royal tourtz
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 255
- 326
Leo nimetoka zangu kutafuta mkate wa kila siku maeneo ya kisesa, nikasema nishuke kwa rafiki yangu hapo kanyama huwa namuita kaka kwa jinsi tunavyoishi.
Nikamkuta shemeji kama kawaida tukasalimiana na kutaka kujua mtoto na dda wa kazi hali zao maana sikuwaona.
Kumbe ndio nawasha moto. Shem akaanza kuniambia dada wa kazi kaondoka mida ya saa kumi na mbili na mda huo ni saa moja na nusu na ameenda na mtoto na hajarudi na hajui yuko wapi, katika kuongea na shem akaniambiamengi mwisho akafikia kwenye hitimisho na kusema atampa mshahara wake ila atamkata nauli aliyomtumia kutoka kijijini na cheji inayobaki ni shilingi 2000, hivyo atampa 2000 na waachane kwa amani.
Nilichosema ,nilimwambia asimfukuze msiku maana anweza pata matatizo na akazua tatizo lingine.
KILICHONIFANYA NIANDIKE NI HIKI.
Nimewaza tu, huyu binti hajaja Mwanza kwa hiari yake. ni wao ndio walimuita aje awafanyie kazi na walimtoa kijijini huko Ghara. Sasa iweje wamkate nauli na wamuache mjini na shilingi 2000 ndio imrudishe au wanafikiri ataishije na kurudi kwao.
Huyo dada wa kazi kipindi wanamchukua hawakujua kama atakuwa na ndugu huku au lah! ili likitokea la kutokea wajue ana sehemu ya kukimbilia sasa kwanini wasimrudishe kwa gharama zao.
Hivi ikitokea huyo dada akapata mwalimu hivi hawezi kumshitaki boss wake na kumuweka kwenye wakati mgumu kisheria maana Mwanza sio kwao na kwa mujibu wa maelezo ya binti ni kwamba kunamtu ni jarani yao huko kijijini naye pia ni dada wa kazi ndio anyemfahamu.
NB nimeshidwa kumwambia yote haya maana nilijua asingenielewa kwa vile alikuwa amekasilika sana nikaona nikae kimya na kweli kwenye saa mbili kasoro dada wa kazi alikuja na mtoto na kweli shem akamwambia jiandae kesho uondoke nakata nauli yako na hapa utakuwa na cheji ya 2000.