Ni kweli serikali ya Samia inaagiza Mayai na kuku wa kula Ikulu Marekani?

Mnapenda sana uzushi na uongo. Muda wote mnawaza namna ya kutunga uongo na kuleta uchonganishi tu . Kazi yenu ni uropokaji Utafikiri walevi wa gongo waliojimiminia wakiwa na njaa tumboni.

Yote hiyo inatokana na hofu ,uoga ,chuki binafsi na wivu wa kuona namna Rais Samia anavyokubalika,kupendwa na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania. Mnajaribu kwa kila njia kutaka kumchafua Rais wetu Mpendwa lakini mbinu zenu zinaendelea kugonga mwamba na kushindwa kufanikiwa kabisa.

Mtaongea kila aina ya uzushi na uongo lakini Mheshimiwa Rais ataendelea kuchanja Mbuga katika Mioyo ya Watanzania. Mama ni Mpango wa Mungu aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu. Hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kumshusha hapo alipo.
 
Chawa pro Max VPN
 
Mimi sipendi inchi inavyoendeshwa,hapa Kuna mradi wa barabara km kama 55 hivi,umetiwa Saini lkn umeahirishwa bila sababu ya msingi.lkn namtaka heche aache kutamka vitu visivyo na ushahidi kwenye mikutano yake badala ya kumjenga vinaweza kumbomoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…