Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Mbona ana qualification za juu sana
Professor Janabi hana qualification yoyote ya kutibu moyo kibingwa, hana. Hakusomea popote na hakuwahi kutambuliwa na baraza la madaktari hapa Tanzania kama Daktari bingwa wa moyo. Na hata pale Muhimbili hajawahi kutibu moyo mtu kibingwa tangu awepo. Hana huo uwezo.
 
Hii Elimu yake inatusaidia nini kwa Kipindi hiki?

Jambo la Msingi aungwe Mkono.

Huu Upuuzi wa Elimu umebakia sana hapa kwetu Africa Mashariki.

Huko kwa Mabeberu kinachoangaliwa ni Uwezo wako Ku deliver.

Tuachaneni na Hizo mambo za Kuangalia Elimu , hazilijengi Taifa.
 
Utamaliza calories buree kuya elezea majitu ambayo yamesha kua na PERCEPTION ZAO ZA KI NEGATIVITY.
 
Mkuu ndio maana naonaga nayazidi maprof mengi tu😁😁😁
 
Utamaliza calories buree kuya elezea majitu ambayo yamesha kua na PERCEPTION ZAO ZA KI NEGATIVITY.
Njoo na facts, acha ushabiki.
Mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana Professor Janabi kutokana na namna anavyoamsha jamii kwenye masuala ya afya.
Lakini hili la kutokuwa na elimu husika ya kutibu moyo kibingwa halafu ajipashike lazima nilipinge. Nyeusi tuiite nyeusi na sio nyeupe.
 
Professor Mohamed Yakub Janabi ni mfano wa kuigwa, ni nadra wasomi wa kiTanzania ku share knowledge yao na watanzania wa kawaida.




Wasomi wahadhiri wa vyuo vikuu hawapo katika mitandao ya kijamii kuweza kutumia elimu waliyopata kwa kodi za raia wa Tanzania, kwa kurudisha kwa jamii kwa mtindo wa kuwapa ufahamu wananchi wa kawaida kuhusu masuala yawe ya afya, ujasirimali, kilimo cha kisasa, ufugaji, ufundi mchundo n.k

Wasomi wa mataifa yaliyoendelea wapo sana katika mitandao ya kijamii kwa kutoka nje ya ma Hall ya lecture na kutoa elimu kwa jamii pana iliyopo nje ya kuta za vyuo vya elimu ya juu.

Usomi maana yake ni kuleta mabadiliko na mguso kwa jamii pana na Prof. Janabi katika hilo ameutendea jambo kubwa usomi wake kwa jamii pana.

Kwa staili hii nadhani atakuwa miongoni mwa watia nia wakuangaliwa sana na kukubalika kufanya kazi WHO Kanda ya Afrika.
 
Acha uongo ndugu yangu.
Standard ya elimu ya utabibu kipindi cha USSR mpaka leo hii haijawahi kuwa bora kupita yetu katika kipindi chochote kile. Mhitimu wa Muhimbili amekuwa better dhidi ya hao wa USSR.
Unaishi kwenye historia za Kinjekitile Ngwale...standard ya bongo ilikua ni kujeuza risasi kuwa maji... that's Bongo medics & Chemistry
 
Daktari bingwa yoyote hapa Tanzania ni lazima awe na Mmed. Professor Janabi hana na hajawahi kuwa nayo.
 
Wasomi wengi wa kiTanzania ni kama waganga wa kienyeji kwa kuficha utaalamu wao.

Katika Tanzania ni maprofesa wachache kama Prof. Issa Shivji siasa / sheria, Prof. Janabi utabibu / elimu kwa umma (Public health), Prof. Prosper Ngowi wa Mzumbe University somo lake la kujiajiri ndiyo wasomi wachache wanaorudi kwa jamii kuwainua ufahamu waTanzania kwa elimu ya buree mtandaoni

Prof. Ngowi, Presenting Paper on Education for Liberation of the Poor in Africa at Nyerere Intellectual Festival UDSM, on 12.04.2018. Key issue; EDUCATION should Liberate the Poor Economically, should be relevant and demand-Driven


View: https://m.youtube.com/watch?v=gUu5YZEaPjk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…