Ni kweli Mkapa alianzisha TRA?

Hapa kuna hisia za kidini zimejificha kwenye accusations and counteraccusations, I am sure.
Sidhani. Wengi ninaowaona hapa, tunafahamiana muda mrefu tu hapa JF, najua ni watu objective sana. Sioni kama kuna hoja ya udini hasa.

Afterall, tunazungumzia wanasiasa tu....
 
Sasa je kuna maboresho yoyote yenye tija ambayo TRA toka kuanzishwa kwake imeyatekeleza au ni bora awali
Kitendo cha kutokuwa chini ya..
Basi ina maana iko huru kimaamuzi

Kama vile watu tunalilia tume huru ambayo haiamuriwi na ...
 
Wakulungwa;

Mchakato wa kuanzishwa kwa TRA ulianza way back 1985 pale dunia ilipopeleka shinikizo kwa Serikali za nchi zote wanachama wa UNO kubadili mfumo wa uendeshaji biashara na kujikita katika ukusanyaji wa kodi;

Aidha shinikizo hili lilikua limeambatanishwa pia na Uanzishwaji wa Vyama vingi ikiwa ni namna ya kudhibiti;

1. Serikali zilizopo madarakani na
2. Utambulishwaji wa mfumo mpya wa Demokrasia

Kama itakumbukwa vizuri kwa wale wahenga ndipo vifo vingi vya makampuni ya kimataifa hasa ya Mafuta Kama SHELL, TOTAL, AGIP, BP GAPCO yalipoanza taratibu kufungasha virago na aidha kwa kuyabinafsisha au kuyafunga.

Vile vile Ndio hasa kifo cha shirika la mafuta TIPA na TPDC mwaka 1999 ikiwa ni zao la sera shinikizo za Dunia ya mwaka 1985.

Pia ikumbukwe kwamba wimbi hili la mabadiliko ndilo lililoingia na ile sera ya Ubinafsishaji ambayo Rais wa awamu ya Pili Mzee Mwinyi alianza mchakato na Marehemu Rais wa awamu ya Tatu kuja kugongelea msumari wa mwisho kwenye jeneza kwa kubinafsisha mashirika, mashamba na viwanda vilivyokua vikimilikiwa na Serikali.

Kwa muktadha huo hakuna mwenye kuweza ku claim kuwa master mind wa kuanzishwa kwa TRA wala Mwenye balls za ku claim kuinforce mfumo wa vyama vingi Tanzania.

NB
Jaribu kutafakari kati ya 1985 - 2005 jinsi mifumo ya uendeshaji Tanzania ulivyokua na viraka huku wale wajanja wakipenya na kukwara keki ya Taifa.
 
Shukran sana Mkuu..
 
Uko sawa kabisa. Kodi Nchini zilikuwa zinakusanywa hata wakati wa Mwalimu labda waseme tu walibadili jina na kuwa TRA. Sijui aliyebadili jina ni nani.
Ndo MKAPA
 
Sio TRA peke yake kafanya mengi sana ukiwemo dira ya 2020 kuingia uchumi wa kati ni akili yake
 
Marehemu anasingiziwa mambo mengi sana
 
Ingia kwenye website ya TRA utaona ilianza lini, kwa kurahisisha ni kuwa TRA ilianzishwa mwaka 1996 , na mwaka uliofuata yaani 1997 ikatungwa sheria ya VAT ambayo ilianza kutumika tarehe 1.7.1998
 
Ingia kwenye website ya TRA utaona ilianza lini, kwa kurahisisha ni kuwa TRA ilianzishwa mwaka 1996 , na mwaka uliofuata yaani 1997 ikatungwa sheria ya VAT ambayo ilianza kutumika tarehe 1.7.1998


Wewe TRA imeanzishwa august 1995..
Website gani hiyo uliyopita wewe?
 
Ni vizuri kukawepo na ukweli zinapoandikwa historia za Viongozi wetu na historia ya nchi yetu Kwa ujumla.
...
Sasa hili la Mkapa kuunda TRA pia linanitatiza sana ..kivipi?
...
Swali linabaki pale pale je Mkapa ndo aliunda TRA?

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 11 ya 1995, na kuanza shughuli zake tarehe 1 Julai 1996.
Mikopo Chefuchefu; demulikuy; Barbarosa; Kataskopos
 
Sasa je kuna maboresho yoyote yenye tija ambayo TRA toka kuanzishwa kwake imeyatekeleza au ni bora awali
Kuna mambo mengi sana yameboreshwa. Makusanyo ya kodi yameongezeka sana tena sana.
 
Prof Saimon Mbilinyi alipokuwa waziri wa Fedha ndiyo aliongoza mageuzi na kuunda TRA. Nakumbuka siku moja alielezea huo mchakato, Mzee yule alikuwa mbobezi wa maswala ya uchumi lakini alipigwa vita sana kundi la wanamtandao wa akina JK na Lowassa wakahakikisha ametolewa kwenye uwaziri maana alikua tishio kwa mtandao na pia alikuwa mtu wa karibu na Mkapa na hata Hassy Kitine alipigwa vita mpaka akachomolewa, Mwandosya nae alikua target ya wanamtandao na walichomfanya hatahau ktk maisha yake. Bhatai mbaya wanamtandao wakavulugana kwenye kugombania madaraka na matokeo yake kila mtu aliona kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 na mapaka sasa mabaki ya matandao yanaendea kuvukuga chama.
 
Nakumbuka kabla ya Mkapa kuwa rais wa awamu ya 3 huko mtaani raia walikuwa wakikimbizana na mgambo wenye marungu wanaofatilia raia wasiolipa kodi ya maendeleo /kichwa.

Baada ya kuwa rais Mkapa alifanya marekebisho makubwa kuhusu ukusanyaji wa kodi ambapo mgambo walikosa kazi za kuwakimbiza wasiolipa kodi hivyo kila raia alilipa kodi ktk bidhaa aliyonunua yaani pesa ilikatwa huko huko wala hapa kuwepo na sababu tena ya kukimbizwa na mgambo yaani mpaka leo tunakwatwa kodi ktk bidhaa tunazonunua kila siku.

Nimekumbuka hili jambo lilifanywa na Mkapa
 


Ungesoma thread yote kabla ya kuchangia usingeandika upupu huu..

Tra mchakato ulianza zamani ukakamilika august 1995..mbilinyi alikuwa waziri kipindi hiki?
 
Ungesoma thread yote kabla ya kuchangia usingeandika upupu huu..

Tra mchakato ulianza zamani ukakamilika august 1995..mbilinyi alikuwa waziri kipindi hiki?
Aksante nashukuru sana Ndugu yangu kumbe nimeandika upupu! Ungenisaidia tu kwa kunieleza ningeelewa lakini kuniambia nimeandika upupu dah kuna watu mna maneno ya kukwaza sana.
 
Wewe ulokua unalialia uanzishwaji wa TRA umesikia mambo aliyoanzisha na kufanya Mzee Mkapa kwenye hotuba ya Mh.Rais?
 
Aliibadili jina na mfumo na kuiboresha hili halilingik... ila ikiwa aliianzisha kweli basi inamaanisha hakukuwepo ulipaji kodi ya mapato wala leseni za biashara!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…