Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 12,001
- 27,175
Wakuu,
Kumekuwa na nguvu kubwa sana kuwaaminisha watu kwamba Tanga ndipo hasa 'yalipozaliwa mapenzi' au kwa maana nyingine ndio makao makuu ya mapenzi hapa Tanzania.
Hii imekuwa ikichagizwa zaidi na nyimbo za wasanii kama yule Bwana Misosi aliyeimba 'mabinti wa Kitanga' huku akiwapa sifa lukuki kuelezea uwezo wa katika tasnia ya mapenzi.
Pia kumekuwepo misemo kadhaa kama huu wa 'Tanga waja leo kuondoka majaliwa' yote kuonyesha kwamba mwanaume akijichanganya kwa binti wa Kitanga basi hawezi kurudi tena kutokana na kupewa mahaba ya hali ya juu ikiwemo kuogeshwa kwa maji ya Iliki na Mdalasini huku akibebwa mgongoni kwenda bafuni na kurudishwa nakadhalika.
Kwenye kipindi cha Valentine's mwaka huu kuna media fulani walikuwa wakirudia rudia sana kwamba Tanga ndipo mapenzi yalipozaliwa na waliandaa mpaka tour ya kwenda huko.
Je ni kweli mabinti wa Ki-Tanga ndio wanayamudu mapenzi kuliko mikoa yote Tanzania au ni kwamba wao ni wabingwa wa 'kupuliza' ili mwanaume asifurukute?
Ili tujue ukweli wa hili tupate majibu ya maswali haya;
1. Je, Tanga inaongoza kuwa na ndoa zinazodumu hapa Tanzania?
2. Je, mabinti wa Kitanga ndio wanaoongoza kuolewa zaidi kuliko mabinti wa mikoa mingine?
3. Je, mabinti wa Kitanga ndio wanaodumu kwenye ndoa zaidi hapa Tanzania?
4. Je, wanaposema Tanga ndipo mapenzi yalipozaliwa,Je na wanaume wa huko nao ni wajuzi katika mapenzi au ni wanawake tu,maana hatusikii wakizungumzwa?
Kwa Mliowahi kuishi /mnaishi Tanga au mliooa mabinti wa Kitanga tunaomba ukweli wa hili.
Asante.
N:B Jibu kwa namba ya swali.
View attachment 2152729