Ni kweli Papa Wemba kauawa na sumu iliyowekwa kwenye Mic?

Watu wanajiuliza, siku Ile ambapo show ilisimama Na kila mtu alikua busy kujaribu kumsaidia Papaa, hafu Ni yeye peke yake alikua anajishughurisha Na Mic! Mbona hakuondoa Na Mic zingine?
 
Kama Ni kweli uzembe wake utaonekana akikamatwa, coz hata video haionyeshi sura yake vizuri!
Mkuu ni hivi; kwenye show za wezetu huwa kuna watu wanakuwa kwenye steji kama wasaidizi na walinzi pia marafiki wa karibu. Piga ua kama hawakufahamu huwezi kuwa upande huo. Angalia show za Werra na JB Mpiana hadi kuna wanawake special wanakuwa wako huko pasipo kazi maalumu. Hicho ni kifo tu cha kawaida wala sifikirii chochote kuhusu huyo kijana (msaidizi).
NB: Hakuna mziki ninaofuatilia na historia za wanamziki kama wa DRC na sifahamu wimbo wowote wa Tz labda OTTU JAZZ BAND tena yakina Moshi William
 
Tatizo lako ndio hilo gentamycine nadhani sijawahi na sitegemei kumsanifu mtu humu ndani khabari hizo nilizisikia lakini kwa uelewa wako na namna unavyowazungumzia watu hao ni dhahiri ningepata majibu murua katika swali langu.So hilo la unafiki sina na niliheshimu uelewa wako ndo maana nikauliza ila tusifike mbali zaidi ya hapa naujali na kuuthamini sana uelewa wako so kama unadhani kuna unafiki hapo shaka ondoa mwisho nashkuru kwa majibu yako tuendelee kuijenga jf dhana si jambo jema.
 
hawezekeni mwanaume mzima baada ya papa wemba kuanguka eti yeye anaikimbilia Mic na kuitoa jukwaani.
kuna namna hapo.
 
Ambaye anaitwa Seguen Mignon Maniata. Bado sijaona DR Congo nzima mpiga drums wa kumzidi au kushindana na huyu Seguen Mignon Maniata.
Ni kweli huyu jama wa bcbg anapiga drums vizuri lakini kiukweli hebu weka mapenzi ya bcbg pembeni ,mi naona yule jamaa Estatica ndo kiboko yao kwa drums kwa wapiga drum wakikongo kwa mfano wimbo maarufu wa Fally wa Bakandja,hebu cheki jamaa alivyozikunguta mle.
 
Papa Wemba? Ndiye nani mbona simjui? Kuna single yoyote kapiga na Ally Kiba au Sugu?
Na alikua anaishi wapi hapa Dar?
 
Mkuu mimi ni mpenzi sana wa Hao wana mziki wa Congo wote uliowataja hapo juu, tafadhali naomba utuaimulie wayafanyayo ili tufanye maamuzi mapema wengine hapa.
 

Mkuu kwa wanaujua muziki wa DR Congo ukisema Champion Estatica anamzidi Seguen Mignon Maniata wanaweza hata wakakutupa tu Mto Ruaha ukaliwe na Mamba kwa kuwaudhi. Watu pekee ambao ndiyo wanamtia tumbo joto au wanakaribiana kiuwezo na Seguen Mignon Maniata mpiga drums maarufu wa Bendi ya Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana ni hawa wawili tu :
  1. Papii Kakol mpiga drums hatari wa Werrason na Bendi yake ya Wenge Musica Maison Mere.
  2. Ramatoulaye Diabate mpiga drums hatari wa Bendi ya Extra Musica chini yake Roga Roga kama Rais wa Bendi.
NB: Ukiachia hao wawili niliokutajia hapo waliobaki wote wanajifunza kila siku kupiga na kukaanga chips ( drums ) kwa FUNDI na MTAALAM mwenye mapigo yake Seguen Mignon Maniata.
 
Mkuu mimi ni mpenzi sana wa Hao wana mziki wa Congo wote uliowataja hapo juu, tafadhali naomba utuaimulie wayafanyayo ili tufanye maamuzi mapema wengine hapa.

Mbona tayari nimeshaweka kila kitu chao hadharani Mkuu? Angalia posts zangu kuanzia page ya 5 nimeweka aina yao ya uchawi wanaoutumia. Ipitie ili upate maarifa zaidi.
 
Mbona tayari nimeshaweka kila kitu chao hadharani Mkuu? Angalia posts zangu kuanzia page ya 5 nimeweka aina yao ya uchawi wanaoutumia. Ipitie ili upate maarifa zaidi.

Popoma katika ubora wako
Shikamoo mzee
 
Popoma katika ubora wako
Shikamoo mzee

POPOMA Shangazi yako. Marahaba! Tukutane whatsapp Kijana mbona hujaonekana tokea leo asubuhi hadi sasa? Kulikoni? Kardinali Evan anakuulizia.
 
Naona kuna haja ya kuanzisha jukwaa la wakongomani
 
Mkuu cku tena kwann isiwe leo utupe iyo story
 

Yanawenawezekana unayosema, ila mtu anaweza ku take advantage ya maneno ya daktari. Ni wengi wenye kujitabiria vifo kwa namna moja ama nyingine. ndugu yangu aliwahi kununua mikeka mitatu kwa siku moja, mumewe akamshangaa ni ya nini yote hiyo, akasema tunaweza kupata shughuli wageni wakakosa pa kukaa. mume akahoji wageni gani wa kujaza viti mpaka kwenye mikeka, mke akajibu huwezi jua. wiki hakupita mnunua mikeka akaumwa ghafla na kupoteza uhai, mikeka aliyonunua ikapata shughuli.
watu husema tu bila kujua wasemacho lakini mwisho wa siku ni kama umejitabiria. tunabaki kusema ndio maana ilikua hivi na vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…