Ni kweli Papa Wemba kauawa na sumu iliyowekwa kwenye Mic?

Ni hisia tu zisizo na mashiko....huyo jamaa kama ni fundi wa sound sioni kuna ajabu gani akawa anahangaika na mic zake....

Kuitoa mic baada ya Papaa kuanguka ni labda kuona tu inahitajika nafasi eneo lile......

Isitoshe tumeshaambiwa Papaa alitoka kuumwa muda si mrefu, so sioni kwa nini kunazuka sintofahamu.
 
Fundi wa mic ananyata???we huoni akinyata??hata hiyo picha huoni akirudisha mic kwa kunyata???
Huoni anavyoweka mic kwa mashaka??
 
Fundi wa mic ananyata???we huoni akinyata??hata hiyo picha huoni akirudisha mic kwa kunyata???
Huoni anavyoweka mic kwa mashaka??
Hiyo video ipo kwa slow motion kaka....

Na kama umeshahudhuria shughuli mbalimbali utaona huwa wanatembea tu kwa tahadhari kwamba wasisumbue waliopo stejini...nimeshaona hivyo sehemu nyingi tu...

Mwaka jana nilikuwa Zanzibar kwenye tamasha la filamu nilishtuka kuona mtu anatoka nyuma ya steji kwa kuunyata mpaka nilipomuona ameenda ku adjust urefu wa mic pale stejini.
 
Nadhani hii habari wanaikuza Sana ukweli ni Heart failure ndo kilichomuondoa na si kuuliwa.
Papa Wemba alikuwa mgonjwa na Dr.wake ali suggest apumzike lakini alipuuza. Ifike mahali tuangalie mambo mengine kiupana zaidi tuache kuendeshwa na hisia.
 
Mkuu unaonekana unajua sana mambo ya wanamuziki waki kongo,hivi yule Gibson wa Koffi yupo wapi siku hizi?
 
Kwanza gentamycine hongera zako umeeleza kwa kina unachokijua na uhalisia wa jambo na pana watu wengi wameyaelewa maelezo yako.
Kuhusu hili la kunyata limenikumbusha miaka ya nyuma refarii akiongea na wachezaji wa timu pinzani kisha I katokea timu nyingine kufungwa utasikia wachezaji na mashabiki wao wakisema refa alikuwa anaongea nao kabisa.So kimsingi kama watu wabaya wangekuwa na nafasi nyingi za kumuua nasi pale uwanjani kwa Sumu ambayo hata mletaji ingeanza kumuondoa yeye au alikuwa na patriot?maana sadamu husein alikuwa akitupa scud marekani wanatuma patriot kuizuia.
 
Mkuu unaonekana unajua sana mambo ya wanamuziki waki kongo,hivi yule Gibson wa Koffi yupo wapi siku hizi?

Aliachana na Koffi Olomide na kuwa katika mpango wa kuanzisha Bendi yake na bado hajafanikiwa kihivyo na sasa inasemekana anataka kujiunga na Mwimbaji mwenzie aitwae Solei Wanga ambaye anafanya vizuri kiasi. Tatizo la Wanamuziki wa DR Congo wanadhani kila Mtu tu anaweza kuanzisha Bendi yake kwakuwa tu wameshakuwa na majina huku Wakisahau kuwa hao wanaowaiga akina Koffi, JB na Werrason wameingia MAAGANO makali sana ya KISHIRIKINA ambayo nisingependa kuyaweka hapa HADHARANI kwani mnaweza MKAOGOPA na hata KUWACHUKIA. Hata hivyo hao Wanamuziki wote wakishindwa huko waendapo hurudi kwa hawa Wakubwa zao waliowakuza. Kwa mfano Mwanamuziki mwingine wa Bendi hiyo hiyo ya Quarter Latin ya Koffi Olomide aitwae Shela Mputu aliondoka kwa Koffi kwa NYODO sana ila sasa anampigia magoti Koffi arudi kundini ila Koffi kampotezea.
 
Na allan mpela(afande imeishia vp na jb kuna wakati nilisikia alitaka kurudi bcbg?
 
Na allan mpela(afande imeishia vp na jb kuna wakati nilisikia alitaka kurudi bcbg?

Alain Mpela " Afande " ni kweli anataka kurudi BCBG na alikuwa ni kipenzi mkubwa sana wa JB Mpiana na hata katika nyimbo zote za rhumba ( za taratibu ) za Wenge Musica BCBG kama OMBA na JEANNETE JB Mpiana humuimba mno Alain Mpela huku akitaka hata kulia kwani alimpenda sana na alimkuza mwenyewe. Kikwazo kikubwa sasa cha Alain Mpela kurudi kundini ni kwakuwa tayari nafasi yake imezibwa vizuri mno na Mwanamuziki Bishoo na fundi wa kuchezea sauti aitwae Jean Didier Loko JDL a.k.a Tramendou lakini kama pia haitoshi Alain Mpela wakati akitoka BCBG alikuwa ndiyo Kiongozi wa Wanamuziki wa Bendi ( Directoreire de artiste ) nafasi ambayo sasa JB Mpiana kampa Mwanamuzi Mkongwe na ambaye ndiyo anatunga nyimbo karibia 85% za Wenge Musica BCBG na pia anapanga mashairi na anatengeneza mistari yote ya nyimbo aitwae Jules Kibens a.k.a Le Professeur a.k.a Molongeshi hivyo JB Mpiana anaogopa kumrudisha Alain Mpela Afande asije akaleta chuki za kimadaraka kundini. Kwa faida yako / yenu huyu Mwanamuziki Jules Kibens ni Mwalimu cha Lugha wa Chuo Kikuu cha Kinshasa na ni mtaalam sana wa lugha ya Kifaransa na kile Kifaransa sanifu unachokisia kikiimbwa katika nyimbo nyingi za Wenge Musica BCBG kimetengenezwa na Jules Kibens.
 
Nashukuru kwa kunijuza kuhusu Gibson wa Koffi,na Soleil Wanga namfahamu ni yule mrefu mweusi naye huwa anaimba ana kasauti fulani hivi,na kuna wakati alibleach ndevu zake,lakini mkuu mbona umezungumzia wanamuziki vijana kushindwa kutusua kama walivyotusua kina Ngiama Makanda na JB itakua vigumu kwao ,lakini umewasahau watu kama Fally na Ferre Gola mbona wao wametokea hapo hapo kwa kina Koffi na wapo juu hasa Fally kwa mtazamo wangu namuona yupo juu sana,hawa je? na wao wana maagano?.
 
Waswahili banah! Kila kifo lazima atafutwe mchawi. Ndio maana wabibi wanateketea huko Shinyanga na Mwanza kwa sababu za kipumbavu kama huu uvumi unaosambaa kuhusu kifo cha Papa Wemba.
 
Mkuu uko deep, big up!
 
Mkuu gentamycine embu tuambie bana uchaw wa hao jamaa wengine please ama PM mkuu nami nawafatilia ila upande huo sjawah kupagusa ila nlisikaga tena majuz tu juu ya uchaw wa koffi olomide ingawa sjaamini mkuu..
 
nimekuelewa Fulani ivi kama ingekuwa we ni wakili wa mtuhumiwa ni dhahir umeshinda kesi mkuu
 


mmh! wewe ni mtangazaji wa radio one bisha usibishe tena yule baba wa hawavumi lakini wamo. time will tell
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…