Mimi kilaza wa mambo ya afya naomba nikuelewe hivi mkuu:
1. Msc ya Tropical Medicine sio kigezo sahihi kinachohitajika kwa daktari kwenda ngazi ya kuja kubobea magonjwa ya moyo. Msc hiyo ni hafifu, hata Degree holder wa Pharamacology anaweza soma.
2. Ili mtu akasomee kuwa Cardiologist inabidi kwanza asome Mmed, na sio Msc.
Lakini kwa maelezo ya
DR Mambo Jambo ambayo nilichanganya nikadhani Prof. Janabi ana Mmed ya Tropical Medicine kumbe ana Msc ya Tropical Health, je mtu mwenye Msc hiyo (badala ya Mmed) naye ana sifa za kubobea kwenye cardiology?
Wakuu kumbuka mwanzoni hoja ya ndugu Zanzibar-ASP ilikuwa Prof. Janabi hana Mmed ya Internal Medicine hivyo hana sifa. Kwahiyo nikataka kumtetea kuwa hana Mmed ya Internal Medicine ila ana ya Mmed ya Tropical Disease, sasa nazidi kuambiwa pia hana hiyo Mmed bali ana Msc ya Tropical Health.
Nimerudi kwenye CV yake naona MD, Msc. PhD.
Kwahiyo ndugu DR Mambo Jambo nakuuliza tena, Msc ya Tropical Health ya Prof. Janabi inafaa kuwa mbadala wa Mmed ya Tropical Medicine. Ili Zanzibar-ASP aridhike?
Update: Nimekuja kujua hapa kupitia kwa DR Mambo Jambo kuwa Mmed ile ni (Internal medicine Specified In Tropical Medicine). Mwanzoni nilijua Internal Medicine na Tropical Medicine ni vitu viwili tofauti, mnaandika kwa kifupi sana nyie waganga.