Ni kweli pilau lina sumu zaidi ya 10?

Ni kweli pilau lina sumu zaidi ya 10?

tomjelly

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
560
Reaction score
198
Habarini wapendwa,

Nimekuwa nkisikiasikia mara nyingi kua chakula aina ya pilau sio kizuri kwa afya ya binadamu. Hivyo nimekua nikikikwepa, pia pindi nilapo chakula hiki lazima tumbo linisumbue. Tena kuna tetesi ambazo mi binafsi sijazithibitisha kuwa chakula hiki kina sumu takribani zaidi ya 10.

Naomba mwenye uelewa kuhusu hili anifafanulie kwani kinachonichanganya zaid ni kwamba chakula hiki mara nying hupikwa na viungo asilia kabisa ambavyo pengne ni tiba mfano: vitunguu swaumu, vitunguu maji, iriki, mdalasini na bizari nyembamba.

Sasa Swali ni je! kivipi hasa pilau huwa sumu?

Natanguliza shukrani.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kuhusu suala la sumu ninachoelewa ni kwamba wengi pilau huwaletea shida tumbo kujaa gesi kwasababu ya spices
 
Sijui kuhusu suala la sumu ninachoelewa ni kwamba wengi pilau huwaletea shida tumbo kujaa gesi kwasababu ya spices

spices ndio nini? naomba niambie japo kwa ufupi mkuu. samahan kwa usumbufu
 
spices ndio nini? naomba niambie japo kwa ufupi mkuu. samahan kwa usumbufu

"Spices " anaamanisha viongo. Pilau linawekwa viongo vingi kama mdalasini, hiliki, pilipili mtama n.k.
 
Chakula tangu lini kiwe na sumu? ina maana hao wanaopika mahotelini Pilau huwa wanatia ndani yake Sumu? Mkuu tomjelly jaribu kujieleza vizuri.

ahsante mkuu MziziMkavu kwa kutia neno hapa. ni hivi mimi kwa maoni yangu chakula kinaweza kuwa na sumu ndio, na nnavyosema sumu simaaanishi tu kua itakuua moja kwa moja bali namaanisha unaweza ukawa unajiua taratibu kwa kula aina fulani ya vyakula, mfano vya kusindikwa, vyenye sukari na chumvi nyingi (salt & sugar are sweet poison), vyenye mafuta mengi, n.k.

Nimeileta hii mada hapa jukwaani sababu ni miaka kadhaa imepita tangu niliposkia kwenye television kua daktari mmoja wa tiba mbadala/asili/hebarist mashuhuri nchini, angechambua sumu takribani 14 zilizopo kwenye PILAU siku hiyo saa 4 usiku, bahati mbaya sikufuatilia. ila nliweka akilini kua pilau si chakula bora kwa afya ya binadamu kutokana na kumuamini huyu dr. japo sikufanikiwa kutazama uchambuzi wake ucku huo.
 
Je hizo spices \ viungo vinadhuruje? Naombeni majibu kwa anaefahamu chochote kuhusu hili, ni wakati gani na kivipi na ktk mechanism ipi hasa chakula hiki (PILAU) ni harmful Kiafya? Bado sijapata jibu la kitaalamu.
 
angepatikana anaejua kupika pilai standard humu ndani na kuelezea kimoja kimoja kinachowekwa mpaka unapata pilau na process zake tungejua kuwa ni sumu au sio sumu
 
angepatikana anaejua kupika pilai standard humu ndani na kuelezea kimoja kimoja kinachowekwa mpaka unapata pilau na process zake tungejua kuwa ni sumu au sio sumu

good idea, tuwaite kwa kuwa-tag nafikiri wapo weng huko jukwaa la mapishi.
 
M nngeshakufa coz naipenda vbaya mno

sio lazima ufe mapema, ila kuna uwezekano kuwa kwa kupendelea kula baadhi ya vyakula utaweza kupata shida ukifikia umri fulani sababu ya sumu zilizokua zikijirundika mwilini kutokana na lifestyle ya siku za nyuma.
 
Mimi navyojua ni kwamba siyo sumu kama sumu ulivyoelewa ila wewe mpikaji ndo unaweza kuifanya kuwa sumu kwa mambo ya fuatayo:-

1.kuweka mafuta mengi sana...watu wengi wanapopika pilau huweka mafuta mengi sana kwa madai ya kwamba ndo linanoga .

2.Uwekaji wa viungo vingi sana ......watu wengine hupendelea viungo vingi kwamba ndo linakuwa tamu,hii hupelekea kuleta shida kwa wengi kwa kupata gas tumboni au kuharisha pia mafuta ni sababu.....pia gas ikizidi sana hupelekea vidonda vya tumbo.

3.Wengine hupika lile pilau la vitunguu maji ambavyo huunguzwa sana na kuwa vyeusi kabisa .....hii direct kwa kufanya hivi ni sumu tosha.

Suluhisho

1.Vizuri kutumia mafuta kiasi na mafuta mazuri hasa Yale yatokanayo na mbegu kama Alizeti,Olive,karanga n.k haya hayana cholesterol.

2.Kuweka viungo vichache vya aina moja,kwanza sikuhizi pilau halipikwi kwa viungo vingi, siku hizi watu huweka aina mbili au tatu tu na mwingine moja kabisa.

3.Kuacha upikaji wa pilau kwa kuunguza vitunguu.

4.Pia sababu red meat(nyama nyekundu) imekuwa ni shida na sababu nyingi ya kuleta Magonjwa . Kama ni mlaji sana wa pilau vizuri kutumia white meat(nyama nyeupe) kama kuku kwa upikaji wako.
 
everlenk Ubarikiwe kwa maelezo mazuri yenye elimu stahiki. Nashkuru sana. Tazama sikukuu za christmass na mwakampya zaja. hakika ntaifkisha elimu hii ktk kaya nnazoishi.
 
Last edited by a moderator:
Mada nzuri saana.....huyu bwana hamanishi pilau tunayokula anayo maana nyingine kubwa saana.hebu msomeni "in between the lines" Big up muanzishaji wa huu uzi
 
Back
Top Bottom