babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 14,478
- 18,341
NAAMINI WOTE TUMESIKIA KISA CHA HUYU BWANA KUDAIWA kuhusishwa na wizi wa vifaa vya magari.na naamini pia asilimia 90 ya wote waliosoma au kusikia taarifa hizo wameamini kwamba huyu jamaa ni kibaka na hasa akihusishwa na madawa ya kulevya.simtetei huyu jamaa lakini tumpe pia haki yake kiubinadamu,katika yote hayo usikute huyu jamaa si mwizi na wala hajihusishi na vitendo hivyo,inawezekana kabisa kwamba kwa namna ingine kabisa amejikuta kahusishwa na hivyo vitendo bila hata yeye kuelewa kaingizwa vipi,au la aliuziwa mojawapo ya vifaa vilivyoibiwa na ndipo zigo la k**ba likamwangukia,na kwa bongo kila kitu kinawezekana,nakumbuka niliwahi kupakaziwa nimebeba madawa ya kulevya pale airport na wale jamaa eti usalama wa taifa waliniweka pale kwa masaa matano mpaka wakalazimisha kuninyanganya baadhi ya pesa nizlizotua nazo baada ya kugoma kutoa rushwa.walinivuruga akili kisaikolojia kiasi kwamba nikapata ajali ya kufa siku hiyo hiyo baadae ila mungu akasaidia nikapona.bado naandaa hicho kisa cha bongo ntakiweka hapa.kwa kweli siku hizi naichukia Tanzania,maana siyo ile nilikua nikiimba naipenda kwa moyo wote