Ni lazima mtoto kulia mara baada ya kuzaliwa?

Ni lazima mtoto kulia mara baada ya kuzaliwa?

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
5,606
Reaction score
7,032
Habari za Jumapili wadau wote wa JF.

Hili jambo limekuwa likinitatiza kwa muda mrefu- Kwamba mtoto anapozaliwa ni lazima alie na asipolia automatically basi, jitihada zitafanyika ili alazimishwe kulia. Nimewahi kuambiwa kuwa, kulia humfanya mtoto mapafu yake yafunguke kumwezesha kuanza kupumua.

Swali- Kama suala ni kufungua mapafu, je, mapafu hayawezi kufunguka kwa kicheko? Kwanini iwe lazima atoe sauti ya kulia?

Je, hili jambo ni la kisayansi pekee au pia lipo suala la kiroho? Naomba wajuzi wa Mambo ya Kisayansi na Kiroho mnisaidie kupata ufahamu kuhusu jambo hili.
 
Mtoto kulia mara tu baada ya kuzaliwa ni katika mambo ambayo husubiriwa kwa hamu kubwa sana na wataalamu wa afya.

Anapolia, ni ishara kuwa ana uwezo wa kupumuwa mwenyewe bila kuhitaji masada.

Huwa tunasema, dakika ya kwanza baada tu ya mtoto kuzaliwa ni dakika ya hatari sana kwa sababu ndani ya hiyo dakika ni lazima mtoto apumuwe kupitia mapafu yake yeye mwenyewe. Akiwa tumboni alikuwa akipata masada wa kupumuwa kupitia muunganiko wa kitovu chake na kondo ( placenta ).

Nini kinatokea ?
Anapolia, hupelekea vifuko vidogo vidogo vya hewa ndani ya mapafu kufunguka kwa mara ya kwanza na kuruhusu hewa kuingia ndani ya mapafu yake kwa mara ya kwanza kupitia uwezo wake yeye mwenyewe na sio vile alivyo kuwa tegemezi kupitia kitovu na kondo alipo kuwa tumboni.

Pia, tumboni mtoto anakuwa amezungukwa na maji ( amniotic fluid ) na hutokea maji haya yakaingia ndani ya mapafu na kwenye pua. Kitendo cha yeye kulia pia husaidia kuondoa maji hayo na hivyo kumuwezesha kupumuwa vizuri.

Ukiachana na kusaidia kwenye mfumo wa upumuaji, mtoto anapo lia pia husaidia kwa kiwango kikubwa kwenye mzunguko wa damu kutoka kwenye moyo na kuelekea kwenye mapafu na sehemu nyenginezo.

NAWASILISHA ✍🏾✍🏾✍🏾
 
Mtoto chini ya miezi miwili hawezi kucheka, anaweza akasmile ila sio kucheka. Kulia sasa 😂😂😂

Au ndio mwanzo mgumu 😂😂😂
 
Habari za Jumapili wadau wote wa JF.

Hili jambo limekuwa likinitatiza kwa muda mrefu- Kwamba mtoto anapozaliwa ni lazima alie na asipolia automatically basi, jitihada zitafanyika ili alazimishwe kulia. Nimewahi kuambiwa kuwa, kulia humfanya mtoto mapafu yake yafunguke kumwezesha kuanza kupumua.

Swali- Kama suala ni kufungua mapafu, je, mapafu hayawezi kufunguka kwa kicheko? Kwanini iwe lazima atoe sauti ya kulia?

Je, hili jambo ni la kisayansi pekee au pia lipo suala la kiroho? Naomba wajuzi wa Mambo ya Kisayansi na Kiroho mnisaidie kupata ufahamu kuhusu jambo hili.
Kulia kwa mara ya kwanza kwa mtoto ni suala MUHIMU sana. Hii inatokana na ukweli kwamba ni wakati huu ambapo mzunguko wa damu wa mtoto aliyekuwa ndani ya tumbo la mama akitumia mfumo tofauti wa mzunguko wa damu(foetal circuralation) akiogelea kwenye kimiminika (amniotic fluid) ambapo alikuwa akimtegemea mama kupitia kondo la nyuma(placenta) kupata oksijeni, hubadilika na kwenda kwenye mfumo wa kujitegemea mwenyewe/mapafu yake.

Presha anayoitoa mtoto kwa kulia huenda kufungua mapafu na kupunguza kiasi cha damu kwenye njia iliyokuwa inamsaidia mtoto kuchepusha damu toka upande wa kulia wa moyo kwenda kwenye upande wa kushoto wa moyo na kuendelea na safari mwilini.

Mabadiliko haya huruhusu damu kwenda kwenye mapafu na hatimaye kufuata mfumo wa kawaida wa milango yake(valves) na vyumba vyake vyote(chambers) kisha kwenda mwilini.

Njia hizo mbadala huendelea kufunga taratibu lwa wastani wa miezi sita, kutokufunga kwake huleta hitirafu kwenye moyo na mzunguko wa damu.

Kucheka au kulia ni matokeo ya ayapatayo kiumbe/mtoto na kutoa vichocheo ambavyo kimsingi wakati wa kazaliwa ni vichocheo hasi/stress ambayo humsababishia mtoto kuwa na mwitikio husika/kulia.
 
Back
Top Bottom