Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Jamanieee hao usalama ni watu wa kawaida tu (hususani hawa wa hapa kwetu)

Tofauti kubwa iliyopo ni kwamba wanafanya shughuli zao kwa SIRI. Hapo ndio nguvu yao ilipo.

Hata wewe ukiweka maisha yako PRIVATE watu watakuwa wanakuogopa kwa kuwa hawakujui vizuri.

Hata Secret Societies kama Illuminati, Freemasonry, Klu Kla Klux et al zinatumia USIRI kama mbinu mojawapo.

Sababu nyingine: Kwa kuwa CCM inawatumia sana, hivyo imewapa nguvu fulani ( kuwaweka juu ya sheria kwa raia ) kiasi kwamba hata akikuonea huwezi kumfanya chochote.

Suala la kutoaminiana ni kawaida tu kwenye mambo ya ulinzi na usalama, hata walinzi hawaaminiani.

Na kuhusu kutojuana ni kawaida pia, hata mwalimu hajuani na walimu wote nchi nzima unless mmekuwa assigned sehemu moja.

Wanaruhusiwa pia kuwa na vifaa/silaha ambazo wewe raia huruhusiwi kuwa nazo kitu kinachowapa nguvu dhidi ya raia!

Mambo mengine yote ni yale yale.
Wanajuana sababu Wana tabia zilizofanana. Wengi ni wakimya, Kuna vigezo vingine wanavyo pia Kama physique na vingine.

Wakikutana walitaka kukutana Wana code zao ambazo wenyewe kwa wenyewe wanazijua. Kwa bongo hawawezi kufuga ndevu, kunywa pombe kupiga kiasi, kuropokaropoka.

Nadhani pia waliyoingia intake moja wanafahamiana lakini Kama hawakuwa mafunzoni pamoja so rahisi kufahamiana. Mfano Toss aliyekuwa attached Kwa mkuu wa wilaya hawezi kumjua Tiss aliyekuwa labda Sabasaba Tantrade mpaka wajitambulishe kwa namba or sort of a code

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini wasinywe pombe?au wasfuge ndevu +nywele?Me nadhan inategema upo kitengo gan..idara +kaz aliopangiwa mtu ndo inayomshape aweje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi nadhani wameathirika na zile story mitaani miaka hiyo na nashangaa sana mpaka sasa hv bado kuna watu wanaamini hivyo.
Hawa jamaa hawana usiri wowote wanajulikana sana tuu ula ni kwa sababu hawana uniform au sare kama jeshi la polisi au jw, magari yao ukiyaona utayajua, wanakoishi tunapajua nk nk.
Tofauti kubwa ni kwamba wengi wao ni kama jicho la tatu kwa serikali, kwa hiyo anaweza akawa polisi lkn majukumu yake ni zaidi ya polisi, au akawa meneja wa bank lakini jukumu lake ni zaidi ya umeneja, anaweza akawa mwalimu nk nk. Hivyo kujulikana au kutojulikana kwao kunategemeana na majukumu yao ya kiutendaji, ila wengi wanjulikanaga tuu kirahisi.
Pia kuna wale matapeli wa uswahilini watakudanganya kumbe hawana lolote, na hao ndio wanaopaint hii picha watu wengi walionayo kichwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi, weekend hiyooo na kamvua kwa mbali hapa Arusha!

Nipo Triple A hapa. Kuna jamaa yangu ananiambia eti wana usalama/TISS hawafahamiani na hawaaminiani kabisa!

Yaani kila mmoja ana majukumu yake na mahala pa kureport. Hawana mazoea ya mwenzangu uko wapi, unafanya nini!

Hawaaminiani, hawajuani kivile!

Hii kitu ni kweli au ni mfumo kama tu wa TAMISEMI au taasisi zingine?

Sent using Jamii Forums mobile app

Yote ni sahihi japo kuna zaidi ya hayo...na haina haja kuyasema we don't dare talk about Gallant state officers and men.
 
Hiyo ya kufungwa jela imeniogopesha sana
Kwa watu wa chini ni ukweli. Unaweza kuwekwa kitengo au kupewa kazi ambayo iliufanikishe lazima uwe muokota makopo ama muuza karanga. Saa zingine unapewa kesi unafungwa jela kutoka mpaka upate ulichotumwa.

Kuna OCD moja rafiki yangu sana anawaogopa wauza karanga hata awe mtoto. Hawa walitumika sana enzi za Jakaya

God save us

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote ni sahihi japo kuna zaidi ya hayo...na haina haja kuyasema we don't dare talk about Gallant state officers and men.
Ila wapo kawaida sana na kama ulikua ni mkazi wa Mwananyamala Royal au kijitonyama utakuwa umekutana nao sana na pia hua wanahadithia tu wanayokutana nayo kwenye kazi zao. Ni watu kama watu wengine hua tunapenda story zao maana hua ni behind the scene ya mambo mengi nao pia huchalala tukawakopesha pia so kwa kifupi labda ni ile licence to kill waliyonayo na hapo pia sio wote. Ila wapo wengine wamekaa kichangudoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weeee nan kakudanganya unakaguliwa kama kama kawa hata kama unajulukana labda tu atayekuwa zamu aamue kukupotezea au mtu ajisahau wakati akiwa na hudumia wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
Haujanielewa nasema kwamba TISS wanajuana na ndio maana wakienda kwenye vituo vyao vya kazi wakipita getini hawazuiwi kuingia maana aliyeko getini anajua kama ni mfanyakazi wa ndani humo iwe Malindi,Eagle Wing , Makumbusho etc
 
Sijui ni kwa nini lakini kila ninapoenda au kuishi basi watu hunichukulia tofauti sana, yaani huwa wananihusisha na hawa jamaa, mpaka sasa imefikia kipindi natamani NIWE kweli. Kuna sehemu niliwahi kwenda ikafikia kipindi nikikuta watu wanaongea basi nikifika wananyamaza au kubadili story mpaka niondoke hilo eneo(mwenyeji wangu akaniambia hao jamaa wanakuhisi wewe ni usalama) kuna mahali pia niliwahi pata kazi, basi ofisi nzima wananiogopa, kuna bro mmoja tulipozoeana sana ndio akaja kuniambia, watu wanahisi wewe ni usalama, wanakuogopa, tukirudi kitaa (huwa situlii sana hapo, ingia toka nyingi mpaka nimekuwa mkubwa) pia watu huwa wanamuuliza mzee wangu hivi huyu mwanao huwa mnaongea nae kweli (me mkimya) anafanya kazi gani? (Baba aliwahi niambia wanahisi wewe ni usalama) Yaani mpaka watu wazima wa mtaani wananiogopa, kila ninapoenda mimi huwa nakuwa treated tofauti, nahusishwa na hao jamaa mpaka nimezoea na nimejikuta naanza kutamani niwe Usalama kweli sasa. Huwa najiuliza mimi nina nini? Nina Onekana vipi? Sijawahi pata jibu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna baadhi ya movie ukiziangalia tu,,

Baada ya mda unajiona ww ni usalama[emoji86]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna aina nyingi za ndege zilizo hai na zisizo hai.
Kuna ndege akifa hakuna mdudu wala kiumbe chochote kula mzoga/mabaki yake.
Vivyo hivyo kuna ndege ikianguka hakuna wa kupona,ingawa hutegemea itilafu,aina ya ndege na yupi rubani wake.
Kuna ndege wala nafaka,nyama,majani,minyoo,asali za maua,matunda na hata samaki na nyoka.
Ninaamini ndege walio wengi wanafahamiana ingawa sio wote.
 
Wanabodi, weekend hiyooo na kamvua kwa mbali hapa Arusha!

Nipo Triple A hapa. Kuna jamaa yangu ananiambia eti wana usalama/TISS hawafahamiani na hawaaminiani kabisa!

Yaani kila mmoja ana majukumu yake na mahala pa kureport. Hawana mazoea ya mwenzangu uko wapi, unafanya nini!

Hawaaminiani, hawajuani kivile!

Hii kitu ni kweli au ni mfumo kama tu wa TAMISEMI au taasisi zingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kibarua kigumu kama hiki mkuu. Unaweza ukapewa kazi halafu baada ya kutoka tu nyuma yako anatumwa agent mwingine wa TISS kuja kukuchunguza kama na wewe utaenda kuifanya kazi yako kwa weledi. Kwa kifupi ni kwaba hakuna kuaminiana.

Zamani mtu ambaye yuko TISS alikuwa na uwezo wa kuoa/kuolewa na mtu ambaye sio TISS ila nowadays utaratibu umebadilika, ukiwa TISS unaoa/kuolewa na TISS mwenzako!
 
zibitisha kuhusukuoa au kuolewa
 
Duh! Duh! Mmh umedanganya hakuna kitu kama hicho ningetoa uthibitisho lakini kwa sababu za kiusalama siwezi ila umedanganya!
 
Back
Top Bottom