Da Asia
JF-Expert Member
- Sep 25, 2011
- 731
- 819
Kusema ukweli sijapata nafasi ya kuitizama ila kidogo Mkuu wangu nina uzoefu na hawa Wanamuziki hasa wa miziki hii ya dansi ya Kikongo na hata hapa kibongo bongo kwa hizi bendi zetu pia. Sitaki uamini 100% yale maelezo yangu kwani yawezekana ikawa ni Sumu kama usemavyo ila nimekuelezea tu kwa uzoefu wangu na ni ngumu mno kuwekewa SUMU katika Mic anayoenda kutumia isipokuwa ungeniambia kuwa alifanyiwa UCHAWI ningekuamini kwa asilimia zote kwani hakuna Mwanamuziki unayemjua Wewe wa DR Congo ambaye HAROGI. Kuna siku nitakuja na UZI hapa nikuambie UCHAWI wa wote hao hasa hasa Koffi Olomide, JB Mpiana, Werrason, Roga Roga wa Bendi ya Extra Musica, Zaiko Langa Langa, Hayati Pepe Kalle, Hayati Madilu System na hawa vijana wa sasa wawili Fally Ipupa na mwenzake Fere Gola. Mkuu nikikuambia wanayoyafanya unaweza hata ukaogopa kulala au ukazichukua dvd zao hapo ulipo sasa na ukazichoma moto! Wanamuziki ambao najua walikuwa HAWAROGI ni Hayati Franco na Hayati Tabu Ley pekee.
Ili kunogesha maelezo yako, naomba utuletee hizi habari za uchawi asap kabla vuguvugu la Papaa halijapoa