Nani kakwambia naamini hizo bedtime stories?
Wewe na ndevu zako unaamini mtu alitokea na kutoweka? Mtu kasimuliwa na yeye kaja kusimulia na wewe unaamini? Inabidi uwe zwazwa kiasi gani kuamini huu upupu?
Kwa akili zenu nikiwaambia namjua mtu aliyeenda sayari ya Pluto na kurudi mtaamini?
Mtu asikudanganye ukaamini kuwa unachokiona tu kwa macho yako ya damu na nyama ndicho halisi. Kuna mambo yanayoendekea hata hapo ulipo lakini utayaona tu kama utaweza kuona beyond upeo wa macho yako ya kawaida.
Mtu yeyote anayepinga uwepo wa uchawi anaweza akawemo kwenye moja ya haya makundi:
1. Ni mjinga, kwamba hajui kuwa huu ulimwengu unaoonekana ni matokeo ya ulimwengu usioonekana kwa macho ya kawaida isipokuwa tu kwa wale wenye aina ya macho yawezayo kuuona
2. Ni mchawi, na kama ilivyo kawaida ya wachawi wengi, hutafuta kuuficha uhalisia wao. Hawataki watu wajue kuwa wao ni wachawi, na ikiwezekana, hutafuta kuwaaminisha watu kuwa uchawi haupo.
Lakini kwamba uchawi upo, hilo ni jambo linalojulikana kwa wengi.
Binafsi nimeshakutana na matukio kadhaa ya kichawi, madogo kwa makubwa. Mojawapo ni la mwaka 2007 tukiwa Singida ambapo mtu aliingia ndani bila kufungua mlango. Nilimwona kwa macho yangu, na wenzangu nao pia. Lakini baada ya kutamka "KWA JINA LA YESU", alitoweka.
Alienda na kwenye chumba cha wenzetu pia ambacho kilikuwa mbali kidogo na tulikokuwa hivyo wasingeweza kutusukia tukiliongelea hilo. Aliingia kwenye hicho chumba bila kufungua mlango, na akatoweka bila kufungua mlango.
Kesho yake Asubuhi tulipokutana na wenzetu na kuwaeleza kilichotutokea, walitujulisha kuwa na wao walikutana na hiyo hali.
Ni tukio lililoshudiwa na zaidi ya mtu mmoja katika vyumba tofauti. Mimi, kwa macho yangu mawili nililishuhudia hilo, na wenzangu pia. Hakuna namna mtu anaweza kunidanganya katika hilo.
Kama ingelikuwa nimesimuliwa, ningeweza kutilia mashaka. Lakini tukio nililolishuhudia kwa macho yangu mawili nitawezaje kulitilia
mashaka?
Nimeshakutana na mengi zaidi ya hayo lakini hayakuweza kunitisha kwa sababu ninamwamini Mungu.
Uchawi upo, haijalishi kama unaamini au huamini.