazi ya kibingwa ni daktari bingwa pekee mwenye hayo majukumu.

Ukiona Daktari ambaye sio bingwa anatoa matibabu ya kibingwa basi ujue anafanya hivyo chini ya usimamizi wa daktari bingwa. Tofauti na hapo ni makosa.

Nakuhakikishia kwa 99% kwa elimu ya kutibu moyo aliyonayo Janabi (ya kawaida mnoo) tukisema akae pale JKCI kutibu moyo yeye mwenyewe (bila kusimamiwa na madaktari bingwa waliopo pale) huenda atapaswa kuishia kumpima mgonjwa presha na mapigo ya moyo tu, kwa sababu hana sifa za kutibu moyo kibingwa.
 
Kwa hiyo medicine ya Urussi sio internal medicine
Kuna tofauti kati ya Medicine (Md) na Mmed in Internal medicine, bila kujali ya Urussi, Tz au popote pale duniani.
Moja (Md) ni degree ya kwanza ya udaktari na nyingine (Mmed in internal medicine) ni degree ya pili ya udaktari (ndio udaktari bingwa) ikijikita eneo fulani ya kutibu magonjwa fulani fulani kama moyo, ubongo, figo, maini nk.

Sijui sana, labda wajuzi zaidi watakuja kutupa mwanga zaidi.
 
Tibalishe dk
 
Ulivyoleta uzi sikukubaliana na wewe ingawa sikuchangia, ila baada ya kufuatili now naungana na wewe
 
Jamaa mjanja mjanja tu.Ndo maana kafuta post ya CV yake kule Twitter.
CV yake aliyokuwa ameiweka kule ilikuwa imejaa uongo na ujanja ujanja mnoo. Sasa wakenya, waganda na waghana walishaanza kuichambua na kuipiga spana kiasi cha kuua the whole professional credibility yake. Na bora kafanya hivyo sasa, japokuwa amechelewa sana maana inaweza kuzaa mengi mnoo.
Watu hawajui tu, academic impersonation ni kosa kubwa mnoo kimataifa, inaweza kukufutia vyeti, titles nk.
 
Ulivyoleta uzi sikukubaliana na wewe ingawa sikuchangia, ila baada ya kufuatili now naungana na wewe
Hata mimi niliposikia hii kitu kwa mara ya kwanza mahali fulani (kutoka kwa hawa wakenya ambayo wanatudharau mnoo sisi waTz) nilipinga mnoo (maana nilikuwa Pro Janabi), lakini nilipochungumza kwa kina na kuuliza baadhi ya madaktari kimya kimya nikagundua kitu tofauti kabisa. Mtazamo ukawa tofauti kabisa.
 
Nitakuelewesha hapa hapa baada ya kudadisi na kuhoji watu kadhaa.
Ni kitu rahisi mnoo kuelewa.

Kwa mfumo wa taaluma ya udaktari hapa Tanzania unaosimamiwa na MCT, udaktari bingwa wa moyo ni ngazi ya tatu (miongoni mwa ngazi za juu kabisa) katika taaluma ya udaktari. Na mhitimu utatambulika kama superspecialist (Cardiologist). Na kufikia hiyo ngazi lazima uwe umepitia ngazi ya degree ya kwanza (bachelor) ya udaktari (Md), halafu ngazi ya degree ya pili (masters) ya udaktari (Mmed), na hapa lazima iwe Mmed in internal medicine (au Mmed in Paeditriac kama utatibu watoto moyo kibingwa)

Sasa Mmed in internal medicine ina uwanja mpana, ina mambo mengi na yote mhusika anajifunza kwa pamoja ikiwemo moyo, figo, ubongo, damu, ini, tumbo nk. Sasa Daktari akishasomea hiyo na kuhitimu anakuwa Daktari bingwa (specialist), na baada ya hapo ikitokea mhusika anataka kuwa mbobezi (super specialist) anachagua eneo moja tu na anakwenda upya kulisomea kwa kina zaidi. Akihitimu anakwenda MCT kule wanampa hiyo status ya kuwa cardiac Superspecialitist (Cardiologist)

Sasa Msc in tropical health sio sawa na Msc in Tropical medicine!. Why? Tropical health haichagui kama wewe ni Daktari (hata muuguzi anasomea) lakini Tropical medicine inajieleza kuweza kusomewa na Daktari tu, yaani Medicine.

Na Msc in Tropical medicine sio sawa Mmed in internal medicine. Kwanini? Tropical medicine ni kipengele kimoja tu katika Mmed in internal medicine ambayo imebeba vipengele vingi huenda zaidi ya vipengele 10.
 
Huyo ni tapeli kama matapeli wengine tu!!

Na huko WHO wanamjua vizuri. Anakwenda kuangukia pua
 
Tuweke hapa tujifunze jinsi ya kuandika CV
 
Mkuu nilikuwa najibu post uliyoweka kwa maneno yako mwenyewe hii hapa chini. Rudi ukarekebishe huu uzushi ufanye uungwana. πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½

Jibu ni NO.
Professor Janabi hajawahi kusomea hicho kitu, hana huo ujuzi, hajawahi kutambuliwa kuwa na hiyo sifa hapa Tz, na huwa hatibu hicho kitu. Kama huamini fika JKCI halafu uulize ni lini alitibu moyo katika level ya kibingwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…