Ni kweli maisha ya Messi wa Simba yako hivi?

Ni kweli maisha ya Messi wa Simba yako hivi?

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Ni nadra sana kunikuta najadili maisha ya mtu binafsi. Lakini kama mjadala huo utakuwa unahusiana na jambo lolote linalogusa public interests, basi huwa sina budi kujadili

Wiki zaidi ya moja iliyopita kumeendelea kuwepo kwa mvutano wa Ramadhan Singano aka Messi wa Simba na klabu yake. Katika hali ya kushangaza, blogger mmoja maarufu nchini (nadhani mtakuwa mnamjua tu) amemshawishi mchezaji huyo wa Simba kuonyesha hali ya maisha yake anayoishi, pengine kwa lengo la kuuonyesha umma kwamba mchezaji huyo amekuwa ananyonywa na klabu yake kiasi kwamba maisha yake yamekuwa duni ukilinganisha na ukubwa wa jina lake. Mchezaji huyo alipigwa picha akiwa ndani na nje ya nyumba yake na kuonyesha vitu vichache anavyomiliki katika gheto alilizamia kwa kaka yake

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu kipato alichonacho Messi na hali ile iliyoonekana. Baadhi ya vipato hivyo ni:
1. Hela ya usajili sh. milioni 13 yaani 13,000,000/= aliyopewa mwaka 2013
2. Mshahara kutoka Simba sh. 700,000/= kwa mwezi take home usioguswa na kodi yoyote
3. Gari aina ya Suzuki Carry 4WD la kubeba mizigo alilopewa mwaka 2013 bure na shabiki wa Simba Musley Luwah wa Oman, (kadiria mwenyewe kwa siku 'hesabu' yake ni shilingi ngapi anayoletewa na dereva. Kwa uthibitisho wa hili gari, soma hapa: Messi wa Simba azawadiwa gari - Global Publishers
4. Posho za klabu yake ambazo hubadilika mara kwa mara (mapato mtakadiria wenyewe)
5. Posho alizokuwa anapata wakati akiwa mchezaji wa timu ya Taifa - kila siku ya kuwepo kambini sh. 50,000/= pamoja na posho nyingine za kucheza mechi
6. Tangazo la biashara analofanya ITV la magodoro ya Dodoma maarufu kama kwa mzee Mangungu (mapato mtakadiria wenyewe)
7. Hela anazookoa katika matumizi anapokuwa kambini na Simba na Taifa Stars (gharama za Hotel malazi na chakula ni juu ya timu). Jaribu kufikiria ni asilimia ngapi ya muda wake katika mwaka anakuwa yupo kambini akila na kulala bure
8. Hili lingine ni personal sana sitalizungumza kwa undani, ila kwa ufupi hana watoto, familia wala wazazi wategemezi so hela nyingi anabaki nazo yeye

Sasa wenye akili mjiulize, ungekuwa wewe ndio kijana unapata mapato hayo, maisha yako yangekuwa ya kichovu vile?
-Vijana wangapi wanahangaika lakini hivyo hivyo wanajitahidi kujitegemea na si kuishi kwa kaka zao?
-Messi kusema ana maisha duni, huku sio kumkufuru Mungu?
-Kama amejibana kwa kaka yake kwenye single room na kuna TV na kitanda na viti vichache, ina maana kaka yake alikuwa hana fenicha yoyote kabisa isipokuwa alikuwa anamiliki chumba tu kitupu?
-Ni kweli pale ndipo anapoishi Messi au ana makazi mengine?

Maswali hayo nawaachia, akili mlizoambiwa za huyo mmiliki wa blogu inabidi mchanganye na zenu, halafu muone kama huyu Messi amefanya usanii wa kutuonyesha chumba feki au ndio chumba chake halisi
 
unaweza kukuta mkataba huo watangazo unamilikiwa na kiongozi fulani wasimba,yeye akapewa elfu hamsini au laki akamaliza kazi yake..kikubwa wachezaji wengi watanzania ni wale walio kimbia shule,wengi hata elimu ya utambuzi ni mushkeli sasa wanaishi maisha ya kindondo tu na kiswahiliswahili basi..Wachache sana ambao wanajitambua na wana usimamizi mzuri nadhani hawafiki hata 10%
 
Nmelisema sana hili. Huyu dogo amenishangaza mno. Either atakuwa anahonga sana au aliamua kuichafua tu klabu ya Simba.
 
Tuwe wakweli kabisa, kati ya mchezaji na club, nani mwenye uwezo wa kuchakachua mkataba? Yaani sSingano afoji sahihi ya viongozi, mhuri wa club nk? Au ni rahisi zaidi kwa club kuweka miaka mitatu badala ya miwili?

Na je vipi ule aliosaini eti wa mwanzo ulikosewa? hapa tatizo la Singano ni kutokwa kuwa makini basi. Alikwa na imani viongozi ni waaminifu. Wachezaji watarajiwa wa vilabu hivi wasome alama za nyakati.
 
Nmelisema sana hili. Huyu dogo amenishangaza mno. Either atakuwa anahonga sana au aliamua kuichafua tu klabu ya Simba.
Mnasema pesa ya usajili alipewa 13mil lkn kihalisia waliomleta Simba walikula 8mil na yeye 5mil tu kwa ahadi zingine hewa. Yani bongo mchezaji anaposajiliwa anaambiwa tunaandika pesa ya usajili 20mil lkn tutakupa 8mil unasemaje? Kibongobongo huwezi kuikataa hiyo hela japo unanyonywa huku unaona. Bongo ni zaidi ya ujuavyo
 
Hata kama alipewa 1m. Unahisi ni sahihi kwake kulala mzungu wa nne na kaka yake? hapa sijazungumzia mkataba wake na simba nazungumzia tu pesa hizo ndogo ndogo anazozipata.
 
hako kadogo kana matatizo halafu kanatumiwa kwa faida na maslahi ya watu fulani huku kenyewe kakijua kuwa kanasaidiwa
 
Tuwe wakweli kabisa, kati ya mchezaji na club, nani mwenye uwezo wa kuchakachua mkataba? Yaani sSingano afoji sahihi ya viongozi, mhuri wa club nk? Au ni rahisi zaidi kwa club kuweka miaka mitatu badala ya miwili?

Na je vipi ule aliosaini eti wa mwanzo ulikosewa? hapa tatizo la Singano ni kutokwa kuwa makini basi. Alikwa na imani viongozi ni waaminifu. Wachezaji watarajiwa wa vilabu hivi wasome alama za nyakati.

Hapa tumehama mada kidogo, sio nani kafoji mkataba ila je kwa muono wako wewe yale tuliyoonyeshwa na Shaffih Dauda ndo maisha halisi ya Ramadhani Singano?

Bila kugubikwa na mapenzi au chuki ya aina yoyote, kuwa huru kuchangia.
 
unaweza kukuta mkataba huo watangazo unamilikiwa na kiongozi fulani wasimba,yeye akapewa elfu hamsini au laki akamaliza kazi yake..kikubwa wachezaji wengi watanzania ni wale walio kimbia shule,wengi hata elimu ya utambuzi ni mushkeli sasa wanaishi maisha ya kindondo tu na kiswahiliswahili basi..Wachache sana ambao wanajitambua na wana usimamizi mzuri nadhani hawafiki hata 10%

Mtoa mada katoa vyanzo mbalimbali, mbona wewe umeainisha kimoja tu cha Tangazo la Mangungo?
 
Hapa tumehama mada kidogo, sio nani kafoji mkataba ila je kwa muono wako wewe yale tuliyoonyeshwa na Shaffih Dauda ndo maisha halisi ya Ramadhani Singano?

Bila kugubikwa na mapenzi au chuki ya aina yoyote, kuwa huru kuchangia.

Yale ya Shafii Dauda bila shaka ni kuongeza chumvi kwenye issue yenyewe. Hilo halina ubishi. Hoja ya msingi kijana anaonewa. Si mara ya kwanza huo ujanja ujanja wa viongozi kuwakomoa wachezaji.

Afadhali wachezaji wawe na mawakala wa kuwasimamia tena wasajiliwe TFF kabisa. Hatua ya kwanza, mchezaji mwenyewe awe na mkataba na wakala ili hoja zake zitambulike rasmi TFF!
 
Mleta mada nakupa hongera,umechambua vizuri sana,Mashabiki na wapenzi wa Yanga ndio wanaopotosha na kukuza jambo!
 
Sibonike, katika posts zako zote khs suala hili nafikiri hii ndo best post. Ni kweli dogo anaonewa kwa sababu haiingii akilini eti Ramadhani Singano afoji mkataba na Simba, lakini inavyoonyesha wakienda mbele zaidi atashindwa tu kwa sababu umeshafanyika uhuni mkubwa hapo.

Lakini ili kuokoa kipaji cha huyu dogo, watu kama Shaffih Dauda waache uchonganishi na ushabiki wa kipuuzi na kutafuta sifa za kijinga.
 
Pale Simba anae ishi kifalme ni Okwi tu wengine njaa zinawauma balaa.
 
Hata kama alipewa 1m. Unahisi ni sahihi kwake kulala mzungu wa nne na kaka yake? hapa sijazungumzia mkataba wake na simba nazungumzia tu pesa hizo ndogo ndogo anazozipata.

Unalijua jiji la darisalama wewe?
 
Hoja ni kuchakachuliwa mkataba. Suala la yeye kuishi kwa kaka yake ni matokeo ya ahadi hewa za Simba. Wenye kupaswa kujibu hoja hiyo ni klabu iliyoahidi kumpatia makazi nje ya mshahara wake. Rejea sakata la Kessy.

Acheni kutafuta huruma. Simba ndiyo iliyokiuka mkataba kwa kutompatia pesa ya pango. End of story.
 
Mleta mada nakupa hongera,umechambua vizuri sana,Mashabiki na wapenzi wa Yanga ndio wanaopotosha na kukuza jambo!

Shughulikeni na viongozi wenu wanaochafua sifa ya klabu kwa kugushi mikataba ya wachezaji wake.
 
Ngoja nipime iq yako kwa swali hili jepesi. Mesi na aveva na wenzake una mwamini nani? Ukipatia ntajua wewe wa mjini au umekuja juzi juzi huyajui ya mjini!!
 
Back
Top Bottom