Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Unavituko wewe, haya nenda kwa mwamposa.Niliambiwa na X wangu kuwa ile anezaliwa,alipolia alikua ananililia Mimi...Leo hataki hata kuniona .
Kulia kwa mara ya kwanza kwa mtoto ni suala MUHIMU sana. Hii inatokana na ukweli kwamba ni wakati huu ambapo mzunguko wa damu wa mtoto aliyekuwa ndani ya tumbo la mama akitumia mfumo tofauti wa mzunguko wa damu(foetal circuralation) akiogelea kwenye kimiminika (amniotic fluid) ambapo alikuwa akimtegemea mama kupitia kondo la nyuma(placenta) kupata oksijeni, hubadilika na kwenda kwenye mfumo wa kujitegemea mwenyewe/mapafu yake.Habari za Jumapili wadau wote wa JF.
Hili jambo limekuwa likinitatiza kwa muda mrefu- Kwamba mtoto anapozaliwa ni lazima alie na asipolia automatically basi, jitihada zitafanyika ili alazimishwe kulia. Nimewahi kuambiwa kuwa, kulia humfanya mtoto mapafu yake yafunguke kumwezesha kuanza kupumua.
Swali- Kama suala ni kufungua mapafu, je, mapafu hayawezi kufunguka kwa kicheko? Kwanini iwe lazima atoe sauti ya kulia?
Je, hili jambo ni la kisayansi pekee au pia lipo suala la kiroho? Naomba wajuzi wa Mambo ya Kisayansi na Kiroho mnisaidie kupata ufahamu kuhusu jambo hili.