Ni kweli smart TV zinatumia Umeme Mwingi?

Ni kweli smart TV zinatumia Umeme Mwingi?

Mwenzako kaomba elimu we unamletea kejeli
Kuna vitu huwezi kuviwazia kabisa kwenye vitu vya umeme! Uwe una kaa kwako au umepanga cha kwanza TV, king'amuzi, feni sio vitu vya kuwazia kabisa! Deki ya CD, breender, heater, jiko la umeme, rice cooker, pressure cooker, pasi ya umeme ndio vya kuumiza kichwa
JamiiForums154410317.jpg
 
Mimi binafsi Kwa uchunguzi nilioufanya niligundua smart tv ya mtumba inatumia umeme mwingi kuliko ya dukani

Nilikuwa nikiwasha smart tv ya mtumba Baada ya muda ukigusa Kwa nyuma Kuna kuwa na joto Kali sana kiuhslisia lile joto ni umeme

Baada ya kununua smart tv ya dukani ukiwasha hata kama kutwa mzima ukigusa Kwa nyuma hakuna joto
Uliweka mahala pale pale uskute ukuta mmoja baridi mwingine wa moto
 
Nimesikia mara nyingi watu wakisema kwamba Smart TV zinatumia umeme mwingi, na kama ni kweli, why zitumie umeme mwingi, naomba kupewa elimu, asanten[emoji120]
Si kweli, kitu kinachofanya TV iwe smart ni kifaa kidogo sana kinachotumia processor ya simu lowend (cortex A53 ama A55) hivyo usmart wa TV unaongeza watts kama 3 tu.

Tv kula umeme mwingi inatokana na Panel unayotumia, Oled, Led, Plasma etc.
 
In comparison to what ? Nadhani hilo ni swali la maana zaidi....

Unaweza ukasema Pipa linachukua nafasi zaidi kuliko kikombe lakini kumbe lihahifadhi maji zaidi kuliko ungepanga vikombe ili uweze kutunza hizo lita 200

 
Kama chombo chako ni 5000W ujue ukikitumia kwa mda wa Saa Moja utatumia 5 units. W inamaanisha joules per sec.
 
Nimesikia mara nyingi watu wakisema kwamba Smart TV zinatumia umeme mwingi, na kama ni kweli, why zitumie umeme mwingi, naomba kupewa elimu, asanten[emoji120]
Hizo ni story za vijiweni tu hazina ukweli sababu pamoja na kwamba ni smart ila ni LED hivyo ziko poa tu
 
Ukweli ni kwamba kadri inavyokuwa na watts nyingi ndio umeme mwingi unatumika... Changanya na subwoofer unayotumia.... Wengi tunasema TV na redio hazitumii umeme mwingi bila kufanya utafiti.... Changanya na utitiri wa taa kwenye nyumba halafu tuendelee kuambizana stori za vijiweni...

Sent from my 2107113SG using JamiiForums mobile app
 
Nimesikia mara nyingi watu wakisema kwamba Smart TV zinatumia umeme mwingi, na kama ni kweli, why zitumie umeme mwingi, naomba kupewa elimu, asanten[emoji120]
Hata TV isiyo smart TV nayo inakula umeme na afadhali hizi za smart sababu zina mfumo tofauti na TV za kawaida, pia kama unatumia Home Theatre kwa pamoja umeme unaondoka tofauti na usipotumia.
 
Chombo chochote kinachotumia umeme angalia tu pawa yake "Watts".

Nadhani hapa kwenye “Watts” panachanganya

Kuna Watts za speaker na Watts za umeme zinazotumika

Sidhani kama zile watts zinaonekana kwenye subwoofer ndio consumption ya umeme
Maana bili zingekuwa balaa

I stand to be corrected
 
Back
Top Bottom