Ni kweli Rais Samia ana nasaba na familia ya Mfalme wa Oman?

Ni kweli Rais Samia ana nasaba na familia ya Mfalme wa Oman?

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Habarini

Nimeona hii kitu ikanistua, naomba kujuzwa juu ya huu undugu na kama kweli, wanyama wetu watabaki kweli?

Maana enzi za awamu ya mzee ruksa, mkewe alituhumiwa/shutumiwa kusafirisha wanyama hai kwenda arabuni saivi Rais Samia anasema ataimarisha usafiri wa majini ili kusafirisha wanyama hai.

Nijuzeni kuhusu hili swala.
Screenshot_20220614-195946_WhatsApp.jpg


==================

Taarifa hii imetolewa ufafanuzi hapa: NADHARIA - Ni kweli Rais Samia ana nasaba na familia ya Mfalme wa Oman?
 
Kitu muhimu kwa nyakati hizi ni kuwafundisha watu wetu kuishi kwa akili. Waafrika waishi kiafrika wakijilinda, waarabu, wahindi na wazungu vivyo hivyo.

Jamii zimeingiliana , zimezaliana na hivyo watoto, wajukuu na vitukuu hawana shida yoyote.

Watu wetu waishi kwa utayari wa ushindani na kutumia akili za kawaida kulinda taifa letu.

Kelele na maandishi ya kipropaganda ni zilipendwa. Tupambane katika hali halisi. Uwezo wa kumshinda yeyote duniani tunao.

Haya yote ya ubaguzi wa wazi ni woga unatokana na fikra za kizamani.
 
Hao jamaa!

Wanahusishwa na ukatili kwetu na kutudumazankimaendeleo!!

We hujui jamaa walikuwa ndio wafanya biashara wa utumwa!!?

Waarabu wanamchango mkubwa wa kudumaa kwa maendeleo maeneo waliyoishi humu kwetu NCHINI!!
Inaonekana wewe ni kichwa maandazi. Uwezo wako wa kutafakari mambo ni sawa tu na wa watoto wa shule ambao wanaweza wakapewa taarifa fulani na wakashindwa kuing'amua juu ya ukweli na uongo wake.
 
Obama Pia ni Mkenya
BwM nae ni …
Na katika hili halitoonekana tatizo lolote lile. Ila atokee tu mtu awe na uhusiano wa kiukoo na familia za kiarabu basi hali ndio kama hii unayoiona.

Islamophobia ni tatizo ambalo watu hawajawa tayari kulishughulikia. Kimsingi watu wasio waislam wanatengenezewa woga wa hali ya juu kuhusu Uislam. Hapa yote haya ni kwasababu ya dini ya Mheshimiwa rais.
 
ni kawaida kwa wanzanzibar wenye asili ya pemba kuwa na unasaba wa kindungu na waarabu wa oman.

hata marehemu jiwe anadaiwa alikuwa na unasaba na wahutu wa burundi, mkapa na wamakonde wa msumbiji.

lakini pia nyerere wanasema naye alikuwa na ndg zake kati ya rwanda na burundi.
 
Hao jamaa!

Wanahusishwa na ukatili kwetu na kutudumazankimaendeleo!!

We hujui jamaa walikuwa ndio wafanya biashara wa utumwa!!?

Waarabu wanamchango mkubwa wa kudumaa kwa maendeleo maeneo waliyoishi humu kwetu NCHINI!!

Kwa hiyo ulidumazwa na ukakubali kudumaa kwa miaka zaidi ya 250 seriously [emoji19]
Ndio maana mnashindwa kuendelea na kutwa kutegemea misaada na kuomba

Kwa sababu ya kuwa dhalili kiasi hiki
Tuache fikra hizi kwani huu ndio utumwa wa akili
 
Mkuu

Tetesi

Kuwa mama atoka kwenye kiuno cha ruksa na pia mama yake mama ni muoman!!pia Dada yake mama yaani Mtoto wa Mzee ruksa kaolewa huko KWA mwanamfalme wa uarabuni!!!ni ukoo mkubwa Sana tu kwakweli kama tetesi ni za kweli!!
Kama hiyo tetesi ina ukweli basi Mama ni Mtanganyika wa Mkuranga 😂😂😂
 
Na katika hili halitoonekana tatizo lolote lile. Ila atokee tu mtu awe na uhusiano wa kiukoo na familia za kiarabu basi hali ndio kama hii unayoiona. Islamophobia ni tatizo ambalo watu hawajawa tayari kulishughulikia. Kimsingi watu wasio waislam wanatengenezewa woga wa hali ya juu kuhusu Uislam. Hapa yote haya ni kwasababu ya dini ya Mheshimiwa rais.

Hawa wenye akili hizi ni wabaguzi ambao hawajawahi kuvuka hata mipaka waliopo

Wamejifungia kwenye bubbles na kuwa na mawazo mengine ni vigumu sana
Wivu na roho mbaya ya kujiona wao ni wabora kuliko wengine wakati miaka zaidi 250 tangu mababu wameuzwa bado wanalalamika tu na kutwa kuombaomba

Najaribu kujiuliza Kuna shida gani kuwa na asili ya kiarabu?
 
Back
Top Bottom