Ni kweli tumefungwa lakini kitendo cha kuwazomea wachezaji bandarini hakikubaliki na siyo cha kimichezo

Ni kweli tumefungwa lakini kitendo cha kuwazomea wachezaji bandarini hakikubaliki na siyo cha kimichezo

Mashabiki wa msimbazi kazi kweli kweli. Yaani mnataka kushinda tuuu basi hakuna haja ya kuingia uanjani. Kaeni getini muokote ngawira mtangaze ushindi wa 3 - 0.
Mpira ni dakika 90 sio kelele za huyo jamaa yenu manara. Mtoeni kwanza anaboa sana
 
Mashabiki wa simba ni sawa na wale wazazi masnitch kwa watoto wa majirani. Kutwa wana wananga watoto wa wenzao kuwa wana tabia mbaya, hawana akili nk. Mara mtoto wao anabebea mimba nyumbani au anakula ziro form 4, wanabaki tu na aibu na kuanza kujikosha. Simba jifunzeni kuwa na akiba ya maneno mnachonga sana kabla ya mechi
 
Simba sc ndiyo haswaaa wangoa Viti na vituko vingine uwanjani pindi wazidiwapo maarifa na timu pinzani. Ushahidi upon wa kujitosheleza.
Mnapenda kujisahau
Kati ya simba na yanga yupi mwanzilishi wa kung'oa Viti pale taifa
 
Washabiki wa Yanga hawana upuuzi kama huo,tutake radhi
Usipate shida sana juu ya hilo. Hiyo ndo tabia ya mashabiki duniani kote. Ukiwafurahisha, watakushangilia, ukiwaboa watakuzomea. Ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe. Wahusika wa team kwa maana ya uongozi,benchi la ufundi na wachezaji pia watakua wamepata ujumbe loud and clear; kilichobaki ni wao tu kuufanyia kazi. Jiulize, je ni mara ya kwanza kwa msimu huu simba kufungwa? Kwa nini wazomewe sasa?
"Great power, comes with great responsibilities".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKICHEKA NANGURUWE IPO SIKU WATAINGIA NA WEWE MSIKITINI
WALIWACHEKEA KUPITILIZA
 
Mkuu kuna tofauti gani wewe uliyekuwa una mshambulia Manula kwa makosa ya kibinadamu! Ni heri kuizomea Timu kuliko kumshambulia Mchezaji mmoja ...ina muumiza sana na inaweza ikamharibia kabisa...MBONA HUONI KUNDU LAKO!
Simba siyo manula tu , pamoja na kufungwa uliona akilaumiwa kakolanya ?
 
Kuzomewa kunawafaa sana wanapovurunda... kama kushangiliwa kunavyowafaa wakifanya vizuri.
 
Kwa hiyo mlitaka mtibwa wafungwe kisha wazomewe wao, walishtuka mapema kuna zomeo wakakaza buti😁😁😁
 

Usipate shida sana juu ya hilo. Hiyo ndo tabia ya mashabiki duniani kote. Ukiwafurahisha, watakushangilia, ukiwaboa watakuzomea. Ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe. Wahusika wa team kwa maana ya uongozi,benchi la ufundi na wachezaji pia watakua wamepata ujumbe loud and clear; kilichobaki ni wao tu kuufanyia kazi. Jiulize, je ni mara ya kwanza kwa msimu huu simba kufungwa? Kwa nini wazomewe sasa?
"Great power, comes with great responsibilities".
Kuzomea ni ishara ya hasira, kuchukizwa na kutoridhishwa na alichokifanya mzomewa kwa anayezomea. Lakini tusihukumu kabla ya kujihukumu.

Je, hao wazomeaji ambao sanasana ni wanachama lakini hasa ni washabiki na wapenzi wa Simba wametimiza wajibu wao kwa klabu, kama wachezaji wanaowazimea walivyokwishatimiza wajibu wao? Iweje madogo ya Zanzibar yawahukumu wachezaji dhidi ya makubwa ya Tanzania na Afrika?

Wachezaji wamechangia damu na jasho lao kuiletea ubingwa wa Ligi Kuu misimu miwili mfululizo, wakaifikisha timu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa. Wao wazomeaji wamechangia nini? Walio wanachama wamelipa ada zao? Wapenzi wamejiongeza hadi kuwa wanachama, au angalau wana nia hiyo?

Huwa tunapenda kufananisha uovu wetu kwa matendo ya ‘wenzetu’. Lakini tusifananishe maziwa na tui. Hao ‘wenzetu’ kuzomeana ni sehemu ya utamaduni wao kufikia hata viongozi wa Kitaifa kupopolewa kwa mayai au nyanya mbovu. Tuchague ya kuiga na kufananisha. Mbona tunakataa kwa kauli yenye nguvu maswala ya ushoga na ndoa za jinsia moja zinazopigiwa debe na ’wenzetu’ haohao kuwa ni haki za msingi za mwanadamu?

Ila kwa hili hatuwezi kutomhusisha Manara. Yeye ndiye aliyewajaza wadau wa Simba upuuzi wa kuamini kwamba bila ya kutaka yenyewe, Simba haiwezi kufungwa timu yoyote Tanzania hii. Kama wazomeaji hao walaanika wanakosa akili na utulivu wa kutafakari usahihi wa kauli za msemaji wao, wanawategemeaje wachezaji wawe na akili na utulivu wa kushinda kila mechi ndani ya Tanzania hii?
 
Simba kama wana akili wamfukuze Manara, anafanya udhalilishaji wa kijinga sana kwa Yanga, sasa hivi hakuna utani wa jadi bali ni chuki na kudhalilishana kwenye mitandao ya kijamii, anachofanya sio sawa.
 
Back
Top Bottom