Ni kweli mtu akichezea kichapo cha kutosha ukimpa maji anaweza kufariki?

James_patrick_

Senior Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
102
Reaction score
194
Habari ndugu zangu,

Naomba kuuliza,hivi ni kweli mtu akichezea kichapo cha kutosha ukimpa maji anaweza kufariki? Na je, kama ni kweli ni kitu gan upelekea hali hiyo.
 
Una tango nn mpaka unataka kuuwa manz
 
Jibu ni ndio kwa asilimia 50. Kwanza kabisa, kuchezea kichapo kikali,huathiri ubongo. Ubongo ukivurugika,pia moyo hupata mshituko. Ila ungesema maji baridi. Kuna jama wazuri kwa kutesa watu hasa kama bado wanachunguzwa kwa makosa furani. Hawa,ukiomba maji ya kunywa,utapewa vinywaji vingine na si maji. Sema tu hata mi kitu ambacho sijajua, maji yameundwa na nini cha kuathiri mtu mwenye hali ya mshtuko wa moyo?!!
 
Kwa mimi ninavyoelewa kidogo, mtu akitoka kufanya mazoezi mfano kukimbia au gym halafu muda huohuo anywe maji hasa ya baridi uwezekano wa kudondoka au kuzirai ni mkubwa kwa sababu ya mapigo ya moyo kwenda kasi (mwili umechemka) halafu ghafla uupe maji ya baridi lazima utaharibu... so it depends pia na aina ya kipigo/kichapo

ni sawa na REJETA IMECHEMKA HALAFU PAAP UIFUNGUE UWEKE MAJI GHAFLA...MMMH

wenye uelewa zaidi wataongezea
 
Upo vizuri...unajua vingi zaidi ya ulivyoandika hapa.
 
Habari ndugu zangu,

Naomba kuuliza,hivi ni kweli mtu akichezea kichapo cha kutosha ukimpa maji anaweza kufariki? Na je, kama ni kweli ni kitu gan upelekea hali hiyo.
Si kichapo tu, hata mtu akiwa amejeruhiwa kwa ajali ya gari au kingine, akiomba maji usimpe. Atakufa. Kiu ya ghafla inayohusiana na mtu kuumia ghafla inasababisha mwili uingie kwenye relaxation mode, ambayo inaua mtu. Mwili unatakiwa kuwa katika agitated mode wakati umeumia sana. Ni sawa na mtu alieumia anasikia usingizi, usimwache alale mwili uka relax, atakufa. Ndio maana utasikia kwenye movie wakisema "stay with me, stay with me, keep awake, open your eyes" na unatakiwa uwe unamsemesha
 
Hapa nimeelewa .
 
Habari ndugu zangu,

Naomba kuuliza,hivi ni kweli mtu akichezea kichapo cha kutosha ukimpa maji anaweza kufariki? Na je, kama ni kweli ni kitu gan upelekea hali hiyo.
Hata akipata ajali ya bodaboda usimpe maji ya kunywa muda huo, hii ni kutokana kama amejeruhiwa ndani ya utumbo atatoka damu kwa wingi kwani kitu cha baridi huyeyusha damu.
 
Kwamba mwili usiruhusiwe kuwa ktk quite mode😇🤗
 
Mbona wachezaji wa AFCON hawakuanguka wakati wa COOLING BREAK?
 
Mbona wachezaji mpira wanakunywa maji baridi wanapokuwa wanaendelea kucheza uwanjani?
 
Kumbe uwa wana maana hii, ndo naelewa leo
 
Mbona wachezaji mpira wanakunywa maji baridi wanapokuwa wanaendelea kucheza uwanjani?
Mkuu,
Kwanza kabisa,kama utafatilia,wale jama wanafatiliwa kwa karibu na madaktali professionals. Hivyo,maji wanakunywa ndio,lakini angalia kwa makini,utaona kiasi wanachokunywa. Wanapooza koo tu si kwa ajili ya kupooza mwili. Si kwamba hawataki,bali wanakuwa na kipimo hawatakiwi kuzidisha. Maana wengi wao kama husukutua mudomo na kuyatema.
Kingine, si maji tuuu. Kuna vimiminika vingi hupewa. Kama unafatilia,kuna tuchupa tudogo kama twa visungura. Yale sidhani kama ni maji tuloyazoea.
Na mwisho kabisa, kumbuka tukio la wachezaji kuchemka mwili,ni kitu wanachokuwa wamekiandaa,hakistui mfumo wa mwili. Hapa kilichoongelewa ni mfano kama wa mwizi,kibaka, na watu wengine wanaokamatwa na watu wasiojulikana.
Kwanza jiulize. Kwa nini mtu akipigwa na kuachwa mahututi,akilala nje,anakata upepo. Huo ni ubaridi tu,wala si maji. Na akiwa mzima,anakesha. Kwa nini mtu akipata ajali na kukosa msaada kwenye ubaridi hachomoki.
 
Habari ndugu zangu,

Naomba kuuliza,hivi ni kweli mtu akichezea kichapo cha kutosha ukimpa maji anaweza kufariki? Na je, kama ni kweli ni kitu gan upelekea hali hiyo.
Msingi wa hili uko kwenye mfumo wa kumeza kimiminika au chakula kuelekea tumboni.

Kuna utaratibu unaoratibiwa na ubongo wakati wa kumeza unaitwa "GAG REFLEX".
Huu ni utaratibu ambao huelekeza chakula kwenye njia yake badala ya njia ya hewa. Hali hii huanzishwa AUTOMATIC chini ya usimamizi wa UBONGO.

Unapokuwa unaumwa sana au kupata ajali au mshituko mkubwa kuna wakati hali hii hupotea (ubongo hushindwa kuratibu kitendo hiki). Hivyo, ukimpa mtu maji au chakula kuna hatari ya kwenda kwenye MFUMO WA HEWA (CHOKING/ASPIRATION).

Kwa kuwa mtu huyu anakuwa hawezi kukohoa vyema au kuongea, maji yale au chakula kinaenda kuzuia mfumo wa upelekaji hewa kwenye damu kupitia MAPAFU. Oksijeni hupungua na mwisho mgonjwa kupoteza maisha au madhira mengine zaidi, mfano:upumuaji usiofaa na maambukizi kuanza kwenye mapafu iwapo atafanikiwa kutokupoteza maisha.

NB: Hapa ndo umakini unahitajika unapowalisha: WAGONJWA, WATOTO, WAZEE SANA, MTU ALIYEKUNYWA POMBE( AU DAWA) NA HAJITAMBUI VYEMA.
 
Unafahamu kazi ya esophagus?
 
Kitaalam Zaidi
Sio wale WA sijui relaxation,Mara cooling
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…