Ni kweli pilau lina sumu zaidi ya 10?

Ni kweli pilau lina sumu zaidi ya 10?

ahsante sana MziziMkavu kwa kunitoa tongotongo.

Sasa ntaanza kulila kwa fujo, hasa pilau lilioandaliwa vizuri (kitaalamu). Ili nsisumbuliwe tumbo.

Kinachopelekea kuumwa tumbo pengine ni wapishi kuzidisha viungo kipita kiasi
 
Last edited by a moderator:
Kinachopelekea kuumwa tumbo pengine ni wapishi kuzidisha viungo kipita kiasi

exactly! mkuu Nimegundua hili ndo tatizo haswaa! pia na kuviunguza had vinakua vyeusi / mkaa. bila kusahau kumiminia mafuta utadhani yamemwagikia!!!. :becky:
 
exactly! mkuu Nimegundua hili ndo tatizo haswaa! pia na kuviunguza had vinakua vyeusi / mkaa. bila kusahau kumiminia mafuta utadhani yamemwagikia!!!. :becky:

Pole, hilo sio pilau sasa, viungo vinatakiwa viwe brown na sio vyeusi, mafuta yawe masafi na yasizidi (I prefer olive oil) uwe unapika mwenyewe na usisahau kuweka zabibu kavu ili litoke tamu zaidi.
 
Pole, hilo sio pilau sasa, viungo vinatakiwa viwe brown na sio vyeusi, mafuta yawe masafi na yasizidi (I prefer olive oil) uwe unapika mwenyewe na usisahau kuweka zabibu kavu ili litoke tamu zaidi.

Ahsante mkuu. siku za kupika pilau home ntakua nasimamia show mwenyewe.
 
Duuh, Jana mwisho nimekula pilau.

Pitia uzi taratiiibu utaelewa kua pilau kiuhalisia sio sumu bali Zaidi asilimia 90% ya waandaaji huku kitaani (bongo) ndo hulifanya liwe sumu.
 
Habarini wapendwa,

Nimekua nkisikiasikia mara nyingi kua chakula aina ya pilau sio kizuri kwa afya ya binadamu. Hivo nmekua nkikikwepa, pia pindi nilapo chakula hiki lazima tumbo linisumbue. Tena kuna tetesi ambazo mi binafsi sijazithibitisha kuwa chakula hiki kina sumu takribani zaidi ya 10.

Naomba mwenye uelewa kuhusu hili anifafanulie kwani kinachonichanganya zaid ni kwamba chakula hiki mara nying hupikwa na viungo asilia kabisa ambavyo pengne ni tiba mf: vitunguu swaumu, vitunguu maji, iriki, mdalasini na bizari nyembamba.

Sasa Swali ni je! kivipi hasa pilau huwa sumu?

Natanguliza shukrani.

Wapendwa mulioshiriki huu mjadala.......niwaombe kwa nia njema tu musome tena hilo bandiko la ndugu yetu..murudie mara mbili na muwaze nje ya Hii pilau au Hili pilau na muchukulie day to day activities,nadhani tutakuwa na jibu sahihi la pilau.Tomjelly yuko makini saaana na anaangalia mbali...hebu tumpe challange nasi tujifunze.Tukatae siyo pilau ya kuliwa.
 
Changamoto ya kwanza: kwa nini Tomjelly kaleta uzi wake tarehe 11th Dec kwa nini isiwe siku 10 au 15 kabla ya hiyo 11th Dec.
 
Changamoto ya kwanza: kwa nini Tomjelly kaleta uzi wake tarehe 11th Dec kwa nini isiwe siku 10 au 15 kabla ya hiyo 11th Dec.

Labda post hii imekuja december. kwasababu sikukuu za new year & christmas zimekaribia ambapo siku hizo Mapilau huungurumishwa karibu kila nyumba. :becky:
 
Kinachopelekea kuumwa tumbo pengine ni wapishi kuzidisha viungo kipita kiasi

basi bwana Nakumbuka siku moja nlikaribishwa pilau kwenye nyumba flani ya wahindi. yaani pilau lipo kwenye sahani ndogo tu ila linaelea kwenye mafuta ambayo ukiyachuja unaweza jaza kikombe cha kunywea kahawa. kama unalia mkono basi ukichukua tonge halafu uinue mkono mafuta yanachuruzikia kwapani. :becky::becky::becky::becky:
 
tomjelly.....pamoja na yote mimi binafsi sikubali kama una maanisha pilau ya kuliwa.niwe mkweli.. tatizo langu ni kuhamisha ninayo amini kuyapeleka kwa mwingine akayaelewa na kuyakubali
 
Last edited by a moderator:
Wewe sema tu kwa uwazi ambacho unaamini kinazungumziwa hapa. bantu.garage yatakua ni maoni tu na nafkiri yataheshimiwa. usiogope.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom