Ni kweli Mkapa alianzisha TRA?

Usimwamini sana Mchonga
 
Mkuu wataalam wanaanzisha vitu lakini credit huwa zinaenda kwa viongozi wa kisiasa; ukihangaika na hayo mambo utapata kiharusi bure tukukose.
 
Kati ya masharti tuliyopewa na benki ya Dunia na ndugu yake wa karibu ni uanzishwaji wa taasisi huru ya ukusanyaji mapato inayojitegemea.

Hii ilikuwa ndani ya package ya ubinafsishaji. Sijajua sababu kamili ya kusema Mzee Mkapa ndiye aliyeanzisha TRA lakini imeanza kazi kipindi chake cha uongozi.

Anahitaji pongezi kwa hilo.
 

Kuteua bodi na viongozi ni kazi rahisi kuliko kutengeneza taasisi kisheria.
Sheria ndo inaweka mifumo yote ya tasisi iweje.

Unapoteua hizo bodi, unakuwa unatekeleza tu hiyo sheria.

Kwa mfano leo hii Magufuli akivunja bodi ya TRA na kuiunda upya, haitamaanisha kuwa JPM katengenza TRA nyingine, unless otherwise apeleke muswada bungeni aifumue hiyo mifumo ya TRA aunde nyingine tofauti kabisa
 
Wote Mkapa na Kikwete hawasemi ukweli ulio kamili. Nitaeleza chimbuko la TRA na mchango wa kila mmoja katika nafasi aliyokuwa nayo wakati huo.

TRA ilitokana na makosa aliyofanya Profesa Kighoma malima wakati akiwa waziri wa fedha, na kikwete akiwa Naibu waziri wa fedha; Malima alikuwa akitoa misamaha mingi ya kodi, na vile vile akasemekana kuwa ana account maalumu ya Waziri wa Fedha huko London. Wakati huo Tanzania ilikuwa inapokea mikopo mingi sana kutoka IMF na World Bank. Mwaka 1993 World bank ikasitisha kutoa mikopo hadi kuhakikisha kuwa Tanzania inasimamia kodi zake vizuri na vile vile inatumia fedha za mikopo na misaada vizuri; mojawapo ya masharti yalikuwa ni kumwondoa Malima kutoka Wizara ya fedha, na vile vile kufanya kazi ya ukusanyaji kodi isiingiliewe na wanasiasa, bali kuwepo na chombo huru cha kukusanya mapato ya serikali.

Hatua ya kwanza katika kutekeleza masharti hayo ilikuwa ni Mwinyi kumfukuza kazi Profesa malima, ndipo Kikwete akapanda kuwa waziri wa fedha, nadhani mwishoni mwa mwaka 1993 au mwanzoni mwa mwaka 1994. Through process hiyo, ile account ya Waziri wa fedha iliyokuwa London ambayo ilikuwa na signatory mmoja tu (Prof malima) nayo ikawa frozen. Inasemekana sababu kubwa ya ya kifo cha profesa ilikuwa ni ule mshituko alipokwenda London na kukuta hana pesa; wakati huo hakukuwa na mtandao kama leo.

Hatua ya pili ilikuwa ni kuundwa kwa Taasisi ya kukusanya pesa na vile vile kujenga utaratibu wa kukusanya kodi kwa mfumo wa computer. World Bank ilileta wataalamu katika kusaidia uundwaji wa TRA na vile vile kufundisha maafisa wa kodi namna ya kukusanya kodi kwa njia ya Computer. Hayo yalianza mwishoni mwa mwaka 1994 na muundo wa TRA ukakamilika mwishoni mwa mwaka 1995. Baada ya maandalizi ilipofika mwishoni mwaka huo wa 1995 au mwanzoni mwa 1996 ndipo TRA ikazinduliwa.

Kwa hiyo muasisi mkubwa wa TRA siyo kikwete wala Mkapa bali ni World Bank. Kikwete alikuwapo kama waziri wa fedha mwaka 1994-95 wakati wa mchakato wa TRA unaendelea; halafu Mkapa aliizundua TRA akiwa rais mwishoni mwa mwaka 1995 au mwazoni mwa 1996.
 

Worldbank ilishauri, ila wataalamu wa Mzee ruksa wakachukua ushauri wakatengeneza mifumo ya TRA, wakapeleka muswada bungeni, muswada ukapita na ukasainiwa na Mzee ruksa kuwa sheria mwaka 1995.

TRA ikaanza kufanya kazi rasmi, July mwaka 1996.

Kwa hiyo sidhani kama ni haki kumnyima rais aliyekuwepo madarakani mwezi August mwaka 1995 credit ya uanzishwaji chombo hicho wakati yeye ndo alitia saini sheria ya kuanzisha chombo hicho. Haijalishi wazo lilianzia wapi
 
Sijelewa unachoongea au kupinga kwenye post yangu hiyo; elewa kuwa bila kuwapo kwa TRA World bank ilikuwa imekataa kutoa pesa kabisa. Viongozi wetu walishiriki katika unanzishwaji wa TRA lakini hilo ilikuwa ni brainchild ya World bank. Hakuna kiongozi anayeweza kusimama na kusema kuwa ndiye mwanzilishiwa TRA, wote walikuwa ni watekelezaji wa maagizo ya world bank.
 
Sawa mkuu. Mimi naamini tunazungumza jambo moja tu kwa namna tofauti. Hakukuwepo TRA kipindi cha Mwinyi (ilikuwepo sheria tu). Kama mlipa kodi, usingeweza kumshataki Commissioner General wala TRA mwaka 1995, maana hakuwepo/haikuwepo pamoja na kuwa sheria ilikuwepo tayari. Chombo (TRA) kiliundwa (kilianza kuwepo) mwaka 1996.

Yes, Mzee Ruksa amechangia, lakini na BWM alichangia pia. Wote wanapata sifa.

Mkuu, Kichuguu ameweka pespective nyingine. Asante sana. Sio mjadala mbaya huku tukimsindikiza BWM.
 
Kwani hapo nyuma kodi ilikuwa inakusanywa vp tufahamu jamani
 
Hata wewe huelewi vizuri, juna uhakika, kwa hiyo kubali yaishe
Labda tum tag Kikwete.
Lqkini sheria ya TRA ilitungwa na kupitishwa lini?

Je mamlaka huru ya kukusanya mapato ilianzishwa lini?
 
Hata wewe huelewi vizuri, juna uhakika, kwa hiyo kubali yaishe
Labda tum tag Kikwete.
Lqkini sheria ya TRA ilitungwa na kupitishwa lini?

Je mamlaka huru ya kukusanya mapato ilianzishwa lini?
Kabla ya TRA establishment kodi ilikuwa inakusanywa kwa mfumo upi labda
 
Kwani hapo nyuma kodi ilikuwa inakusanywa vp tufahamu jamani
Zilikuwepo departments chini ya wizara ya fedha. TRA ni Mamlaka inayojitegemea kiutendaji (nje ya wizara) na pia ni corporate body (inaweza kushtaki na pia kushtakiwa kwa jina lake).
 
Zilikuwepo departments chini ya wizara ya fedha. TRA ni Mamlaka inayojitegemea kiutendaji (nje ya wizara) na pia ni corporate body (inaweza kushtaki na pia kushtakiwa kwa jina lake).
Ina maana kuna baadhi ya mambo ambayo TRA imeboresha lakini mengine imechemka katika ukusanyaji ukilinganisha na hapo zamani sivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…