Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Wanajuana sababu Wana tabia zilizofanana. Wengi ni wakimya, Kuna vigezo vingine wanavyo pia Kama physique na vingine.

Wakikutana walitaka kukutana Wana code zao ambazo wenyewe kwa wenyewe wanazijua. Kwa bongo hawawezi kufuga ndevu, kunywa pombe kupiga kiasi, kuropokaropoka.

Nadhani pia waliyoingia intake moja wanafahamiana lakini Kama hawakuwa mafunzoni pamoja so rahisi kufahamiana. Mfano Toss aliyekuwa attached Kwa mkuu wa wilaya hawezi kumjua Tiss aliyekuwa labda Sabasaba Tantrade mpaka wajitambulishe kwa namba or sort of a code

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji22][emoji22]
 
Umekaa wap m nko restaurant hapa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mulemule mzee big up...niliwahi kutumika bila mwenyewe kujua katika haya mambo...nilipokuwa chuo nilikua na mahusiano na binti mmoja kumbe bhn ni MTU wa kitengo na nilikuja kujua mwaka wa pili wa masomo,na ana bosi wake kabisa ambaye ndio huwa anampa maelekezo siku moja nkamwambia natamani sana na Mimi nifanye kazi hii akanambia sikushauri ni kazi inayohitaji uzalendo na ni ngumu sana hasa kwa watu wa level za chini kama alivyokuwa yeye na akanambia pale chuo wapo wengi tu na huwezi kuamini wengine..sasa siku moja akanikutanisha na bosi wake bila kujua bosi akanitumia katika shughuli za nchi huku nikiwa sijui nilikuja kujua mwaka wa mwisho kabisa kazi ikiwa imeisha nilichoka...
 
Ni kweli tunafundishwa kutokuaminiana maana mtu unayemuamini anaweza kukuchoma muda wowote.
 
Itakuwa umetumwa uje ufanye uchunguzi juu hili kwa akina sie 'miangu nene nzala tee' kama tunafamu kuwa wazee wa k. Nyama wanajuana au la.. wanajuana kwenye majukumu au la! Wadau washakujibu mkuu TISS kilichobaki we peleka ripoti ofisini
 
Hata Kama Siyajui haya mambo Lakini kwa logic ya kawaida kabisa.
Kama wanaenda kozi wataachaje kufahamiana walioenda kozi intake Moja?
Kama wanaofisi wataachaje kufahamiana walio ofisi Moja?
Kama kuna kazi wanazifanya kwapamoja wataachaje kufahamiana?
Ninavyoona Itakua kuna watu wnaopewa majukumu maalumu na hivyo kutofahamika kwa urahisi, pia baadhi ya undercover kutokana na unyeti wa kazi zao huenda hawafahamiki.
Utaachaje kumjua DSO au RSO na watu wake kwenye ofisi husika na kila majukumu wanaonekana na Watu wanafanya nao kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye kufuga ndevu, si kweli kwamba hawafugi, wasiofuga ni wale wanaofahamika. Kila mtu ana purpose yake katika eneo husika kuna wengine ni wazugaji tu, wanakuwa na mwonekano usiokuwa wa kimaadili ya utumishi ili watu wasiwastukie. Hao ndio wakusanya taarifa wazuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…