Wote Mkapa na Kikwete hawasemi ukweli ulio kamili. Nitaeleza chimbuko la TRA na mchango wa kila mmoja katika nafasi aliyokuwa nayo wakati huo.
TRA ilitokana na makosa aliyofanya Profesa Kighoma malima wakati akiwa waziri wa fedha, na kikwete akiwa Naibu waziri wa fedha; Malima alikuwa akitoa misamaha mingi ya kodi, na vile vile akasemekana kuwa ana account maalumu ya Waziri wa Fedha huko London. Wakati huo Tanzania ilikuwa inapokea mikopo mingi sana kutoka IMF na World Bank. Mwaka 1993 World bank ikasitisha kutoa mikopo hadi kuhakikisha kuwa Tanzania inasimamia kodi zake vizuri na vile vile inatumia fedha za mikopo na misaada vizuri; mojawapo ya masharti yalikuwa ni kumwondoa Malima kutoka Wizara ya fedha, na vile vile kufanya kazi ya ukusanyaji kodi isiingiliewe na wanasiasa, bali kuwepo na chombo huru cha kukusanya mapato ya serikali.
Hatua ya kwanza katika kutekeleza masharti hayo ilikuwa ni Mwinyi kumfukuza kazi Profesa malima, ndipo Kikwete akapanda kuwa waziri wa fedha, nadhani mwishoni mwa mwaka 1993 au mwanzoni mwa mwaka 1994. Through process hiyo, ile account ya Waziri wa fedha iliyokuwa London ambayo ilikuwa na signatory mmoja tu (Prof malima) nayo ikawa frozen. Inasemekana sababu kubwa ya ya kifo cha profesa ilikuwa ni ule mshituko alipokwenda London na kukuta hana pesa; wakati huo hakukuwa na mtandao kama leo.
Hatua ya pili ilikuwa ni kuundwa kwa Taasisi ya kukusanya pesa na vile vile kujenga utaratibu wa kukusanya kodi kwa mfumo wa computer. World Bank ilileta wataalamu katika kusaidia uundwaji wa TRA na vile vile kufundisha maafisa wa kodi namna ya kukusanya kodi kwa njia ya Computer. Hayo yalianza mwishoni mwa mwaka 1994 na muundo wa TRA ukakamilika mwishoni mwa mwaka 1995. Baada ya maandalizi ilipofika mwishoni mwaka huo wa 1995 au mwanzoni mwa 1996 ndipo TRA ikazinduliwa.
Kwa hiyo muasisi mkubwa wa TRA siyo kikwete wala Mkapa bali ni World Bank. Kikwete alikuwapo kama waziri wa fedha mwaka 1994-95 wakati wa mchakato wa TRA unaendelea; halafu Mkapa aliizundua TRA akiwa rais mwishoni mwa mwaka 1995 au mwazoni mwa 1996.