Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,263
- 18,201
Something is not right.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana mkuu! Silazishi ukubaliane Na Mimi, nlikua nataka tujadiri kile tunachoona kwenye video, kwa mfano kwa uelewa wako WA Muziki WA Kongo, nilitegemea ungechangia hivi (baada ya kutazama video)....May be Swala la kutolewa Mic Na stand yake Na kuletwa nyingine Ni kawaida, hata Mic Na stand yake ilipotolewa baada ya Papaa kuanguka Ni kawaida, coz Papaa Ana Mic zake Special Na Ni za gharama kubwa, so ilijulikana hangeweza kuendelea tena Na show ndo maana Mic yake ikatolewa Ili ikahifadhiwe! Mfano hapo juu ndo nilitamani kusikia, yani maoni yako baada ya kutizama video!......na sio kukulazimisha ukubaliane Na Mimi.Siwezi kuzungumzia tukio tu unalolilazimisha Wewe katika hiyo video bali nazungumzia uzoefu wangu generally kwa hawa Wanamuziki wa DR Congo ambao nina uhakika nao tena hata usio na mashaka ila kwakuwa unataka uridhike na uwe na amani basi ngoja nami niungane na Wewe kuwa PAPA WEMBA amewekewa SUMU au KAUWAWA!
Yes! Mkuu wewe umeitizama video, i agree with you!Maelezo mazuri ingawa unaweza kuwa unapotosha...Ukiiangalia vizuri ile video yule mtoa mike alionekana kabisa ananyatia, the guy seemed not an official assistant of PAPAA WEMBA, he was the asshole bitch with coward action!!
Mkuu Wanamuziki wa DR Congo hata tu ukifa kwa KIPINDUPINDU kwa uchafu wako mwenyewe watasema UMEULIWA. Franco tu ambaye kila Mtu anajua kuwa alifariki kwa kuugua SIDA ( UKIMWI ) Wakongo wanakuambia aliwekewa SUMU na Hayati Mobutu aliyekuwa Rais wa Zaire enzi hizo wakisema walitofautiana Kisiasa. Kama hiyo KIFO cha Tabu Ley ambaye hakuna asiyejua kuwa aliuguwa mno saratani lakini alipokufa tu Wakongo wanakuambia KAUWAWA na yote tisa kumi mwaka jana mwanamuziki wa Bendi namba mbili au ya Kikosi cha pili cha Wenge BCBC kiitwacho PPU aitwae Tatty Nkusa ambaye ndiyo alikuwa ameshapandishwa Kikosi cha kwanza alipata AJALI ya kugongwa na gari alipokuwa anaendesha pikipiki yake akitokea katika kumbi za starehe lakini hao hao Wakongo wanakuambia KAUWAWA.
Labda nikusaidie tu kukuambia kuwa hakuna Watu wajanja na wanaoenda na FURSA kama Wanamuziki wa Congo na kwa taarifa yako tu hao hao unaowasikia wanasema PAPA WEMBA kauliwa watatumia Msiba huu KUJINEEMESHA kimaslahi huku wengine wakiandaa sasa MATAMASHA ya Kumbukumbu ya KIFO cha PAPA WEMBA sehemu mbalimbali ili wapige HELA na huko watakapokuwa wanaenda watakuwa wanawaseti Watu wazidishe UVUMI kuwa jamaa kauwawa na propaganda zao zingine nyingi nyingi ili mradi tu wajaze nyomi ukumbini au uwanjani.
PAPA WEMBA wiki moja kabla alikuwa na tatizo la heart attack na physician wake alimwambia apumzike wiki mbili ndipo arudi kuendelea na mziki na ile siku aliyofariki ndiyo kwanza alikuwa kamaliza siku ya tano ( 5 ) tokea atoke kupewa huo ushauri na daktari wake je ulitegemea nini hapo Mkuu? Na ukumbuke kuwa hawa Wanamuziki wakubwa na matajiri wa Kongo hawatibiwi na Madaktari " hohe hahe " bali Madaktari wao huwa ni wale WATAALAM na BINGWA kabisa wanaojua wanafanya nini. Uzembe wake wa kutozingatia masharti ya afya ndiyo yamemfanya apoteze maisha kwa heart failure na pengine hiki KIFO cha PAPA WEMBA kiwe fundisho kwetu kuzingatia yale yote tunayoambiwa na Madaktari.
Kwani Papa wemba alijihusisha na siasa? wamuue ili wapate nini, alikuwa na ugomvi na nani? au hakuheshimu wake za watu, tuelezeeni kwanza maisha yake kwenye jamii iliyomzunguka yalikuwaje?
Ndipo tutapata pa kuanzia kujiunga nanyi ku speculate.
Kwa maana hata mwanamuziki mkongwe wa reggae Joseph Hill "culture" alifia stajini huko ujerumani.
Joseph Hill - Wikipedia, the free encyclopedia
Nimeweka hiki kipambanuzi ili kuubaini uwezekano wa kufia kwenye stage ukiperform.
Maelezo mazuri ingawa unaweza kuwa unapotosha...Ukiiangalia vizuri ile video yule mtoa mike alionekana kabisa ananyatia, the guy seemed not an official assistant of PAPAA WEMBA, he was the asshole bitch with coward action!!
Polonium haiui mtu ghafla mkuu. Hii inakuua polepole kwa kuua viungo muhimu one after another na mwisho wake unapata massive multiple organ failure ndiyo unaondoka. Ni kifo cha mateso sana!Hiyo sumu inaitwa'' Polonium 210 is a chemical element'' with symbol PO and atomic number 84,
A rare and highly radioactive element with no stable isotopes.
Polonium is chemically simiral to bismuth and tellerium and it occurs in uranium ores.
Application of polonium are sparse and include heaters in space probes.
Antistatic devices or as source of neutrons and alpha particles.
NOTE;
Polonium is highly dangerous toxic substance.
Refer the death of Alexander Litvinenko.
Polonium 210 is a problem to human being only when it gets into the body,
The radioactive substance can enter into the body by eating or drinking contaminated things ,by breathing contaminated air or inhaling or ingesting body
fluids from someone contaminated with it.
kwa kesi ya Papa Wemba itabidi kusubiri uchunguzi wa kitaalamu na Madaktari bingwa ndio watasema ukweli na hii inategemea familia yake .
Mnunulisho wa hii sumu ya polonium 210 inaonekana kama hatua ya mwisho wa mgonjwa wa kansa,
inaathiri Maini,Figo,na mfumo wa hewa na maumivu makali ya kichwa.
Ata baada ya kifo cha Yasser Arafat kulikuwepo na uvumi wa aina hiyo lakini mamlaka za Palestina mpaka leo zinakanusha kwamba ni kifo cha kawaida tu.
Hapana mkuu! Silazishi ukubaliane Na Mimi, nlikua nataka tujadiri kile tunachoona kwenye video, kwa mfano kwa uelewa wako WA Muziki WA Kongo, nilitegemea ungechangia hivi (baada ya kutazama video)....May be Swala la kutolewa Mic Na stand yake Na kuletwa nyingine Ni kawaida, hata Mic Na stand yake ilipotolewa baada ya Papaa kuanguka Ni kawaida, coz Papaa Ana Mic zake Special Na Ni za gharama kubwa, so ilijulikana hangeweza kuendelea tena Na show ndo maana Mic yake ikatolewa Ili ikahifadhiwe! Mfano hapo juu ndo nilitamani kusikia, yani maoni yako baada ya kutizama video!......na sio kukulazimisha ukubaliane Na Mimi.
Kwenye makala hizi ,ndipo huwa nafurahi kupata stori zako Popoma.Hata kama ni uongo,lakini unavyonegesha stori wasokujua lazima waamini.Unaandka vizuri sana,ila asilimia 90 ni kamba tupu
Kongo kila kifo kina speculation... Naina na watanzania tumeanza kuwa hivyoKwenye makala hizi ,ndipo huwa nafurahi kupata stori zako Popoma.Hata kama ni uongo,lakini unavyonegesha stori wasokujua lazima waamini.Unaandka vizuri sana,ila asilimia 90 ni kamba tupu
Papa Wema, Joseph Hill, Mariam Makeba wote walikufa wakifanya kile wakipendacho. Autopsy si ajabu ikaonyesha ni massive fatal heart attack iliyosababishwa na kujitumikisha kupita kiasi, kutojali afya kutokana na kuwa bize muda wote, matatizo ya moyo ya muda mrefu (yanaweza kuwa hata hayajulikani) na sometimes ni critical dehydration kutokana na homa ya kawaida tu.
When it is time to go you must go hakuna ujanja. Prince naye kaanguka kwenye elevator kutokana na matatizo ya kutojali na kutochukulia mambo serious. Ana flu anakwenda kununua over the counter medication pharmacy za Wallgreens mara kwa mara kumbe tatizo ni kubwa.
Wapumzike kwa amani wapendwa hawa. Wamekufa kwa ghafla bila mateso ya kuumwa kwa muda mrefu tena wakiwa wanafanya kile wakipendacho. Sisi hatujui tutakufaje. Mungu na Atusaidie!
Polonium haiui mtu ghafla mkuu. Hii inakuua polepole kwa kuua viungo muhimu one after another na mwisho wake unapata massive multiple organ failure ndiyo unaondoka. Ni kifo cha mateso sana!
Wemba alishavuka miaka ya kuwa kileleni
Heart failure imemuua... Waafrika tunapenda sana conspiracy, mauchawi na majungu
Asante sana mkuu and coming from you, I am humbled. Mimi huwa ni muumini mkubwa wa rational thinking kwanza na siyo hizi conspiracy theories ambazo mara nyingi huwa hazina mashiko. Nilikuwa hata nawaza aina ya sumu inayoweza kuua mtu ghafla kwa kunusa microphone tu. Nerve agent? Sumu kama hii inakuwa dispersed through the air na ni lazima iwe concentrated na yenye nguvu sana kiasi kwamba hata anayeitega ni lazima avae mask. Hii siyo sumu ya kutegwa hovyo hovyo tu tena katika ukumbi wa dansi. Lazima kungekuwa na watu wengine ambao wangepata angalau kizunguzungu na kuanguka. Na hii ni very high risk mission kisa tu kwenda kumuua mwanamuziki ambaye hao wauaji wanaweza kumuua kirahisi tu kwani siamini kama alikuwa analindwa. High risk mission kama hizi walikuwa wanajaribu CIA wakati ule wakihangaika kumuua Fidel Castro. Lakini kwa Papa Wemba? Haiingii akilini kabisa.Huwa nawapenda mno na sana Watu wenye AKILI, UPEO, MAARIFA na FIKRA zilizotukuka kama Wewe Mkuu na umedhihirisha kuwa hukwenda Chuo Kikuu kula tu Pilau, Ugali na Chips kama wengine wanavyonithibitishia kwa aina mbovu sana na analysis wanayoifanya juu ya KIFO au sababu KUU iliyopelekea PAPA WEMBA kupoteza maisha. ANDIKO lako Mkuu limemaliza kila kitu na nadhani mada sasa iwe tu close. JF inatakiwa iwaenzi sana Watu wa aina yako wenye kujua kufanya TAFAKURI TUNDUIZI ( critical thinking ) juu ya MASUALA ( issues ) kwani ndiyo mnadhihirisha kuwa kweli JF ni home of great thinkers. Nimekukubali KUNAKOTUKUKA Mkuu safi sana!
GENTAMYCINE ukitulia unakuaga kichwa sana but maji yakijaa baharini tu majanga....respect sana kwa haya maelezo yako.Pole sana Mkuu kwa kuwa na mashaka ya Kifo cha Jules Shungu Kikumba Pene Wembandio alias PAPA WEMBA na pole pia kwa wale wote walioguswa na huu msiba wa JABALI la Afrika ambalo lilibaki la Kizazi cha kwanza baada ya Franco, Tabu Ley, Kabasele Yampanya PEPE KALLE, Madilu System.
Ukweli wa sababu ya Kifo chake ni MSHTUKO wa MOYO kwani imegundulika kuwa wiki moja kabla ya kwenda Abidjan alikuwa anaumwa sana BP na alipewa tiba ambayo ilimlazimu apumzike kwa angalau wiki mbili ndipo arejee kuendelea na muziki lakini mara baada ya PAPA WEMBA kuona kapata nafuu na huku tena Watu wa Kundi la Muziki maarufu ya nchini Ivory Coast la MAGIC SYSTEM ambao ndiyo walikuwa waandaji wakuu wa lile TAMASHA kumpelekea mwaliko aliona asikose kwenda kwani alitaka kuitumia hiyo siku pia kutambulisha album yake.
Kwa mnaoingia sana katika kumbi za muziki nadhani mnatambua aina ya sauti kubwa ambayo inaambata na mitambo mikubwa kabisa na spika za kufa mtu ambazo zinapiga kiasi kwamba kama una matatizo ya kushtuka kwa moyo au kisukari huwezi kukaa pale hivyo hata Marehemu PAPA WEMBA wakati amepanda pale stejini huku akiwa ana siku tano tu tokea atoke kwa Daktari wake kwa matatizo ya moyo ilikuwa ni dhahiri kuwa ile sound set up ya pale ingemuathiri.
Kujibu swali lako kwamba labda aliwekewa SUMU baada ya kuona yule Mtu anakuja kuitoa ile Mic pale na baadae kurudi na nyingine si kweli kwamba ni SUMU bali kila Mwanamuziki Kiongozi wa Bendi huwa na Mic yake MAALUM ambayo husetiwa KIUTAALAM sana na Band Sound System Engineer na hufanyiwa test mara kwa mara ili Bwana mkubwa akipanda nayo tu pale mbele isimumsumbue na huwa haiwi moja bali huwa mbili.
Na pia tambua kuwa kila Mwanamuziki Kiongozi wa Bendi hasa za Kikongo huwapa jukumu MAALUM watu wanaowaamini sana na mno la kukaa au kutunza hizi mic ili kuepuka hujuma kwani kwa msiojua hakuna Watu ambao huwa Wanarogana katika muziki kama Wakongo na ikumbukwe kuna wakati Werrason alimchezea mchezo JB Mpiana katika TAMASHA ambapo katika huo Uwanja kulinyesha mvua kubwa sana lakini cha kushangaza pembezoni na huo uwanja JUA KALI lilikuwa linawaka ( mfano wake ni kwamba pale ukumbi wa Diamond Jubilee sasa pawe wazi halafu inyeshe mvua kubwa lakini maeneo ya jirani kama Makao Makuu ya SKAUTI, Makao Makuu ya Jeshi, Shule ya Msingi ya Muhimbili na yale maeneo mengine kote kuwe na jua kali na linawaka kisawasawa ) hivyo kupelekea JB Mpiana kutofanya onyesho lake na alipokuja kugundua kuwa alifanyiwa ule mchezo na Werrason na yeye JB Mpiana akalipiza ambapo siku moja Werrason na bendi yake ya Maison Mere walikuwa na onyesho lao na cha kushangaza kila Werrason akishika Mic sauti haitoki lakini akiondoa tu ile Mic sauti inarudi na hata alipobadilishiwa Mic zingine tatizo lilikuwa ni lile lile hali ambayo ilipelekea sasa vipande vyote vya uimbaji vya Werrason aviimbe mwanamuziki wake aitwae Herritier lakini cha moto alikiona.
Mshika Mic mkuu wa Koffi Olomide ni yule Mkewe wa sasa aitwae Cindy ambaye ni Mwanamuziki wake pia japo hapo kabla mshika Mic wake alikuwa ni yule muimbaji aitwae Gibson a.k.a Kardinale huku mshika Mic mkuu wa Werrason ni yule mpiga drums wake maarufu aitwae PAPII KAKOL huku JB Mpiana mshika Mic wake mkuu akiwa ni Rapa wake kipenzi aitwae Gentamycine au Antibiotique Lisimo. Hao washika Mic wao wote ndiyo Watu ambao WANAAMINIKA nao kuliko Mtu yoyote katika bendi zao zote hizo na ndiyo wenye sauti kuu pia ya KIMAAMUZI ndani ya hizo bendi za hao MANGULI wa muziki tajwa hapo hivyo kuwekewa SUMU ni jambo gumu mno Mkuu na hawa jamaa Wakongo wanajilinda na vingi na hasa hasa ni NDUMBA.